Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, January 7, 2013

ZANZIBAR: Muungano wa mkataba


Kwa nini mfumo huu?

Written by   //  07/01/2013
Moja kati ya malalamiko makubwa hasa kwa upande wa visiwani juu ya mfumo wa muungano wa sasa ni wa kujibebesha mamlaka yanayokwenda kinyume na makubaliano makuu ya 1964. Wakati ule article of union ilikuwa na mambo 11 kama ya muungano sasa hakuna idadi kwani kuna general charter katika katiba inayoipa mamlaka katiba ya muungano kuengeza masuala ya muungano bila ya hata idhini ya wahusika. Mifano iko mingi tu, wala hakukuwa na consultation ya wananchi juu ya mabadiliko hayo. Katiba muungano wa mkataba, nchi husika zitayaingiza masuala yaliyokubaliwa ndani ya mkataba na kuyaingiza katika katiba zao ili kuweka mipaka ya mamlaka zipi za muungano na zipi za nchi husika. Miungano mengi ilio solid na strong ni ya mifumo ya namna hii ambayo imeweka kipaumbele zaidi katika maendeleo ya wananchi rather than muundo wa kimamamlaka wa nchi moja.
Jee kuundwa kwa mfumo huu ni kuvunja muungano?
Si kweli, tukitaka kuangalia kwa undani zaidi hasa katika mfumo huu wa sasa utakuta tayari muungano wa sasa una utata hasa kutokana na mabadiliko makubwa ya katiba ya Zanzibar ya 2010 yaliorejesha mamlaka makuu ya nchi kwa rais wa Zanzibar hadi kufikia kuleta mjadala wa ni ipi nafasi ya rais wa muungano. Kwa sasa kutokana na mabadiliko ya 2010 yalioridhiwa na 65% ya wazanzibari yamemfanya rais wa muungano kuwa na mamlaka ya ceremonial zaidi na mamlaka makuu visiwani kurejea kwa rais wa Zanzibar, mfano mabadiliko ya mikoa badala ya kufanywa na rais wa muungano sasa yabafanywa na rais wa Zanzibar bila ya hata ushauri wa rais wa muungano. Au kumpa uamiri jeshi wa vikosi vya SMZ, au hata katiba ya Zanzibar kutamka bayana kuwa Zanzibar ni nchi kinyume na tafsiri ya ubabaishi ya status ya Zanzibar katika katiba ya Jamhuri. Sasa tujiulize jee hayo yote yameweza kuvunja muungano kwa kuwa na katiba mbili za zinazokingana? Hakuna logic yeyote ya wanaosema kwamba ili tuwe na mfumo wa mkataba basi ni lazima tuuvunje wa sasa, kwani tulipokuwa na article of union ya mambo 11 tulivunja kwanza muungano tukaweka katiba ya 77 ya pamoja na kumong’nyoa mamlaka ya nchi husika bila ya idhini wa wananchi wenyewe? Au huu wa sasa na mabadiliko ya Zanzibar yaliona legitimacy ya wananchi 65% yalikuja baada ya kuvunja muungano? Au pale rais wa Zanzibar alipoondolewa madaraka yake ya umakamo wa rais wa muungano kinyume na makubaliano ya 1964 yalihitaji kuvunja muungano kwanza. Wanaodiriki kusema kwamba wanaotaka mfumo wa mkataba wana agenda ya kuvunja muungano hawana hoja zenye mashiko ila ni kuwatia khofu wananchi wasiwe na uwezo wa kuujadili muungano kwa kina na kutafutia suluhisho la kudumu. Huu wa sasa ukiwa unalindwa na katiba ya jamhuri tayari una mashakil makubwa kutokana na mabadiliko ya katiba ya Zanzibar na bado muungano tunao, kinachohitajika kufanywa ni kuondosha mode ya mfumo wa sasa kwenda katika mfumo wa mkataba kwa kutumia phase maalum.


Jee tunaweza kubakiwa na mfumo wa sasa huku tukiwa na marais wawili wenye mamlaka sawa?
