Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, December 27, 2012

ZANZIBAR: SUZA wafikirie kuanzisha shahada (degree) ya Biotechnology

Written by   //  27/12/2012
Nimatumaini yangu makubwa kwamba  wahusika na wadau wa State University of Zanzibar (SUZA) wanatembelea na kusoma yanayoandikwa hapa Mzalendo.Nachukuwa nafasi hii  kumpa pongezi za pekee Vice chancellor, Prof.Rai  na timu yake yote kwa jitiahada zao za kujitolea katika kukipeleka mbele chuo chetu hichi (SUZA) ili kiweze kufikia malengo waliyojiwekea kwa manufaa ya Zanzibar na watu wake.  Najisikia fahari kubwa sana kuona SUZA, chuo pekee cha wananchi wa Zanzibar kikiwa kina songa mbele kwa hatua za haraka!  Nikiwa kama mzanzibar najihisi  nna deni la kuchangia katika kuiwezesha SUZA kutimiza ndoto zake za kuwa “ catalyst for  social change”.  Nnalo deni kwa Wazanzibar wenzangu kuhakikisha SUZA inafikia matarajio na kukidhi haja za wazanzibar hawa waleo na wakizazi kijacho. Hivyo kwa nafasi yangu ya sasa nianze japo kwa kuchangia kimawazo katika kufikia hayo. 
Nimesoma sehemu mbali mbali katika blogs na magazeti hotuba ya Pof . Rai na ile ya Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini, Mzee Moyo. Nimefurahi kusoma kwamba siku zijazo, SUZA wanatarajia kuanzisha shahada za masomo mbali mbali, kama vile Sayansi ya mazingira, sayansi ya bahari na skuli ya medicine. Hii ni hatua kubwa na yakusifiwa na kila mzanzibar na asie mzanzibar anaeitakia mema Zanzibar. Wote tunajuwa umuhimu wa kuwa na wataalamu wetu wenyewe katika fani hizo.
Pamoja na umuhimu wa wataalamu wa fani hizo zinazotarajiwa kuanzishwa mapema miaka ijayo! Nami napenda niwashauri wadau wa SUZA akiwema VC, Prof Rai, na DVC academic, kaka yangu Dr. Haji Mwevura, nawaomba wafikirie na waweke katika mikakati yao ya miaka 2-3 ijayo ya kuanzisha shahada ya Biotechnology. Biotechnology si field mpya sana kwa nchi zilizoendelea kama vile USA,China, Japan, nchi za ulaya na hata India. Lakini field hii ni mpya kwa nchi za Afrika.
Kwa mara ya kwanza East afrika ilianzishwa chuo kikuu cha Dar es salaam mwaka 2003! Mpaka mwaka huo wa 2003 kwa nchi zilizoko kusini mwa afrika ilikuwa ni South Afrika na Tanzania tu ndio wenye field hiyo. Mpaka hivi sasa ni vyuo vikuu viwili tu kwa Tanzania wanavyotoa degree ya Biotechnology,  ni SUA na UDSM!  Pamoja na upya wake barani  afrika,  lakini mahitaji yake ni makongwe sana, pengine tangu mwanzo wa dunia!
Biotechonology ni usanifu wa kutumia mifumo ya viumbe hai na viumbe vyenywe ( binaadam, bacteria, virus, fungus, panya n.k) ili kutengeneza products zenye manufaa au matumizi yoyote ya kiteknologia  yanayotumia  mifumo ya viumbe hai, viumbe hai au vinavyotokana na viumbe hai kwa ajili ya kutengeneza au kurekebisha products au processes kwa matumizi maalum.  Biotechnology inauwanda mpana sana, kuanzia kwenye mazingira (Environmental Biotechnology), viwanda (Industrial Biotechnology), afya (Medical Biotechnology) na kilimo (Agricultural Biotechnology).
Mh. Rais wa Zanzibar Dr. Ali Shein, kwenye mahafali ya nane ya SUZA, alishauri SUZA inzingatie mahitaji ya elimu yanayohitajika kwa maendeleo ya Zanzibar. Wataalamu katika specialization zote hizo za Biotechnology nilizo zitaja hapo juu wana hitajika na wazanzibar wakawaida moja kwa moja katika maisha yao ya kila siku. Ntarudia kuelezea umuhimu wa kila field kwenye paragraphs zijazo.
Kwanini SUZA tunahitaji uwepo wa Department ya Biotechnology na shahada yake?
