Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, December 24, 2012

Umakini wa Zitto tumaini kwa Taifa (5)



Na Gladness Mboma

WAPENDWA wasomaji wa makala hii nina imani kila mmoja anaendelea kuifuatilia kwa makini na leo nitaendelea na sehemu ya tano inayohusiana na mahojiano kati ya wanachama wa Jamii Forum na Mbunge wa Kigoma Kaskazini,Bw. Zitto Kabwe kuhusiana na mambo mbalimbali yanayohusiana na siasa

SWALI:Mkuu Zitto ningependa kujua kitu kingine kutoka kwako. Katika Mabadiliko ya Katiba yanayokuja kuna uwezekano mkubwa wa MAWAZIRI wasitokane na nafasi za UBUNGE. Kwa muono mwingine wewe umetangaza kutogombea ubunge jimboni kwako.

Hii inaweza kuchukuliwa kuwa unawinda UWAZIRI kwa kulifikiria hili?

JIBU:Duh, umewaza mbali hata mimi sikuwa nimewaza hivyo. CHADEMA ikishinda niwe au nisiwe Mbunge ninaamini nitakuwa Waziri ili kuweza kutekeleza mabadiliko tunayohubiri katika harakati.

Nimetangaza kutogombea Ubunge, kwanza kuomba ridhaa ya chama changu kuwa mgombea Urais na hilo lisipowezekana nitakuwa mpiga debe wa mgombea Urais. Sitaki itokee tena yaliyotokea mwaka 2010 ambapo mgombea Urais alibaki mpweke kwani kila mtu alikwenda kugombea Ubunge.

SWALI:Je, utaratibu wa sasa wa bunge la JMT wa kupiga kura kwa kuuliza wanaosema NDIYO na wanaosema SIYO ni sawa na unakidhi matwaka ya kidemokrasia uendelee au ubadilishwe? Kwanini?

JIBU:Kuna mashine ya ki elektroniki za kupiga kura ndani ya Bunge. Nadhani tuanze kutumia hizo ili pia kuweka rekodi za wabunge kuhusu kura zao. Itasaidia sana kujua misimamo ya watu kwenye masuala mbalimbali ya nchi.


SWALI:Nini msimamo wako juu ya uwepo wa wabunge zaidi ya 100 wa viti maalum ambao kimsingi wanaligharimu Taifa mamilioni ya fedha?

JIBU:Naunga mkono mfumo wa uchaguzi utakaohakikisha kuwa vyombo vya maamuzi vinakuwa na uwiano sawia wa wanawake na wanaume. Napinga mfumo wowote wa upendeleo maana inadhalilisha.

Hivyo Katiba mpya ifute mfumo wa viti maalumu na kuweka mfumo wa uchaguzi utakaohakikisha vyombo vya maamuzi vinakuwa na wanawake na wanaume kwa uwiano sawia. Mimi ni muumini wa mfumo wa Uwakilishi wa uwiano (Proportional Representation).

Nchi za scandinavia zina mfumo mzuri sana wa uwiano ambapo viti vya Bunge vinapatikana kutokana na uwiano wa kura ambazo kila chama kimepata. Sio lazima tufuate mfumo wao, tunaweza kuwa na mfumo mchanyato. Ujerumani wanafuata mfumo mchanyato na kuna wabunge wengi tu wanawake.

Rwanda pia imefanikiwa kuwa na wanawake wengi sana Bungeni ingawa inabidi kuwa makini kufuata mfumo wa Rwanda demokrasia yao ina mashaka kidogo. Hata hivyo kuja jambo la kujifunza.

SWALI:Kuna taarifa kuwa CCM inatumia vyombo vya ulinzi na usalama katika kuudhoofisha harakati za vyama vya upinzani, na hasa CHADEMA. Mheshimwa Zitto, una mtizamo gani katika hili?

JIBU:Ni kweli kabisa. CCM inatumia sana vyombo vya dola kumaliza upinzani. Hata hii ya kugawa wanachama na kupakaza matope baadhi ya viongozi ni kazi ya usalama wa Taifa.

Wanapandikiza chuki ili viongozi tusiaminiane. Viongozi vichwa maji wasiojua kazi ya usalama wa Taifa wanafurahia mambo haya kumbe wanatumika
Mhe, kuelekea uchaguzi wa mwaka 2010 gazeti la MwanaHalisi lilichapisha mawasiliano ya simu baina yako na ndg Jack Zoka wa TISS, mpaka leo sijasikia sehemu ukikanusha; kwakuwa hakuna kanusho toka kwako, unaweza kutueleza mazungumzo yenu yalihusu nini?.

Naomba nikusahihishe kwamba MwanaHalisi walichapisha mawasiliano hayo baada ya uchaguzi. Suala hili nimeshalisemea sana.

Kwanza ni kweli mimi ninawasiliana na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama wakiwemo TISS, Polisi, TAKUKURU na hata JWTZ. Kama kuna kiongozi yeyote wa nafasi kama yangu ambaye hafanyi mawasiliano na watumishi hawa wa Umma basi kiongozi huyo hafai kuwa Kiongozi.

I challenge mtu yeyote aseme kama kuna kiongozi yeyote wa vyama vya siasa ambaye hafanyi mazungumzo na watu wa usalama nk. Jambo la msingi ni mazungumzo mnayoyafanya yanahusu nini? Yanahujumu chama?

Niliwaambia viongozi wangu wa chama kwenye vikao vya chama kuwa kama kuna chembe ya hujuma kwa chama kwenye mazungumzo yangu na watu kama Zoka basi nitaachia nafasi zangu zote uongozi kwenye chama na Ubunge.

Nikawaambia wale waliosema wanao ushahidi wa mazungumzo hayo wayaweke wazi. Sio MwanaHalisi wala washirika wa MwanaHalisi waliofanya hivyo.

MwanaHalisi ilikuwa inafanya kazi ya siasa za ndani ya chama. MwanaHalisi walikuwa na ajenda yao dhidi yangu. MwanaHalisi waliamua kunimaliza kisiasa. Hata hivyo kwangu mimi hayo yamepita ni historia.

Mazungumzo yetu yalikuwa yanahusu nini? Yalikuwa yanahusu nchi. Watu wa Usalama wanasema tunawashambulia sana kwenye mikutano yao na wao sio wanasiasa kwa hiyo mara

Tusiwataje taje. Mara zote nawaambia tutawataja pale ambapo wao wanahusika na kwamba hawapaswi kuhusika na CCM maana wao wanapaswa kulinda dola na sio kulinda CCM.

Wakati nipo Mwanza mapema mwaka 2011 palitokea mauaji ya raia yaliyofanywa na polisi kule Arusha, viongozi wetu wakakamatwa.

Mmoja wa waliokamatwa ni Mzee Ndesamburo, mzee wa zaidi ya miaka 75 na wakawa wanamweka katika mazingira mabaya, niliwapigia watu Usalama kuwaambia kuwa hayo ni makosa.

Wamwache mzee yule na wanataka kumshikilia wamshikilie nyumbani kwake, sheria zinaruhusu.

Wakati mwingine watu wa usalama wana shida zao pia maana wao ni Watanzania kama sisi. 


Itandelea

Chanzo: Majira

No comments :

Post a Comment