NA MWANDISHI MAALUM
12th December 2012
Jana serikali ilisaini mikataba mitatu ya mkopo wa fedha kutoka Benki ya Dunia. Utiwaji saini huo ulifanywa na Waziri wa Fedha kwa niaba ya serikali ya Tanzania wakati Benki ya Dunia iliwakilishwa na Mkurugenzi Mwakilishi hapa nchini.
Mikataba hiyo ni wa miradi ya kuimarisha serikali za mitaa, wa mpango wa maendeleo ya kilimo na wa tatu ni kusaidia usalama wa chakula nchini, kwa jumla mikataba hiyo ina thamani ya Sh. bilioni 489.8 (Dola za Marekani milioni 310).
Asilimia kubwa ya fedha hizi zinakwenda kwenye mradi wa kuimarisha serikali za mitaa ambazo ni Sh. bilioni 402.9 (Dola za Marekani 255), kiasi kingine cha Sh. bilioni 47.4 (Dola za Marekani milioni 30) zitasaidia kuimarisha kilimo kwa kuwasaidia wakulima kupata pembejeo na kusaidia uwekezaji katika sekta hiyo kwa kuhamasisha uwekezaji binafsi kwa kusaidia kuboresha mazingira ya uwekezaji hasa kwa kutazama sera na taratibu zake.
Eneo jingine ambalo litanufaika ni fedha hizi ni usalama wa chakula ambalo litatumia kiasi cha Sh. bilioni 39.5 (Dola za Marekani milioni 25) nia ikiwa ni kuhakikisha kunakuwa na uzalishaji mkubwa zaidi wa chakula cha kutosha nchini, msisitizo pia ukielekezwa kwa wakulima kupata pembejeo muhimu.Mikataba hiyo ni wa miradi ya kuimarisha serikali za mitaa, wa mpango wa maendeleo ya kilimo na wa tatu ni kusaidia usalama wa chakula nchini, kwa jumla mikataba hiyo ina thamani ya Sh. bilioni 489.8 (Dola za Marekani milioni 310).
Asilimia kubwa ya fedha hizi zinakwenda kwenye mradi wa kuimarisha serikali za mitaa ambazo ni Sh. bilioni 402.9 (Dola za Marekani 255), kiasi kingine cha Sh. bilioni 47.4 (Dola za Marekani milioni 30) zitasaidia kuimarisha kilimo kwa kuwasaidia wakulima kupata pembejeo na kusaidia uwekezaji katika sekta hiyo kwa kuhamasisha uwekezaji binafsi kwa kusaidia kuboresha mazingira ya uwekezaji hasa kwa kutazama sera na taratibu zake.
Kwa viwango vyovyote mikataba hii ni ya fedha nyingi, lakini la umuhimu wa kipekee fedha hizo zinalenga kwenye sekta ambazo zinabeba wananchi wengi, yaani kilimo na huduma ya utumishi katika serikali za mitaa. Kwa mantiki hiyo, ni mikataba stahiki kwa mahitaji na matarajio ya maisha ya wananchi kwa ujumla wao.
Tunapongeza juhudi zote zilizofanywa ili kufanikisha kufikiwa kwa utiliwaji saini wa mikataba hii. Tunasema hivyo kwa sababu duniani kote mahitaji ya fedha ni mengi, hata yale mataifa ya Ulaya ambayo zamani yalidhaniwa kuwa yamekwisha kuvuka ngazi ya kusumbuliwa na matatizo ya kiuchumi, hali siku hizi imekuwa kinyume chake kabisa.
Kwa sasa mataifa ya Umoja wa Ulaya yanahaha kuokoa baadhi ya nchi wanachama ambazo kwa takribani miaka mitatu mfululizo wamekuwa kwenye mdororo mbaya wa uchumi, kila juhudi inafanywa ili kuziokoa, katika mazingira kama hayo mahitaji ya fedha ni ya umuhimu wa kipekee.
Tunapopiga picha huko duniani tunaamini kwamba kila taifa linapambana kupata rasilimali fedha ili kupanga maendeleo ya watu wake na kwa kweli kuyatekeleza kwa wakati, hili linatupa sababu kubwa na ya msingi kupongeza juhudi zote za kufikiwa kwa mikataba hii ambayo kimsingi inaangalia mahitaji halisi ya watu wetu katika kipindi hiki.
Pamoja na pongezi hizi, tunawiwa pia kutoa angalizo juu ya matumizi na utekelezaji wa miradi hii. Itakumbukwa kwamba kwa miaka mitatu mfululizo sasa kiwango cha fedha za serikali zinazotengwa kwenda kwenye serikali za mitaa kwa maana ya halmashauri kimeongezeka sana. Ongezeko hili hapana shaka linazingatia ukweli wa hali halisi kwamba idadi kubwa ya wananchi wetu wanahudumiwa na serikali za mitaa yaani halmashauri.
Kadhalika, kwa miaka mingi ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) imethibitisha pasi na shaka yoyote kwamba ndani ya halmashauri nchini kuna matumizi mbaya ya fedha za umma, kwingineko ni wizi wa wazi kabisa unafanywa na watumishi wa umma. Kelele hizi zimepigwa kwa kipindi kirefu sasa kiasi cha kuibua malalamiko na hali ya wananchi kukata tamaa juu ya uwajibikaji wa viongozi wake.
Tunajua kuna baadhi ya watumishi wamewajibishwa ama kwa kuachishwa kazi, kushushwa vyeo au wengine kufikishwa mahakamani kwa makosa mbalimbali ya matumizi yasiyozingatia kanuni au wizi wa mali ya umma. Pamoja na hatua hizi bado hisia za wananchi ni kwamba kuna kazi kubwa zaidi ya kufanywa katika kujenga uwajibikaji na uwazi kwenye utumishi wa umma hasa ngazi za halmashauri.
Ndani ya halmashauri nyingi miradi mingi imekuwa ikitekelezwa chini ya kiwango ama kutokana na uzembe tu wa usimamizi au kwa makusudi ya wazi yenye nia ya kujinufaisha na fedha za umma. Mambo haya yameathiri sana kasi ya maendeleo nchini, lakini pia yamewanyima wananchi wengi haki ya huduma muhimu ambazo hutolewa na serikali.
Tunajua mikataba ya mikopo iliyotiwa saini na Waziri jana ni ya masharti nafuu, haina riba, kwa maana hiyo inatarajiwa iwe neema kwa wananchi wote, hata hivyo ieleweke kwamba kama utekelezaji na usimamizi wa miradi hii hautakuwa wa makini fedha hizi hazitakuwa na maana katika kubadili maisha ya watu wetu. Ni kwa msingi huo sisi tunaiambia serikali kuwa fedha hizi zinahitaji uwajibikaji makini na wa kina.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment