Kitambo kulikuwa na taarifa za kuendeleza eneo la bandari ya malindi hasa lile eneo la boti ndogo ziendazo kwa kasi. Kutokana na Serikali kutokuwa na uwezo hali iliyopelekea kushindwa kuliendeleza iliamua kumkabidhi mfanya biashara mzalendo, Bw Said Bakhresa.
Kutokana na uwezo na uzowefu wake pia mchango wake mkubwa aliofanya katika ukombozi wa usafiri baharini, Bw Bakhresa ameweza kuliendeleza eneo la bandari kule Daressalam kwa kuweka system nzuri na za kisasa. Hivyo kuonyesha moyo wa kutaka kuliendeleza eneo la bandari ya Zanzibar, vilevile.
Hapo mwanzo alikabidhiwa eneo la kuegesha meli, baadae akaruhusiwa kufanya ujenzi wa eneo la kupumzikia wageni, hapohapo bandarini.
Hivi Sasa Bw Bakhresa amekabidhiwa eneo lote la bandari kuanzia kwenye Chuo cha Sayance Baharini hadi kwenye round about ya kuingilia Bandari kuu. Juzi tu alikuwa na ziara ya kupitia na kutembelea eneo hilo na kujionea ujenzi unavyoendelea.
Sio wazo baya hasa Bw Bakhresa akiwa mzawa mwenye uchungu na nchi yake, swali langu ni kuwa jee utaratibu wa kukabidhiwa eneo hili umefuatwa?
Hivi kwanini kila kitu kifanyika kimya kimya hali ya kuwa tunaimarisha utawala bora chini ya misingi ya accountability and transparency?
Jee tungelitangazia eneo hili hivi asingetokezea mwekezaji mwengine hata asiwe mzawa lakini uwekezaji wake ukawa na faida kubwa na nzuri zaidi kuliko huu wa mzawa?
Naomba majibu yenu
No comments :
Post a Comment