1. Kama nilivyogusia hapo awali, hii ni fani mpya kwa Afrika, lakini mahitaji yake ni ya muhimu sana na makongwe, ni mahitaji yanayogusa mataifa yote yaliyo endelea na yanayoendelea. Hivi sasa kuna tafiti mbali mbali  duniani za Bitechnology zinafanywa ili kutatuwa matatizo makubwa yanayoikumba dunia. Kuanzia “global warming” linalo sababishwa na uzalishaji wa green house gases kama vile methane n.k, upungufu wa maji, uchafuzi wa mazingira (uwepo wa maji taka, taka ngumu ambazo ni degradable kama mataka ya sokoni na majumbani na taka ambazo si degradable kama mifuko ya plastiki), uwepo wa bioterrorisms (ugaidi wakutimia biological weapons), uzukaji wa maradhi ya kuambukiza (kama vile Ebola), upungufu wa chakula n.k.
Kutokana na kugusa maisha ya kila taifa, tafiti  katika field hii zinapata support kubwa sana ya kifedha na kitaalam kutoka mataifa ya nje na organizations zake, kama vile World Bank, SIDA, FAO, FDA (USA) n.k Hivyo basi uwepo wa department ya Biotechnology hapo SUZA kutavutia wafadhili wamashirika na mataifa mbali mbali ambao watatoa funds (fedha) ambazo zitawezesha kufanya researches mbali mbali kwa ajili ya kutatua matatizo yanayoikabili Zanzibar na dunia kwa ujumla, pia itapata fedha zakujiendesha bila kusahau scholarships mbali mbali! 
2. Uanzishwaji wa Biotechnology hapo SUZA, kutapelekea baada ya miaka michache ijayo kuwa na wataalam watakaoweza kutumia maarifa kutokana na fani hiyo ili kutatuwa tatizo la uchafuzi wa mazingira kama vile maji taka kutoka majumbani na viwandani linalopelekea uchafuzi mkubwa wa mazingira.  Dunia sasa inatafuta njia kwakutumia Biotecnhology ili  kugeuza maji taka hayo kuwa chanzo cha kuzalisha nishati mbadala (biogas) ambayo hutumika kuendeshea magari badala ya petrol au diesel (mfano Sweden).
Pia kwa kutumia wataalam wetu hao tutafikia hatuwa ya kuzalisha biodegradable plastics (bioplastics) zitakazo ondoa matumizi ya mifuko ya plastic hii ya sasa. Bioplastics hazitakuwa zinachafua mazingira kwani huoza kwenye ardhi kama yaozavyo mataka ya muhogo, viazi au sheli sheli. Pia tutazalisha bioethanol na products nyengine kutoka kwenye mataka  magumu ya majumbani na masokoni. Bioethanol  inategemewa kuwa mbadala wa petrol na diesel kwa kuendeshea mashine, mitambo na magari (mfano Brazil na USA)! Ni nishati rahisi na renewable. 
3. Tukiwa tunazungumzia mapinduzi ya kilimo (modern agricultural), kamwe hatutaweza kufikia huko kama hatuna wataalam waliobobea kwenye agricultural Biotechnology. Uingizaji, uzalishaji, utumiaji na uzuiaji wa matumizi ya mbegu zilizoboreshwa kijenetik (genetically modified seeds), unahitaji  uwepo wa wataalam wazalendo katika fani hiyo. Bila ya wataalam hao, tutaendelea kuwa wategemezi katika kilimo cha kisasa. Lakini pia hatutakuwa na uwezo wakuzalisha mbegu bora kulingana na mahitaji yetu. Hasara kubwa tutageuka kuwa jaa la genetically modified products (GMO) ambazo hatutakuwa na uwezo wa kuzi control, maana hatuna wataalam! Ingawa sisi ni visiwa, lakini hatujajitenga na dunia. Madhali duniani wana advance katika matumizi ya Biotechnology, basi sisi tutakuwa waathirika wa ‘negative outcomes’ za Biotechnology kama hatutakuwa na wataalam wa Biotechnology ambao pia watakuwa na uwezo wa kutengeneza sera (policy) juu ya matumizi sahihi na udhibiti wa matumizi hasi ya Biotechnology. 
4. Mbinu za kukabiliana na maradhi mapya na makongwe yanayoangamiza watu wetu zinahitaji uwepo wa technology ya hali juu. Daktari iliaweze kutoa tiba sahihi anahitaji majibu sahihi ya vipimo. Dunia hivi sasa inaondoka katika diagnosis ya mogonjwa kwa kutumia traditional  techniques, kama vile bacteria plate count, biochemical test n.k. Techniques hizi, hazikidhi haja ya maradhi ya hivi sasa kutokana na kubadilika (mutation) kwa vimelea vinavyosabisha maradhi tofauti, kama vile UKIMWI, TB, n.k. Hivyo basi dunia inaenda kwenye matumizi ya  biotechnological techniques kama vile PCR na DNA-biosensors (ambazo zinahusisha gene za vimelea husika) au immunosensors (ambazo  zinahusisha antibodies kutoka kwa mgonjwa).
