TANZANIA RED RIBBON FASHION
GALA 2012
02 Dec 2012 08:51 AM PST
Mc's wa Onyesho la Mavazi la Red Ribbon Fashion Gala 2012
Abby Plaatjes na Evance Bukuku wakikaribisha wageni na
kutoa utaratibu wa shughuli nzima katika Hoteli ya
Mwanamitindo wa Kimataifa nchini na Balozi wa Tanzania
Mitindo House (TMH) Flaviana Matata akifungua maonyesho
hayo na vazi la Ubunifu wa Khadija Mwanamboka.
Pichani Juu na Chini ni Models wakionyesha mavazi mbalimbali yaliyobuniwa kutokana na Vitenge vilivyotengenezwa na Kiwanda cha Vitenge cha Morogoro Polytex ambacho ni moja wapo ya Makampuni ya MeTL.
Msanii wa muziki wa Kizazi kipya Linex akiimba wimbo maalum
wa kuhamasisha jamii kusaidia watoto yatima na wanaoishi
kwenye mazingira magumu kwenye onyesho la Tanzania
Red Ribbon Fashion Gala 2012.
Muasisi na Mwenyekiti wa Tanzania Mitindo House Bi. Khadija
Mwanamboka (kulia) akimkabidhi cheti ushiriki kwa Meneja Masoko
wa CFAO MOTORS Tharaia Ahmed (katikati).
Mwakilishi wa Kiwanda cha 21 CENTURY TEXTILE kinachotengeneza
vitenge vya Morogoro Polytex kilicho chini ya Kampuni za Mohammed
Enterprises Tanzania Ltd. (MeTL) Bw. Cosmas Mtesigwa akipokea
cheti cha ushiriki kutoka kwa Bi. Khadija Mwanamboka.
Morogoro Polytex ni kiwanda cha kuzalisha vitenge na chenye uwezo wa
kuzalisha mita milioni 100 kwa mwaka na ndicho kiwanda kikubwa kwa
sasa katika ukanda wa eneo la Afrika Mashariki.
Mwenyekiti wa Flaviana Matata Foundation Bi. Flaviana Matata
akipokea cheti cha heshima kwa kushiriki kwenye onyesho la
Tanzania Red Ribbon Fashion Gala 2012 ambalo limefanikiwa
kukusanya kiasi cha Shilingi Milioni 72 kwa ajili ya kuwasaidia na
kuwaendeleza watoto yatima wa kituo cha TMH wakiemo
wenye kuishi na virusi vya Ukimwi.
Chanzo: Vijimambo
|
No comments :
Post a Comment