Uwezekano wa mfumo huo ni sawa na ngamia kupita kwenye tundu ya sindano. Huwezi kuwa na nchi moja yenye wakuu wawili walio sawa, ima tubadili mfumo wa serikali moja au kuwa na mfumo wa mkataba. Tunaweza kuwa na mfumo wa sasa na mmoja wa marais wa nchi kuwa na nafasi ya umakamo katika serikali ya muungano lakini pia kuna masuala kama ni namna gani nchi zitaendeshwa pindipo rais wa nchi moja akitokea katika upande wa upinzani. Au utajustify vipi makamo huyo wa jamhuri kuendesha nchi akiwa na kura za wachache kutoka Zanzibar pekee maana katika muundo huo automatic rais wa Zanzibar atakuwa ni makamo wa jamhuri ya muungano lakini akiwa kachanguliwa na wapiga kura less than 300000 katika total ya 500,000 waliojiandikisha amabao ni wazanzibari huku tukiwaacha milioni 43 wananchi kutoka Tanzania bara. Ni mgongano wa legitimacy ya democracy na ndio maana ima tuwe na muungano wa mkataba au tuwe ni nchi moja ya serikali moja.
Mkataba au Katiba?
Tumeona katika mfumo wa katiba wa sasa kumetokea mabadiliko makubwa yaliouweka muungano katika njia panda. In theory kwa sasa ima katiba ya Zanzibar na mabadiliko yake ya 2010 hayako halali au katiba ya muungano haipo sawa. Point ya kuangalia kwa undani hasa kwa wanaotaka mfumo wa sasa kubakia ni kwamba hicho wananchokilinda tayari washakivunja in principle, tutoe kwa mfano mheshimiwa Nahodha akiwa ni champion wa muungano, ni yeye akiwa mkuu wa mawaziri alieridhia na kufanikisha mabadiliko ya katiba ya Zanzibar ya 2010 yaliotamka kwamba Zanzibar ni nchi na pia kuondosha mamlaka ya rais wa muungano kinyume na katiba ya muungano. Kama alikuwa haridhii mabadiliko yale ni ipi moral au legitimate justification ya kubakia katika serikali iliokwenda kinyume na imani yake? Au anaponyanyuka na kusema rais wa Zanzibar na muungano kuwa na mamlaka sawa kaona wapi duniani nchi moja kuwa na rais wawili? Mfumo wa mkataba utaweza kubainisha kwa uwazi madaraka ya mamlaka husika kwa kupitia zile respective katiba zao zilizopata mandate ya wananchi na kulindwa kisheria zaidi kuliko kuwa na katiba mbili zilizo pararell. Moja kati ya faida za mkataba ni kuwa na uhakika wa mandate gani zinabaki katika mamlaka ya union na pia kuhakikisha hazitochezewa na wanasiasa kwa sababu mabadiliko yoyote yatahitaji referendum ya wananchi.
Kwa nini tusijiunge na EAC hasa ikiwa mfumo tuutakao ni wa Mkataba?
Kwanza future ya EAC kwa maoni yangu ni ya mashakil zaidi, lakini nitajibu suala kwa interest ya Zanzibar zaidi. Kwa sasa Tanzania ina watu milioni 43 bara na milioni moja Zanzibar na tumeona influx ya uhamiaji na matatizo yalioko baina ya indigenous na wengine. Katika kisiwa kidogo kuukaribisha mfumo utaoruhusu kuwa na free movement ya wananchi katika EAC yenye watu milioni 120 katika kisiwa kidogo kama Zanzibar ni disaster, au kuwamo katika union yenye malengo ya sarafu moja pia ni tatizo hasa kwa Zanzibar. Tukiwa na limited land ya kulima na export, biashara ni moja kati ya nyenzo muhimu za mapato ya serikali, tunapojiunga katika mfumo wa sarafu moja na fiscal policies za uchumi mmoja basi itawia vigumu kwa wananchi visiwani kuyakimu maisha yao hasa kutokana na nchi zinazoungana katika EAC kuwa ni moja kati ya nchi zinazoexport zaidi kuliko import kama chanzo cha mapato ya nchi. Ikiwa Uganda, Burundi, Rwanda, Kenya na Tanzania bara watapush zaidi katika devaluation ya sarafu ili kuwasaidia wakulima wa kahawa nk itakuwa na effect kubwa visiwani kwani devaluation ile ya sarafu itafanya ununuzi wa bidhaa nje ya nchi na kuexport nyumbani kuwa ghali zaidi hasa kwa vile thamani ya sarafu itakuwa ndogo kuliko ya ununuzi wa bidhaa, kama unga utacost dola moja kwa kilo, ikiwa devaluation italengwa zaidi kwa wananchi milioni 119 kutoka mainland EAC ili kuwasaidia wakulima, kwa upande wa Zanzibar devaluation ile itawacost wafanyabiashara kwani dola moja ya unga itakuwa ghali zaidi kutokana na sarafu kuanguka.