Vile vile Zanzibar tunawagonjwa wengi wanaosumbuliwa na maradhi ya cancer hasa katika miaka hii ya karibuni, cancer kama itagundulika katika hatua za awali inaweza kuzuiwa isienee, na hivyo kuokoa maisha ya mgonjwa. Lakini diagnosis yake katika hatua za awali inahitaji biotechnological techniques na wataalam katika field ya medical biotechnology. Hivyo basi uwepo wa Biotechnology hapo SUZA utasaidia sana maendeleo katika sekata ya afya na kuzuia maradhi, kutibu na kuokoa maisha ya wazanzibar. Si hivyo tu pia kutawezesha hata ku-develope technology inayoweza ku-detect madawa ya kulevya katika ports zetu hivyo kuzuia wimbi la kuifanya Zanzibar kuwa njia na soko la madawa ya kulevya. 
5. Zanzibar sasa inamatumaini ya kupiga hatua katika maendeleo yake. Maendeleo ya nchi yanategemea viwanda. Bila ya uwepo wa wataalam wa Industrial Biotechnology, Zanzibar haitopiga hatua inayotarajiwa katika viwanda.  Kuwa na wataalam hawa, kutapelekea kuanzishwa kwa viwanda vya wazalendo kuanzia pharmaceutical industries (viwanda vya madawa)  hadi food industries (vya chakula). Kwa sababu wawekezaji wanahitaji wataalam wazawa katika nchi husika ili kupunguza gharama za kuagiza wataalam kutoka nje, pia katika dunia ya sasa viwanda na vyuo vikuu hufanya kazi pamoja (University- Industry Collaboration). Viwanda vinategemea tafiti katika kupunguza gharama ya baadhi ya processes zake uzalishaji au katika kuzalisha products ilyobora zaidi. Vyuo vinahitaji uzoefu (practice) na funds kutoka kwenye viwanda.
6. Bioterrorism, ingawa sio tishio kwa Zanzibar na hata kwa nchi nyingi za afrika, lakini dunia sasa ni kama  kijiji.. soon or later na huku kwetu yatafika, ni vizuri tukawa na wataalam wa fani hizo, ili tuwe tayari kukabiliana, kuzuia na kuepusha majanga ya biological weapons. 
Kufikia hayo niliyoyataja hapo juu si ndoto,  inawezekana tukiamuwa kuekeza kwenye Biotechnology kuanzia sasa. Kumbuka nchi zote zilizoendelea ziliekeza kwenye Research and Development (R&D). 
Waalimu  (lecturers) tutapata wapi?
Ukosefu wa waalimu (lecturers) ni tatizo katika vyuo vingi hasa katika masomo ya sayansi. Tatizo hili lipo kwa fani mpya zinazoanzishwa vyuoni na hata kwa fani kongwe zilizokuepo enzi na enzi. Hivyo ni dhahiri wataalam wa Biotechnology  hasa kwa Zanzibar ni wachache mno! Na pengine kwa staff waliopo  hivi sasa pale SUZA hakuna hata mmoja mwenye basic ya Biotechnology, lakini  hilo si tatizo kama tukiamuwa kujipanga kuanzia sasa. Nimesoma kwamba kuna scholarship za Qabus kwa ajili ya wafanyakazi wa SUZA. Ushauri wangu, katika hizo nafasi 50 za wanaokwenda mara hii, japo nafasi 3 (mapaka 5) wapelekwe kufanya Master of Science in Biotechnology (M.Sc. Biotechnology).
Unaweza kufanya M.Sc in Biotechnology hata kama huna Bachelor in Biotechnology, ILA ni lazima uwe na BSc in either Microbiology and Chemistry, au Biology and Chemistry au molecularbiology and chemistry  au mfano wa hizo! Nna hakika SUZA wapo wengi wenye Biology na Chemistry, wapelekwe kufanya MSc in Biotechnology ambayo itakuwa ni by course work and dissertation, hii itawajenga kuja kuwa waalimu bora wanaojuwa Biotechnology kwa mapana yake na SIO by Thesis only (hii si nzuri kwa asie na basic ya Biotechnology).  Naamini baada ya miaka miwili (2 ) tutakuwaa na wataalam wakuanzia na wengine tukijaaliwa tutakuja (tutatoka tulikojificha).
Mwisho
Huu ni ndio mchango wangu wa kimawazo kwa sasa katika kuifanya SUZA iwe “catalyst for social changes” kwa kuanzisha fani zenye kuhitaji katika maendeleo ya Zanzibar na watu wake.
Ahsante.
A.M (PhD student in Biotechnology).
Chanzo: Mzalendo


No comments :

Post a Comment