Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, November 3, 2012

MAALIM SEIF AMSHANGAA DR SHEIN!


Kama ni hivi mbele kuna Hatari

 03/11/2012  
Asalamu Alaykum.
Kwa wale wenye facbook wabofye hapa wataona alichokisema lakini ikiwa yaliosemwa leo ndio haya basi mbele yetu kuna khatari http://www.facebook.com/salma.said.9081
Na kwa wale ambao hawana facebook basi labda niandike niwachotee lakini nimechoka kwa hivyo ni haya hapa aliyosema Maalim Seif ingawa sijayaandika kwa utaratibu mzuri kwa sababu nilikuwa akisema naandika pale pale katika mkutano wa leo Kibanda Maiti na wale waliokuwa wakifuatilia facebook ndio watakuwa wamepata kusoma vizuri lakini kama kuna makosa ya typing naomba radhi sana na mtanisamehe kwa sababu sasa hivi nachota na kuweka tu, sitaweza kufanya masahihisho juu ya kile nilichokuwa nikiandika uwanjani nawaomba radhi sana.
Maalim Seif anasema Rais wetu Dk Shein alichukua ahadi kwamba atawalinda raia wote bila ya ubaguzi na alipomuahidi Mwenyeenzi Mungu kwamba atawalinda Wazanzibari na atailinda Zanzibar basi akumbuke ahadi hiyo….tunajua kama ni kutokea vurugu basi ni kurudisha amani lakini tujiulize jeee hatua zilizochukuliwa na kurejesha amani zilikuwa sahihi? Tujiulize je ni kweli ni wafuasi wa Uamsho waliofanya fujo? Na kama ni wao walikuwa peke yao? Je njia zilizotumika kudhibiti fujo ziliendana na kulinda haki za kila mzanzibari? waheshimiwa wananchi naomba niwaambieni kabla ya vurugu hizi taarifa za kuhujumu watu na fujo zilikuwepo kuna watu wanajiita ubayaubaya, mbwa mkali, mbwa mwitu, kimyakimya na hawa wakihujumu watu njiani wanafika pahala mtu kapanda vespa na mkewe ama awache mke au vespa - hayo yamefanyika hayo…chanzo cha vikundi hivi ni janjaweed wenyewe wa CCM wakasema sisi hatuna janjaweed walisema tuna vijana tunaowaandaa kufanya fujo wakati wa uchaguzi. hawa janjaweed waliahidiwa kupewa ajira wapo wachache waliopewa ajira na wengi hawajapewa haya ndio matokeo yao, na sasa wanawafunza watoto wadogo, na vijana hawa makao makuu yao ni hapa ofisi ya mkoa ya CCM …ndio makao makuu yao sasa wanasema na rais kasema basi …basi na hii basi lakini ni kwa watu katika majumba tu?….watu wanateswa katika majumba, watu wanapigwa, wanaibiwa fedha zao na kila balaaa kuna maeneo maalumu bububu, magomeni, kwarara, nyarugusu, mtoni na mote humo masheha wanaonesha askari nyumba za CUF. Dk Shein hivi ndivyo tulivyotaka nchii iwe? mwenzako Dk Karume aliiwacha nchi ikiwa na salama….leo tunarejeshwa nyuma…nasikitika sana sana kumsema rais wangu hadharani….kwa sababu nilikwenda kumwambia hili …hili …hili akanambia inshaallah tutachukua hatua….tukasikia ….siku ya pili nikampigia simu ….nipo Morogoro…na nikamwambia kama hukuingilia wewe mambo yatakwenda hivyo hivyo….na kabla sijamwambia yeye nikazungumza na Dk Mwinyihaji Makame, nikazungumza na Mohammed Aboud na yeye ni muungwana akasema atashughulikia kupeleka taarifa hii kwa kamishna, na salamu zikamfika makamo wa pili wa rais, na mawaziri wa CUF wanataka kuongea na makamo wa pili wa rais siku tatu hawakupata nafasi baada ya siku tatu ndio wakaambiwa njooni….na wakamwambia makamo wa pili wa rais akajidai kushangaa aaaah aaaah haya basi tusubiri kikao cha baraza la mawaziri kikao kipo huko tukae watu wasubiri kupigwa ….mpaka kikao….ninasikitika sana kuwasema wenzangu hadharani lakini inanibidi niseme hivyo na hata ninayoyasema nitayasema popote pale nasema rais wangu ameniangusha ameniangusha …leo rais anatoa hutba anasema maskani ya CCM Kisonge anaacha kusema watu hali zao mbaya wamepigwa na wameumia ….na Kisonge waheshimiwa imechomwa ndani haikuchomwa nje sasa hao wafuasi wa Uamsho wataingiaje ndani kuchoma?.
