Zanzibar and Kenya flags raised at UN Head Quarters in New York on 16th December 1963 when the two countries were admitted to the United Nations. Representing Zanzibar was the Prime Minister H.E. Sheikh Mohammed Shamte while Kenya was represented by its Deputy Prime Minister H.E. Mr. Jaramogi Oginga Odinga. UN Secretary General U Thant welcomed the guests.
Written by Stonetown (Kiongozi) // 26/12/2012
Ikiwa ni takribani mwaka mmoja tu, kwa Muungano wa Zanzibar na Tanganyika kutimiza nusu karne, kuna kila dalili kwamba Zanzibar, kama ilivyo Tanganyika imepoteza utaifa na utambulisho wake wote. Kilichobaki ni historia au magofu tu ya masaza ya visiwani hivi ambavyo vilikuwa Jamhuri kamili hapo awali.
Zanzibar ndani ya Muungano haina kikubwa ilichovuna zaidi ya kupoteza utaifa na kila kitu chake. Hata hivyo ieleweke kwamba, kumalizika huku na kufiliska kwa Zanzibar kumechangiwa kwa kiasi kikubwa na viongozi wakuu wa visiwa hivi. Katika sura hii, tuangalie hasa chanzo na mchango wa Wazanzibari wenyewe katika kuimaliza nchi yao wenyewe.
Chanzo cha haya kimeanza na Sheikh Karume na hata Aboud Jumbe kwa kiasi Fulani. Lakini shida na mashaka makubwa ya Muungano kwa Zanzibar yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na viongozi waliofata baadae. Hasa hasa, tangu chama tawala kianzishe mkakati maalum wa kuichagulia Zanzibar Rais, bila kujali ridhaa ya wananchi wa Zanzibar
Bila shaka tunatambuwa wazi kwamba Viongozi wanaoletwa kuitawala Zanzibar hawawi au hawapati ridhaa za wananchi hata kama iatonekana wanaungwa mkono na vyama vyao. Ukweli huwa sio huo. Viongozi kama hawa wakishakuletwa tu hapa, hufuata ridhaa za wakubwa zao na kufanya waliyoagizwa tu, bila kuhoji na kujadili athari zitazofata baadae. Viongozi kama hawa kwa jina moja tunawaita ‘Mamluki’ (puppets).
Zanzibar inamalizwa na viongozi mamluki wa Muungano. Viongozi ambao kwa kutojali maslahi ya nchi yao, utu wao, na utambulisho wao, huweka maslahi binafsi kwanza na kuiingiza nchi hii katika mashaka makubwa ambayo yanaigharimu Zanzibar roho, damu, na nguvu ya watu kuikomboa tena. Baya zaidi ni kuwa maamuzi hayo wakishakuyafanya tu ili kuwardhisha mabwana zao, mabwana hao huwageuka viongozi hao na kuwafanya mahasimu wao wakubwa bila kujali wema waliofanyiwa. Rejeea kwa Karume na Salmin na si muda mrefu Sheni. Labda tuanze na mifano hai .
Dokta Salmin Amour Juma (Komandoo), aliingia madarakani mwaka 1990 hadi 2000. Kabla hajawa Rais wa Zanzibar alikuwa mtoto kipenzi wa Dodoma na katika chama. Akapewa Urais, huku kwa upande mwengine akipewa masharti ya kuipiga mnada bure Zanzibar chini ya Muungano.
Ikumbukwe kwamba Dr. Salmin Amour atakumbukwa kama ‘Baba wa siasa za fitna, za kimaskani, na upemba na Uunguja’ katika vitabu vya historia vya nchi hii na dunia kwa ujumla. Hiki ndicho kikubwa tunachomkubuka Dr. Salmin katika umuri wa Utawala wake. Nje na hayo, Dr. Salmi atakumbukwa kwa mambo matano aliyoyafanya kuizamisha Zanzibar ndani ya kinywa kipana cha Muungano.
Ni Dr. Salmin aliyeoandowa uingiaji wa watu Zanzibar kwa kutumia passpoti. Kosa hili lilichukuliwa kuwa dogo sana wakati alipolifanya lakini mashaka yake yamekuwa ni ya udhia mkubwa kwa visiwa hivi hasa Unguja. Visiwa hivi vidogo vilivyokuwa na watu wasiozidi laki 6 hadi miaka ya 1988, imekurupuka na kuwa ni nchi yenye idadi ya watu inayoongezeko na msongamano wa watu kwa kasi ya asilimia 3 kwa mwaka (sensa, 2002), idadi ambayo ni kubwa hata kuliko Mkoa wa Dar es Salaam.
