Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, December 18, 2012

PROF/ LIPUMBA ANENA

Written by   //  18/12/2012

Mwenyekiti  wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, ameita Tume ya Mabadiliko ya Katiba inayoongozwa na Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba, kuleta katiba mpya itakayotokana na maoni ya wananchi na siyo iliyo ‘mfukoni’.
Alisema hayo wakati akifungua kikao cha Baraza Kuu la Uongozi wa CUF, jijini Dar es Salaam jana.
“Tume ya Warioba tunataka ituletee katiba ya kweli na itakayotokana na maoni yetu. Isiwe iliyochakachuliwa kama, ambavyo inasemekana sasa kwamba, tunatoa maoni ya katiba, lakini iko tayari. Hivyo, tunafanya biashara kichaa,” alisema Profesa Lipumba.
Alisema katiba ijayo iwe na usawa katika suala zima la Muungano, kwani Wazanzibari wanaukataa Muungano kutokana na kutokuwa na usawa, hivyo akataka ipatikane katiba itakayoridhisha pande zote mbili na kusema bila hivyo, Muungano hautadumu.
“Kwa katiba tuliyonayo unaweza ukawa na chama kikashinda uchaguzi na kuunda serikali ya Muungano bila kuwa na mwakilishi mmoja kutoka Zanzibar. Ndiyo maana Wazanzibari wanakuwa na wasiwasi mkubwa na suala zima la Muungano,” alisema Profesa Lipumba.
Alisema muda wa kutoa maoni wa miezi 18 ni mfupi, kwani katiba ni kitu kinachohitaji muda wa kutosha pasi na kuwa na papara ili kuepuka kupatikana kitu kitakachowagawa Watanzania.
“Tuige mfano wa majirani zetu Wakenya, ambao walianza mchakato wa katiba miaka ya 1990 na kupata katiba yao mwaka 2010,” alisema.
Chanzo: Mzalendo

No comments :

Post a Comment