Maalim Seif anasema gari ambayo imetumika kwa jimbo la bububu ndio hiyo hiyo iliyotumika katika kuchoma kisonge wao ndio waliokwenda hapo wakapiga na kisha wakaiba vyarahani na kisha kutoka, wasidhani atujui tunajua na hata tunafahamu kuna mtu mmoja ametoa geloni la petroli kukachomwe kiwanja cha mbao eti kuna CUF pale, halafu tunaambiwa mbawala imechomwa na watu wamekunywa bia hao ni Uamsho? kamishna twambie….wapo watu pale mkoa kuna watu sio askari sio lolote wana silaha…kuna walinzi wamewekwa hawakujuana kuna polisi hawakujuana wakamuua mmoja wao …semeni kweli msisite semeini kweli msiwazuge wananchi semeni kweli…..mmoja akafa tena aliyekufa alikuwa na silaha na sio askari na ubani kupelekwa na wawili wakajeruhiwa wakalazwa bububu hospitali mbona hamsemi kweli? bure mnakwenda kuwapiga majumbani kwao ..wenye hatia mnawajua…mimi nachukia sana halafu kamishna Mussa anasema anafanya kazi kisayansi ….hiyo ndio sayansi yenu hiyo? hiyo ndio sayansi yenu? yaani kumtafuta asiyehusika mkamuadhibu anayehusika mnamficha….leo hii watu walifika pamoja wananchi wale wa polisi jamii walikuwa wakishiriiana sana na polisi leo hii mmeondosha uaminifu mwananchi gani ataiamini polisi sasa hivi? kwa matakwa ya kisiasa……aaaaah haya leo sina muda…..mheshimiwa Taslima haya mnayoyafanya yanaandaliwa huko kwenu kulikuwa na kikao cha watu wakubwa Dodoma viongozi wote wakuu walikuwemo Rais wa Zanzibar, makamo wa rais, na makamo wa pili alikuwepo the only aliyekuwa hakuwemo ni makamo wa kwanza wa rais hakuwemo kwa nini hakuwemo? sababu eti sheria ilikuwa imetungwa na waziri kiongozi lakini yeyee mpinzani ….kwa nini hivi kweli mlikuwa mna njia njema nyie? lakini nasema kila likuwepokalo lina kheri na wewe nisingeweza kukaa katika kikao hicho kikabariki hata siku moja maana wameamua katika vurugu zilizotokea hatua za polisi hazijachukuliwa kwa hivyo kikao kikaamua kwamba vikosi vyake vyote vifanye kazi na matokeo yake ndio hayo yanafanywa sasa mnapigwa ovyooo maana kama ni fujo bara linafanyika kama ni kuuliwa askari ni jambo baya na pia tunalaani sana na tunawaheshimu sana na mimi IGP tunamheshimu sana na ni the best IGP lakini nasikitika kwamba amekuja hapa anasema kumuua askari mmoja ni kuathiri watu 30,000 lakini Mwanza ameuliwa mkuu wa polisi kwa hivyo ameathiri watu zaidi millioni lakini hebu twambieni wangapi wameingiliwa majumbani na kupigwa? hivi wazanzibari wakikataa muungano kuna ubaya gani? ikiwa mateso tunaofanyiwa tuna sababu gani sisi ya kuutaka huu muungano mnayo sababu nyie?.
Maalim Seif anasema hizi fujo zina malengo matatu, moja ni kuwa wazanzibari wameshashikamana na wapo kitu kimoja na watu wanaogopa umoja wa wazanzibari tulikuwa kitu kimoja, madai pamoja na kauli moja tuliona jinsi gani wazanzibari walivyokuwa wakiitetea zanzibar ikafanywa kuvunja umoja huu lengo la kwanza kuvunja umoja wa wazanzibari na ili ufanikiwe nilileta mti na shoka.
Maalim Seif anasema lengo la pili ni kuiandama serikali ya ummoja wa kitaifa wanandika kisonge kwamba eti umoja basi lakini tunawaambia weeeeee labda wewe tunawaamia serikali is there wewe piga kelele weeee tunawaambia hii ipo pale pale, haiondoki hii imeletwa na wananchi …Maalim Seif ni makamo wa kwanza wa Rais wa nchi hii hakuna atakayeweza kunifukuza katika nafasi yangu labda chama changu, au mwenyeenzi mungu achukue roho yake au mie mwenyewe nichoke lakini rais Shein atafukuza mawaziri wake mimi ananiona hivi hivi …….Maalim Seif maoni ya kura ya maoni ya kuingia serikali ya umoja wa kitaifa yatazameni kwa hivyo wasahau ….aliondoka Hamad Masoud akaja Rashid Seif kwa hivyo msijidanganyeeeeeeeeeeeeeeeeeee.