Pia sioni kama its in the best interest kwa visiwani kuungana na nchi zisizoKUWA stable, kama vile Uganda, Rwanda na Burundi, machafuko madogo tu yanaweza kurejesha nyuma maendeleo ya uchumi na kuziingiza nchi katika mashaka ya kujitakia, mfano mdogo tu hivi sasa sakata la ziwa Tanganyika aka nyasa, hivi ni nani angeliamini kwamba nchi mbili ziliopakana katika ziwa moja huku moja ya nchi hizo zikidai umiliki wa ziwa lote ati kwa sababu ya ramani iliochorwa mwaka 1800. Hivi tuseme integration kubwa ya EAC miaka 10 ijayo hatutakuja kusikia Burundi au Rwanda ikidai part ya Kigoma ni yake kwa sababu ya historical na geographical reasons hasa ukizingatia nchi zote hizi katika EAC hazina ukubwa wa ardhi kama Tanzania Bara, kama unahisi ni ndoto tazama namna gani majirani hawa wanaoiangamiza Congo DRC then utaamini katika miungano ya nchi za kiafrika hakuna uaminifu.
Ni kipi kiwemo katika mkataba?
Mfumo wa sasa umejenga zaidi mahusiano ya kiutawala zaidi na ndio frictions zinatokea, mfumo wa mkataba ujijenge zaidi katika masuala ya maendeleo ya wananchi, kwa mfano masuala ya kilimo, mifugo, afya, uondoshaji wa umaskini etc. badala yakung’ang’ania mfumo wa sasa usio na logic tuje na mfumo utakaoufaidisha masikini zaidi na kujenga haki na usawa wa kweli. Katika kitu kikubwa nilichokiona katika mfumo wa EU ni mahakama za EU zikiwa na nguvu zaidi kulinda haki ya raia wa EU. Mfano ni majuzi tu serikali ya uingereza ilishitakiwa katika mahakama ya EU kwa kuwanyima wafungwa haki ya kupiga kura, japokuwa vyombo vikuu vyote vya nchi vilisema hakutakuwa na mabadiliko, mahakama ya EU imeilazimisha serikali kubadili statement yake kutokana na ile rulling yao inayoweka wazi unyimaji huo ni kimyume na haki za binaadamu. Muungano wa mkataba uweke wazi umuhimu wa mahakama zao na kutarget zaidi katika mausala ya kujenga demokraisia zaidi na ulindwaji wa haki za binaadamu.
Jee bunge na serikali ya muungano katika mfumo wa mkataba utakuwa na nafasi gani?
Bunge la muungano litajumuisha masuala ya muungano pekee, ikiwa muungano utajengeka zaidi katika masuala ya maendeleo ya wananchi hakutakuwa na mashaka ya kimamlaka kama sasa au kiutawala kwani katika masuala ya uongozi wa nchi husika mamlaka yatabakia kwa nchi husika bila ya mmoja kumuingilia masuala ya mwenzake. Wabunge wa muungano waendane sio tu na wingi wa population bali zaidi wingi wa masuala yenywe ya muungano. Serikali ya muungano itaundwa na mamlaka ya serikali husika huku rais na makamo wake wakiwa zaidi katika ceremonial position kwa sababu bunge na baraza la mawaziri likiwa na mamlaka ya mwisho kwa majukumu ya muungano. Nchi nyingi zinamfumo wa rais alie zaid katika ceremonial position mfano Israel na ujerumani.
