Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, January 6, 2013

ZANZIBAR: Kusimama Ujenzi wa Uwanja wa ndege Zanzibar- yaliyo nyuma ya pazia

 Abeid Karume International Airport 
ZANZIBAR
(Construction work of the new airport stopped)





Written by  


Structure ya jengo la uwanja mpya wa ndege Zanzibar
Structure ya jengo la uwanja mpya wa ndege Zanzibar
 Wazalendo
Ndio tumeuanza mwaka mpya. Kuna mengi tuliyoahidi mwaka uliopita kuwa yatakamilika mwaka huu. Mutakumbuka miongoni mwayo ni pamoja na:
* uwekaji wa waya mpya za umeme kutoka Bara hadi Zanzibar
* Kukamilika kwa mradi mkubwa wa e-government
* Kukamilika kwa mradi mkubwa wa ujenzi wa uwanja wa ndege mpya na wakisasa, nk
Leo naomba nigusie hili la ujenzi wa uwanja wa ndege mpya na wakisasa.
Kama tunavyofahamu ujenzi wa uwanja huu umekuwa kwenye mashaka makubwa tokea kuanzishwa kwake ambapo 70 billion USD zimetumika katika ujenzi wake. Halkadhalika kuna maongezeko mengine ambayo mwanzo hayakuwemo kwenye mkataba wa awali.
Vilevile, kama tunavyoshuhudia kusimama na kuendelea polepole kwa ujenzi wenye fungu kubwa la fedha za walipa kodi ambao ni mkopo nafuu kutoka serikali ya Watu wa China. Hii ni sawa na kusema kila Mzanzibar atakuwa anadaiwa fedha zilizotumika kwenye mradi huu.
Kuna jengine jipya limejitokeza. Nalo ni jengo la abiria wa uwanja wa ndege mpya na wakisasa limejengwa sehemu siyo. Sehemu liliopo jengo hili kwa mujibu wa ramani na vipimo ni sehemu ya kupark ndege. Jengo lilitakiwa lirudi nyuma zaidi kwenye eneo la nyumba za raia upande wa magharibi ili kupisha nafasi ujenzi wa park za ndege.
Hili ni pigo kubwa kwa mradi huu uliogharibu zaidi ya 70 milioni USD, huku ukichelewa kukamilika kwa wakati wake. Swali zito ni vipi mafundi wa ujenzi huu wataweza kufanya masahihisho ambapo foundation yake ilikuwa kina kikubwa, structure imefungwa na bolts and nuts, huku baadhi ya vipande vyengine kuunganishwa kwa welding.
Ingawa kutakuwa na maswali mengi kuliko majibu, msomaji na wewe unaweza kujiuliza maswali zaidi ya kama haya nitakayojiuliza:
i) Mjenzi wa uwanja pamoja na uzowefu wake hivi hakutanabahi kwamba anatumia vipo sivyo?
ii) Consultant wa ujenzi huu muda wote huo alikuwa haoni au kujuwa vipimo vilivyotumika sivyo?
iii) Wataalam wa serikali yetu jee pia hawakutanabah kwamba hili jengo liko nje ya eneo la makubaliano?
iv) nani atalipa gharama za fidia kwa hasara zote zitakazotokea, au kama kawaida yake mzigo abebeshwe Mnyamwezi, SMZ?
v) Jee Serikali yetu itaendelea kuwa mahusiano mazuri na China, huku tukiendelea kuchukuwa mikopo ya bei nafuu kwa masharti ya kupangiwa wajenzi (contractors) wa Kichina?
Kuna haja ya Wazanzibar kuzinduka kutokana na usingizi wa “Aswhabul Khaf” kuendelea kwetu tutaikuta nchi siyo yetu tena. Haya yote yasingetokezea laiti tungekuwa makini katika utendaji kazi wetu.
Source: Mzalendo.

3 comments :

  1. Ama kiwango cha billion 70 US$ kilinizungusha akili kwa kiwango kikubwa lakini baadae nikaona ni millioni 70.Juu ya hayo,kwa fedha hii,kama ingekuwa nia ni safi,basi tungekuwa mbali kuliko hapo tulipo.Inawezekana njama za ulafi zimetumika.Kwa mtazamo wa kifundi,mzigo wa lawama uwelekee kwa CONSULTANT.

    ReplyDelete
  2. Great article with excellent idea!Thank you for such a valuable article. I really appreciate for this great information.. Zanzibar taxi prices

    ReplyDelete
  3. Positive site, where did u come up with the information on this posting?I have read a few of the articles on your website now, and I really like your style. Thanks a million and please keep up the effective work. Zanzibar budget taxi

    ReplyDelete