Maalim Seif– Na lengo la tatu ni vitisho ili watu wasende kutoa maoni lakini kwa ummoja wao tunataka zanzibar irejeshwe mamlaka yake kamili na kisha kuwe na mkataba lakini jambo la kutia huzuni tume watu wakizungumzia muungano wa mkataba wanamhoji na kumzonga halafu wanasema eti ukisema muungano wa mkaaba maana yake muungano haupo tena …sasa Jaji Warioba na wenzako heshimuni mawazo ya wazanzibari mheshimiwa Abubakar tunakwambia hii tume ina mawazo ya upande mmoja wa serikali mbili hizi hizi tunasema hatutaki hilo…..
Na msemaji wa CUF vijana Bwana Khalifa anasema wazanzibari wana majonzi makubwa sana kutokana na majonzi wanayotiwa na serikali yao yanayofanywa na vyombo vya ulinzi na usalama wa nchi hii anasema watu sasa hivi wanahama majumba yao wanapita majumbani na kuwapiga na kuwatesa na kuwaibia fedha zao na simu dvd na mambo mengine vitendo vinavyofanywa na jeshi la polisi, anasema inasikitisha sana.
Khalifa anasema wazanzibari walishasahau mambo hayo lakini wanalazimishwa kurejeshwa katika siasa zilizopitwa na wakati anasema inasikitisha kuona watu wazima wananyolewa kwa nguvu, wanapigwa mbele ya familia yao, anasema vikosi vya ulinzi vinathubutu kuuwa raia wasio na hatia na badae kutoa taarifa za uongo kwa kisingizio eti marehemu alikuwa mvuta unga anasema haya ndio maneno yanosemwa, anasema jee hukumu ya mvuta unga ni kuuliwa hata kama ni kweli,
Khalifa anasema vitendo hivi vinatuma imani kwamba hii ni hujuma kubwa ya serikali ya umoja wa kitaifa ili turudi tulipotoka, anasema tunalazimika kusema hivi kwa sababu jaribio hili lilianzia kwa uchaguzi wa bububu, anasema tukio jengine la kumteka sheikh Farid ni mpango maalumu na kumuuwa askari pale bububu ilikuwa ni mpango wa kufanya haya ili yatokee.
Khalifa anasema hadi sasa ubayaubaya, jangawidi na mbwa mwitu wangapia wamekamatwa hadi sasa? anasema watutajie kama ni kweli wana nia ya kuwakamata na wameshawakamata wangapi? Khalifa anasema hii ni ishara kwama tunapokwenda kubaya, anasema matumaini ya watu kwa serikali ya umoja wa kitaifa yapo njia panda, anasema hatupo tayari kuona zanzibar yetu inasambazatishwa na watu wenye kufuata mabwana zao, sisi wengine hatuna pa kwenda zaidi ya unguja na pemba
Khalifa anasema sisi CUF tunalaani vitendo vyote hivi vinavyofanywa na vikosi vya SMZ na tunaitaka serikali itoe tamko la kusitisha zoezi hili ambalo linawadhalilisha wazanzibari, tunawaambia wana CUF kwamba hili litatuharibia sisi CUF tunaamini kwamba hili haliungwi mkono na CUF na viongozi wake waliopo serikalini, katu hawawezi kututenganisha na kipenzi chetu mpendwa wa watu Maalim Seif.
Khalifa anasema wenye imani kwamba kutupiga na kututesa kwamba eti tutaondosha imani na viongozi wetu tunawaambia kuwa wamechelewa
Khalifa tunasema viongozi wetu wabakie huko huko hadi hapo watakapotuletea serikali yetu yenye mamlaka kamili, tunawaamba wananchi wote wasiingie katika mtego huu, sisi tuwakatishe tamaa tusitoe nafasi wahafidhina na kutuharibia, msimmame wetu yepo pale pale tunataka mamlaka kamili na muungano wa mkataba.
Khalifa ansema salamu zetu zipelekwe kwa Dk Shein kwamba imani tuliompa alipokuwa anaingia madakarani yameanza kundoka na tunamtaka alizingatie sana hili kwani jukumu lake ni kuhakikisha haki za raia zinasimamiwa ipasavyo iwe mkubwa au mdogo
Khalifa anasema tutasimama imara kwa kupigania chama na tutasimamia kikamilfu kwamba wazanzibari wapo imara na tutashirikiana na wenzetu wazanzibari kuitetea nchi yetu kwetu sisi ni zanzibar kwanza na tupo tayari kufa kwa hilo…..hakiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii.