Zanzibar imejaa watu, wenye haki ya kuishi na wasio na haki. Watu wema na wabaya. Kila mtu anakuja tu na anaachiwa aingie afanye analotaka. Athari ya kuondoa uingiaji kwa passpoti, pia umechangia sana kuonegezeka kwa vitendo vya uhalifu, ukahaba, uingizaji wa madawa ya kulevya, kufa kwa tamaduni za asili na hata wizi wa watoto wachanga kwa mara ya mwazo katika historia ya nchi hii.
Dr. Salmin atakumbukwa kwa kufunguwa milango ya uingiaji wa makanisa hapa visiwani sambamba na kutoa viwanja kwa Wakristo bila hisabu wala kujali athari yake baadae. Tunaamini haki ya kuabudu na tunakiri kuwa Zanzibar kuna wakristo lakini wasiozidi aslimia moja ya watu wote. Sasa idadi hio ndogo inakujaje kuwa ifuatiwe na mkururo wa makanisa ambayo waumini wake ni lazima waletwe kwa boti kila Jumamosi kutoka bara kuja kuabudu Zanzibar ili angalau kila kanisa lipate safu mbili za waumini?
Ni Dr. Salmin alienyamaza kimya wakati nafasi ya Rais wa Zanzibar kuwa makamo wa Ris ikiondolewa na kumuweka Rais kuwa ni Waziri tu katika Jamhuri ya Muungano. Ijapokuwa yeye hakukubali hata siku moja kuingia bungeni kama Waziri, lakini ilikuwa tisha toto tu. Hakuweza kulipinga suali hilo na kusema iwapo ni hivi sisi hili hatulitaki. Kwa maana hii tunasema aliridhia kabisa, na hana budi kubeba lawama.
Dr. Salmin pia ndie alieikaribisha TRA na kuunganisha mapato ya nchi hii kwenda bara. Na kwa kufanya hivi alikuwa hajui kuwa ndio anaimaliza kukatwa mishipa ya mwisho ya kuvutia pumzi kwa Zanzibar baada ya kuiuwa biashara ya bandari huru. Leo hii bara inajengwa majumba makubwa, barabara viwanja vya ndege vikubwa kwa mapato ya Zanzibar. Huku Zanzibar miundo mbinu na maendeleo kwa ujumla ikisuasua na kudumaa.
Leo Mzanzibar analipa kodi mara mbili bara na Zanzibar lakini wa bara analipa kodi mara moja tu. Haya ndio malipo ya hisani yetu kwao. Na walipokwisha kupata maslahi yao Dr. Salmin kasahauliwa kama kwamba hajawafanyia hisani yoyote ile. Licha ya kufanya yote haya na mengine nimeyasahau kwa sasa. Malipo yake fedheha, ndio aliypopata.
Pia, hivi makaribuni kulivumishwa taarifa kuwa eneo la bahari kuu litakuwa mali ya Muungano. Pia suali la mafuta nalo likaja tena juu hata baada ya kukingiwa kifua wakati wa jemedari Dr. Karume. Umuhimu wa mambo haya mawili unaeleweka sana kwa maslahi ya Zanzibar yetu. Lakini tukumbuke kuwa kuna Dr. Shein ambae kwa sura yake aliyo sasa amewekwa kuyakabidhi haya tuwe tumemaliza kila kitu chetu. Nina uhakika chini ya Uongozi wa Dr. Sheni haya yote atayapeleka Muungano, kama hajayapeleka hivi sasa.
Kinachomskuma Dr. Shein kukubali haya yote ni yale yale, ya kulipa fadhila na ihsani ya ‘mkono ukulishao’. Yeye amepewa Urais, ambao ni utukufu wa dunia kwa miaka kumi. Kwa jinsi binadamu alivyo jahili wa nafsi yake, miaka kumi ya Urais mtu huiona mingi na kwa hivyo yuko tayari kutoa chochote ili abakie kuwa Rais tu. Mwisho wake atakuja kukaa na sisi atuambie porojo hili na hile, nchi keshaiuza wakati ambao alikuwa na uwezo wa kuitetea.
Kwa hali hii tuendayo nayo na Viongozi mamluki wa Zanzibar wanavyotumiliwa kuihujumu nchi yao kwa maslahi yao binafsi, itafika pahala Zanzibar isiwe na lolote. Hakutakuwa na Rais wala baraza la wawakilishi. Na haya yako njiani. Naamini akiondoka Sheni yote haya yatakuwa yamekwisha. Labda tutabakiwa na mapendekezo ya CUF, ya kuwepo kwa Gavana wa Zanzibar katika Muungano. Basi! Na hapo tutakuwa tumeshajizika na kujisomea hitma yetu.
Natoa hoja.
Chanzo: Mzalendo
Natoa hoja.
Chanzo: Mzalendo
No comments :
Post a Comment