Mzee Mwanakijiji akiwa maskini na taabani wa fikra za maana!
“Tanganyika haihitaji Zanzibar na haiitegemei
Zanzibar kwa chochote. Ni kwa sababu hiyo naamini ili kuharakisha Zanzibar
kujitoa na viongozi hawa wapigania uhuru kuweza kupata nafasi ya kuongoza taifa
la Zanzibar natoa pendekezo kuwa kwa ukarimu wetu kutoka Tanganyika tutenge
shilingi bilioni 400 hizi ili kuwasaidia Zanzibar kuanza maisha mapya wao
wenyewe. ...... Nina uhakika bilioni 400 ni fedha nyingi sana ambazo
Wazanzibari watashukuru.”
Hayo aliyaandika Mzee Mwanakijiji kwenye
moja ya nyaraka zake potofu za huko
nyuma.
Tunaelezwa kila siku na wazee wetu kuwa uendawazimu upo
wa namna nyingi. Mzee Mwanakijiji ni mwendawazimu wa aina yake peke yake!
Hivyo Mzee Mwanakijiji anaona TShs 400 billion ni hela
nyingi sana? Kama ingelikuwa ni hivyo basi Tanganyika leo ingelikuwa ni pepo, kwasababu
imezipata hela kama hizo zaidi ya mara mia. Ziliopo Uswiss tu peke yake ni mara 1000 ya hizo
billioni 400.
Mzee Mwanakijiji ni mwendawazimu chakari na hafahamu kuwa
mchango wa Zanzibar katika kuanzisha BoT peke yake ni zaidi ya trillion moja,
kwa hela za sasa. Labda Mzee Mwanakijiji atakuwa sawa na wale ambao hawajui
nani waliochangia kuianzisha BoT.
Kama Mwanakijiji ndio ameamua kwa
ukarimu wake kuilipa Zanzibar, basi hayo malipo yasiwe 400 billion, lakini yawe kwa kila alichokipata
au kukipokea (tokea 1964) kwa jina
la Tanzania akigawe nusu kwa nusu
baina ya Zanzibar na Tanganyika na sio kutoa 400
billion tu, wakati yeye amechukuwa zaidi ya hizo katika hio miaka yote. Pia
atoe dividend ya 11.2% kwa kuilipa Zanzibar tokea kuanzishwa kwa BoT mpaka leo.
Mwanakijiji anaendelea kuandika kuwa eti Tanganyika
haihitaji ZNZ! Well, he can write anything to enthrill himself, but the
truth is: Kama sio Zanzibar maeneo ya Kariakoo mpaka leo yangeliendelea kuwa madimbwi
ya maji machafu. It was us
Zanzibaris who turned the small dilapidated mud houses of Kariakoo into
beautiful buildings and changed the area into a business centre. That can’t be refuted
by any person who is in his proper senses!
Bara needs Zanzibar more than Zanzibar needs Bara.
Zanzibaris are today one of the economic engines of Mainland. Take us out of Mainland and one of your economic
engines is stalled at the middle of the road. This is the truth that Mzee
Mwanakijiji ought to know!
......bilioni 400 ni fedha nyingi sana? Well, Mzee Mwanakijiji, if so, then you can keep it. Tunacholilia
Wazanzibari sio pesa, bali uhuru wa kuweza kuamua mambo yetu wenyewe bila ya
kuja Bara kupiga magoti!
By Bakari Pandu

No comments :
Post a Comment