Sasa Phillip Habib Kaimu Katibu Mkuu wa CUF, Salim Bimani si mnamjua Bimani anaanza hakiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii…..zanzibarrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrkwanzaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa Bimani anasema kama Katibu Mkuu wa CUF na Makamo wakwanza wa raia tunakupa salamu hivi peleka serikalini ….anasema Professa Lipumba alisema siku ya Mwafaka kwamba tumesamehe lakini hatujasahau kutokana na dhulma na mateso ya nchi hii, anasema watu kadhaa walikufa ..watu walikwenda kwenye ukimbizi, amani na utulivu tulisamehe lakini hatujasahau …tunaona kwamba vitimbi vinaaza na vidole wanatunyooshea sisi lakini vidole vitano vinaonesha basi na wao vinawanyooshea na wao.Bimani anasema nani mwenye kupiga watu? nani anawatesa watu akina mama na watoto eti wanafanya hivi ili tutoke katika serikali ya umoja wa kitaifa anasema yagujuuuuuuuuuuuuuuuuuuuhatutoki hatutoki hadi tukabidhiwa na serikali kamili sisi waruke watoje hatutoki ….tunawaambia wananchi msichokozeke.
Bimani anasema asilimia 47 wazanzibari wa mkoa wa kusini wametaka muungano wa mkataba na asilimia 75 wanataka dola kamili sasa tume ipo mkoa wa kaskazini 55, tume wete asilimia 91 wanataka mkataba sasa vitendo hivi vinafanywa ili watu wavunjike moyo wasende kutoa maoni lakini tnawaambia mwenyekiti Jaji Warioba kwamba tume yake wajumbe wake mkoa wa kaskazini wakiongozwa na bwana Butiku na Lambat tunasema tume hii haiwatendei haki wananchi leo Mzee Butiku anawanyooshea kifimbo leo hii hii ni dharau gani hiii leo mtu anaposema anataka muungano wa mkataba anamkaripia mpaka anaogopa lakini akisema anataka serikali mbili anafurahi ….asije mambo hayo akatufanyia na kutuletea mjini magaharibi suala hilo kitaruka kivumbi tunamwambia ….tunataka tume ituachie tutoe maoni yetu kikamilifu tusikilizwe na kama tume inavyotaka ….tumechoka tumechoka tunasema tumechoka ….na hili tunasema tumechoka ….tumechoka….tumechoka….lakini wale wapenzi wa serikali mbili wameyaona juzi kule bungeni jeeee mlitaona nyie? juzi wabunge waliuliza huu mgao unakwenda wapi? wakajibiwa kuwa ofisi ya makamo wa pili zanzibar, wakasema kwa kuwa sisi ni wabunge na tuna haki ya kusimamia hizi fedha kwa kuwa mbunge yupo hapa na yeye ni makamo wa pili wa rais yupo hapa basi atupe maelezo…akasimama mama Anna Makinda kwamba hapa huyu ni mbunge wa Kitope na sio Makamu wa Pili wa Rais ….hapa sasa anatushushua mama Makinda hivi hivi ikiwa Balozi ameshushuliwa hapa jeee yupo atakayebakishwa? sasa tusikubali tukilinde na tukivushe kwa salama dau hili tupo imara na inshallah Rais wa Zanzibar atakwenda kukalia kiti chake umoja wa mataifa….tuulizwe tuseme tuyatakayo tusibughudhiwe na msitukaripie…..kama utaniuliza kitunguu mboga au vipi lakini nasema tutaifikisha zanzibar tunapotaka….
Mjumbe wa Baraza Kuu la Taifa, Mwanasheria wa CUF na Mbunge wa Afrika Mashariki, Bwana Taha Issa Taslima anakaribishwa kuja kusalimia anasema hana maneno zaidi ya kuleta salamu kutoka wapenzi wa CUF kutoka Tanzania Bara.
Natanguliza shukrani. Na naomba radhi kwa usumbufu wowote mtakaoupata katika kufahamu nilichoandika.
Salma Said,
P. O. Box 1442,
Tel: +255 (024) 223 5219
Mobile: +255 777 477 101
E-mail: muftiiy@yahoo.com
Weblog: http://zanzibariyetu.wordpress.com
Podcast: http://zanzibaryetu.mypodcast.com


No comments :

Post a Comment