Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, November 3, 2012

AT LAST MEDIA COUNCIL OF TANZANIA (MCT) WAKES UP FROM A DEEP SLUMBER!



BARAZA LA KHABARI TANZANIA MCT LASHITUSHWA NA KUZUIWA VYOMBO VYA KHABARI BINAFSI ZANZIBAR KUZUIWA KUTANGAZA TAARIFA ZA UAMSHO

  • Latoa ufafanuzi kupigwa marufuku kuripoti habari za Uamsho

 03/11/2012
BARAZA LA HABARI TANZANIA MCT LIMESEMA KUWA LIMESHTUSHWA TAARIFA YAKUZUIWA KWA VYOMBO VYA HABARI VYA ZANZIBAR KUTANGAZA KHABARI ZINAZOHUSIANA NA JUMUIYA YA UAMSHO NA MIHADHARA YAKIISLAM ZANZIBAR.
HAYO YAMEELEZWA JANA NA KAIMU KATIBU MTENDAJI WA BARAZA HILO NDUGU JOHN MIRENYI WAKATI AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA KHABARI KATIKA UKUMBI WA MCT MLANDEGE MJINI ZANZIBAR.
BARAZA HILO LIMEONGEZA KUWA LINAAMINI KUWA SI VIZURI KUINGILIAA UHURU WA VYOMBO VYA KHABARI NA WAHARIRI.
AIDHA MIRENYI AMEVITAKA VYOMBO VYA KHABARI VYA TANZANIA BARA NA ZANZIBAR KUFANYA KAZI ZAKE BILA YA WOGA,UPENDELEO NAKUZINGATIA MAADILI NA KANUNI ZINAZOONGOZA UANDISHI WA KHABARI.
AMESISITIZA KUWA LICHA YA BARAZA LA KHABARI TANZANIA KUTAMBUA NAKUTETEA KWA NGUVU ZOTE KUWEPO KWA UHURU WA VYOMBO VYA KHABARI NAKUJIELEZA VYOMBO VYA KHABARI VINA WAJIBU WAKUJIEPUSHA KURIPOTI KHABARI ZA UCHOCHEZI WOWOTE UNAOWEZA KUHAMASISHA CHUKI KWA JAMII NA HATIMAYE KUVURUGA AMANI YA NCHI.
TAMKO HILO LA MCT LIMEKUJA KUFUATIA HATUA YA HIVI KARIBUNI YA TUME YA UTANGAZAJI ZANZIBAR KUPIGA MARUFUKU MATANGAZO YOTE YANAYOHUSIANA NA VURUGU ZINAZOHUSISHWA NA JUMUIYA YA UAMSHO NA MIHADHARA YAKIISLAM ZANZIBAR KWA VITUO VYOTE VYA RADIO NA TELEVISHENI BINAFSI HAPA NCHINI.
KIONGOZI HUYO AMEELEZEA HAJA KWA VYOMBO VYA KHABARI KUZINGATIA UWAJIBIKAJI NA KUWA MAKINI ILI KUEPUKA KUCHOCHEA VURUGU.

Baraza la Habari latoa ufafanuzi kupigwa marufuku kuripoti hbari za Uamsho

Meneja wa Baraza la Habari kanda ya Zanzibar (MCT)  Suleiman Seif Omar akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari hawapo pichani kuhusu tamko la Tume ya utangazaji Zanzibar kupiga marufuku kuripoti taarifa za UAMSHO zenye kuashiria uvunjifu amani kushoto ni Kaimu Katibu Mtendaji wa MCT John P.Mireny.
Kaimu Katibu Mtendaji wa (MCT)John P.Mireny akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa Habari hawapo pichani juu yatamko la Tume ya utangazaji Zanzibar kukifungia chombo cha TVna Radio.
Kaimu Katibu Mtendaji wa MCT John P.Mireny akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa Habari juu ya tamko la Tume ya utangazaji Zanzibar kukifungia chombo cha TVna Radio iwapo kitaripoti habari za UAMSHO zenyekuashiria ufunjifu wa amani .
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifatilia kwa makini juu ya ufafanuzi uliotolewa na Kaimu Katibu Mtendaji wa MCT John P.Mireny huko katika ukumbi wa MCT uliopo Mlandege mjini Zanzibar.
Chanzo: Mzalendo


1 comment :

  1. MCT - This is too late and too little. You have failed Tanzanians in this!

    ReplyDelete