Nani atakaeunda serikali ya Muungano?
Serikali itaundwa kwa majadiliano baina ya wakuu wa nchi mbili baada ya uchaguzi wa uongozi wa their respective countries. Mawaziri wakuu ndio watakaoongoza serikali ya muungano na mabaraza yao huku marais wakiwa na ceremonial position zaidi. Bunge pia litaendeshwa kwa uchaguzi na wakuu wa serikali bungeni ni waziri mkuu wa upande mmoja akiwa na deputy wa upande wa pili wakijibu hoja za wabunge husika.
Hoja za wanaoupinga mkataba
Katika statement za viongozi wakuu wanaopinga mkataba hoja zilizojitokeza so far ni mbili. Kwanza ni “huwezi kuwa na mkataba kama hujavunja muungano”, kama nilivyoeleza mwanzo hii ni hoja dhaifu, kwani tukiangalia mabadiliko ya katiba ya 2010 walioyaridhia na kuwaweka madarakani leo yamekwenda kinyume na katiba ya muungano na mbona muungano wenyewe haujavunjika? Hawa ndio wakuu wa tume za kurekebisha kero za muungano wakati huo huo utawasikia majukwaani wakiwaambia wananchi hakuna haja ya mabadiliko kwani tayari tuna katiba yetu, bendera nk. Kauli hizi ndio zinazotupa ufafanuzi wa kwa nini kero za muungano hazijarekebishwa kwa miaka 48 hasa kwa sababu waliopewa majukumu hayo hawaoni haja ya mabadiliko kwa kuamini status yetu tulionayo ishajitosheleza.
Hoja ya pili ni kuwa mfumo wa mkataba ni wa wapinzani na kila cha mpinzani kipingwe hata kikiwa na maslahi ya nchi. Hakuna ukweli kama muundo wa union wa mkataba umeanzishwa na CUF na ukiangalia zaidi waliokuja na mfumo huu ni progressive team kutoka vyama tafauti waliochoshwa na kero zisizo na mwisho. Kukubaliwa kwa hoja ya mkataba na viongozi wakuu wa vyama vya upinzani kunaonyesha ukuwaji wa kisiasa na kidemokrasia katika siasa visiwani.
Kwa upande wa Tanzania Bara hoja zao za kuupinga zimelengwa zaidi katika ile doctorine ya Mwalim Nyerere ya kuwa na serikali kuu moja na kuigeuza Zanzibar kuwa miongoni mwa mikoa ya Tanzania. Pan Africanism movement ndio inaowajenga wenye hoja hizi wakiwemo baadhi ya wazanzibari wanaoamini ni waste of time kuwa na kinchi kidogo kinachojiendesha kimamlaka huku kikidai zaidi nguvu za kujiongoza. Wamesahau kwa muda wa takriban miaka 20 ya Mwalimu madarakani kama rais wa Tanzania hakuwahi kwa uwazi kuwaeleza wazanzibari lengo lake hilo kwa sababu ya opposition iliopo. Na kwa muda wa takriban miaka 48 ya muungano, muundo wa serikali moja umekuwa ndio chachu ya kuvunjwa kwa muungano kila unapotamkwa na kunyoshewa vidole kama ndio direction ya future ya nchi. Infact kilichowapa nguvu wazanzibari kwenda mbali zaidi katika mabadiliko ya katiba ya 2010 ni kauli za wakuu wa nchi hususan bungeni kusema kwa uwazi kwamba Zanzibar si nchi. Wanaoamini mfumo wa serikali moja hawana mashiko makuu na ni sawa na wanaoota ndoto mchana, kwani bila ya referendum ya kuwauliza wazanzibari hatima yao katika mfumo wa serikali moja hakuna katika dunia ya leo atakeweza kuwashurutisha kuingia katika mfumo wa namna hii.
Pia kuna hoja za kwa nini kijinchi cha watu milioni moja kiwe na haki sawa katika kuamua hatima ya jamhuri? Huku nakuita ndio kufilisika kwa mawazo kwani kwao wao wingi wa watu na ukubwa wa nchi ndio kigezo pekee cha kuinyima Zanzibar haki ya kuamua masuala yya muungano. Logic iko wapi kuwa muungano na hatima ya muundo wa muungano uamuliwe na gurupu moja tu la watu kwa kigezo cha population na ukubwa wa nchi huku wakisahau tulipoungana regardless ya population sote tulikuwa ni nchi zinazotambuliwa na UN. Katika article za union au hata ndani ya katiba ya muungano huu wa sasa Zanzibar inatambulika kama ni mdau mkuu wa hio union sasa iweje leo tuambiwe hatuna haki sawa ya kufanya marekebisho ya nchi tulioungana?
Udhaifu mkuu wa wenye maoni ya namna hii ni kusahau katika serikali ya Tanzania, yalio ya muungano ni nusu tu na yaliobakia hayamo katika mandate ya muungano na Zanzibar haiwezi kuchangia maoni kwa yale yasio ndani ya mandate ya muungano. Wanaponyanyuka na kusema hatima ya nchi kupewa haki sawa kwa watu milioni moja wanapotosha umma kwani katiba ya Zanzibar na ya muungano imebainisha wazi ni yepi ya muungano. Hatuwezi kuulizia gesi ya mtwara, au dhahabu, au kahawa kwa vile hazimo katika mandate ya union ila tunachoweza kukijadili kwa usawa ni kwa yale yaliomo ndani ya muungano ambapo ndio wadau wakuu. Nchi hizi hazijawahi kuwa moja, huo ndio ukweli mchungu na hata kwa sasa nafasi ya rais wa muungano ipo zaidi katika ceremonial position kwani madaraka mengi ya rais wa muungano yamevuliwa na mmabadiliko ya katiba ya 2010 na kurejeshwa kwa rais wa Zanzibar kama Mheshimiwa tundu Lisu alivyoyachambuwa mabadiliko ya katiba ya 2010 bungeni.
Hitimisho
Mpaka sasa hakuna aliekuja na hoja yakinifu za kuupinga mkataba, na wanaoupinga wengi wamejengeshwa khofu ya makusudi juu ya kitu wasichokijua. Tafauti gani ya mkataba na ile article ya mwanzo ya union ya 1964 hata iwe vigumu kurejea katika uasili wa muungano based on muundo unaotoa haki kwa nchi husika kuwa na clear mandate ya mambo ya muungano?
Iweje tuwaite wenye kuutaka mfumo wa mkataba kuwa wavunja muungano wakati huo huo tuliridhia kwa asilimia 65 na kufanya kampeni ya kurekebisha katiba ya visiwani iliokinyume kabisa na ya muungano ikaenda mbali zaidi hata tukawa katika black hole ya legitimacy ya union nzima?
Jee kuridhiwa kwa mfumo wa mkataba na wapinzani ndio hoja pekee ya kupinga ideology mpya japo ikiwa imebeba maslahi bora ya visiwa hivi na kwa future mpya ya haki baina ya pande mbili zilioungana knidungu zaidi kwa miaka 48?
Badala ya kuupinga bila ya kuujadili na kuangalia wapi pako sahihi na wapi parekebishwe tena, tunajinyima na kuwanyima wananchi uwezo wa kufikiri na kujiamulia hatima ya muungano wao huku tukijibebesha jukumu tusilokuwa nalo. Hebu na tuupitiie na kuufanyia utafiti strength, weakness, threats na opportunism zake na kuangalia katika mode nyingi za analysis ili mabadiliko yajayo yawe fit for purpose na kuridhiwa na wadau wenyewe wa muungano.
Chanzo: Mzalendo

No comments :

Post a Comment