Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, December 25, 2012

Tusherehekee Krismasi kwa amani na utulivu

NA MWANDISHI MAALUM

25th December 2012


Maoni ya Katuni
Leo Wakristo nchini wanaungana na wenzao duniani kusherehekea sikukuu ya Krismasi ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo zaidi ya miaka 2,000 iliyopita.

Maadhimisho hayo yatakwenda sambamba na ibada katika sehemu mbalimbali za kuabudia pamoja na burudani zitakazofanyika kwenye kumbi za starehe, fukwe na sehemu nyingine za mikusanyiko leo na kesho kwa ajili ya Boxing Day.

Ili kufanikisha maadhimisho hayo, panahitajika kuwapo kwa hali ya amani na utulivu kwa kuwa kinyume chake maadhimisho hayatakuwa na maana.

Kwa maana hiyo kila mmoja bila kujali kama ni Mkristo anapaswa kuhakikisha anajiepusha na vitendo ambavyo vinaweza kuvuruga amani na utulivu wakati wa maadhimisho hayo. 

Mara nyingi wakati wa maadhimisho ya sikukuu za Krismasi, Pasaka na Iddi, wahalifu wamekuwa wakitumia fursa hiyo kufanya vitendo vya uhalifu vikiwamo kuwapora mali watu na kuwajeruhi.

Katika kudhibiti vitendo hivyo vya uhalifu, tunaamini kuwa Jeshi la Polisi litajipanga vya kutosha kuhakikisha unakuwepo ulinzi wa kutosha ikiwezekana kuimarisha doria katika maeneo yote ya nchi yetu hususani katika maeneo ya ibada, burudani na katika mikusanyiko kwa ajili ya maadhimisho hayo.

Tunachukua fursa hiii kuwashauri wananchi kuchukua baadhi ya tahadhari ili kuepukana na uwezekano wa ajali na matukio mengine yanayoweza kusababisha madhara.

Wazazi wahakikishe wanawadhibiti watoto wao wasiende kuogelea katika maeneo ya fukwe na kama watawaruhusu basi wawafuatilie kwa karibu kwa kuwa watoto kadhaa wamepoteza maisha yao kutokana na kuzama wakati wakiogelea kwenye maeneo ya fukwe. Lakini pia wazazi na walezi wawadhibiti watoto kuzurura barabarani ili kuwaepusha kugongwa na magari.

Wamiliki wa kumbi za disko  wachukue tahadhari kuhakikisha kuwa kuna hewa ya kutosha ili kudhibiti uwezekano wa kutokea kwa maafa kama ilivyotokea katika ukumbi mmoja wa disko mjini Tabora miaka michache iliyopita wakati wa maadhimisho ya sikukuu ya  Iddi.

Ikiwezekana wazazi na walezi wa watoto wafuatane nao katika Toto disko kuhakikisha wanacheza salama.

Vuile vile, tunawashauri madereva wachukue tahadhari kwa  kujiepusha na ulevi kwa kuwa ulevi unachangia sana katika ajali zimekuwa zikitokea wakati wa sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya na kusababisha maafa.

Wakati wa sikukuu madereva wengi hupenda kunywa pombe kupindukia na kuendesha magari jambo ambalo ni kinyume cha sheria za usalama barabarani na matokeo yake ni ajali zisizo za lazima  zinazogharimu maisha ya watu. Katika kudhibiti hali hiyo, Kikosi cha Usalama Barabarani kitapaswa kujipanga na kuchukua hatua stahiki dhidi ya maderava wanaokaidi.

Kadhalika, itakuwa vizuri kama watu watajiepusha na unywaji wa pombe kupita kiasi kwa kuwa ulevi ni sababu kubwa inayochangia matukio ya uvunjifu wa amani.

Baadhi ya watu huamini kuwa sikukuu haiwezi kufana bila kulewa. Huu ni mtazamo finyu na uliopitwa na wakati kwa kuwa maadhimisho ya sikukuu za dini yanakwenda sambamba na matendo mema yakiwemo ya kupendana na siyo ulevi na mambo mengine yanayoweza kusababisha chuki, ugomvi  na uhasama.

Tunaamini kuwa kila mmoja kwa wakati wake akiuzingatia ushauri huu tutaisherehekea sikukuu ya Krismasi kwa amani na utulivu.

Tusherehekee kwa kuzingatia mambo yote yanayoashiria upendo na kwa kuzingatia sheria za nchi.

Tunawatakia Watanzania wote Krismasi njema, lakini tunawashauri kuwa tusherehekee kwa amani na utulivu.


CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment