Written by Abdul // 19/12/2012
WANANCHI wapatao laki 2 wamehudhuria mikutano tofauti ya kutoa maoni ya mabadiliko ya Katiba katika Mkoa wa Mjini Magharibi.
Kati ya hao 93,000 ni wanaume na 110,000 ni wanawake tokea Tume hiyo iaze kazi ya kukusanya na kuratibu maoni kwa mkoa huo.
Hayo yamethibitishwa na Mjumbe wa Tume ambaye ni kiongozi kwa timu iliyokuwako katika Mkoa huo, Profesa Mwisiga Baregu wakati akifunga rasmi shuhuli iliyowaweka Zanzibar kwa mwezi mmoja katika Viwanja vya Masumbani.
“Kwa ujumla zoezi la kukusanya maoni kutoka kwa wananchi sasa limemalizika, ila imebakia kwa makundi maaalumu pamoja na Taasisi za Kidini pamoja na vyama vya Siasa,” alisema Baregu.
Baregu alisema kwamba wananchi waliotoa maoni kwa kuzungumza ni 6000 ambapo wanaume walikuwa 2,242 na wanawake 2,759.Pia Baregu alisema watu walitoa maoni yao kwa kuandika Fomu maalumu za Tume nao walikuwa 15,468 kati yao walikuwemo wanawake na wanaume.
Wakati huo huo, mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Nchini, Profesa Mwaisige Baregu alisema vyama vya siasa vimeliteka zoezi la kukusanya maoni visiwani Zanzibar.
Baregu aliyabainisha hayo katika Viwanja vya Masumbani Shehia ya Kilima Hewa Mkoa wa Mjini Magharibi.
Baregu aliyabainisha hayo katika Viwanja vya Masumbani Shehia ya Kilima Hewa Mkoa wa Mjini Magharibi.
Baregu alisema maoni waliyoyapata mengi ni yale yanayotaka mabadiliko au kuendelea kwa mfumo wa Muungano hapa kati ya Zanzibar na Tanganyika.
“Ni wazi kwamba haya ni mawazo ya wanasiasa kwani unapokwenda popote katika vitongoji ambavyo nimezunguka mimi basi maoni ni hayo hayo,” alisema Baregu.
Baregu alieleza kuwa walichokifuata Zanzibar sicho ambacho walikuwa wanakipata kutoka kwa wananchi mbalimabli visiwani humu.
Baregu alieleza kuwa walichokifuata Zanzibar sicho ambacho walikuwa wanakipata kutoka kwa wananchi mbalimabli visiwani humu.
“Hutukuja kuchukua maoni ya aina gani mfumo wa Muungano uwe lakini ndio maoni ambayo tulikuwa tunayapata kwa wananchi wa Zanzibar,” alisema Baregu
Hata hivyo aliwashukuru sana Wananchi wa Mkoa wa Mjini Magharibi kwa kujitokeza kwao katika kutoa maoni.
Hata hivyo aliwashukuru sana Wananchi wa Mkoa wa Mjini Magharibi kwa kujitokeza kwao katika kutoa maoni.
Source: Mzalendo
No comments :
Post a Comment