Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, February 11, 2013

ZACADIA - MKUTANO WA DHARURA - SATURDAY 16, 2013!

Zacadia
Dear All,
Kutokana na dharba ya snow tuliyoipata Ijumaa kuamkia Jumaamosi, mkutano wetu sasa utakuwepo Jumaamosi ijayo tarehe 16 February, 2013, kuanzia saa 6 mchana. Hii ni kwasababu zipo habari nzuri kutoka Zanzibar Diaspora / Ikulu, The People's Bank of Zanzibar Ltd na zaidi ni kutokana na ujumbe mzito unaokuja kututembelea hivi karibuni. Kwahivyo, tunataka kila mtu asikie mwenyewe na sio kuhadithiwa. 

Pahala ni chuoni: Zanzibar Madrassa at Eddystone Avenue.
Wakati ni : Kuanzia saa 6 mchana.
Tufikeni kwa wakati.
Ajenda ni:
[1] Tulipofikia na maendeleo ya shughuli zetu za ZACADIA
[2] Kutambulishwa kwa ma-Directors wa Zacadia
[3] Maelezo kuhusu ziara ya karibuni ya Rais wa Zacadia huko Zanzibar na  
     Pemba
[4] Ziara ya ujumbe mzito wa SMZ utakaokuja hapa Canada. Ujumbe ambao   
     pia utazijumuisha institutions zifuatazo:
          (b) The Zanzibar Social Security Fund
          (c) The Zanzibar Insurance Corporation
          (d) Diaspora Department - Ikulu
          (e) The Tourist Commission of Zanzibar
          (f)  Office of the Attorney General, and
          (g) The Zanzibar Investment Promotion Authority.
[5] Projects za ZSSF kwaajili ya Wana-Diaspora.
[6] Masuala na majibu plus Any Other Business.

Kwa wale waliohudhuria mikutano yetu ya nyuma watakumbuka kuwa tulikuwa tukiwasiliana na Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ Ltd) ili kupata kampuni ya online ya kupeleka pesa nyumbani yenye bei nafuu kuliko Western Union au MoneyGram. Tulisisitiza kuwa hio kampuni iwe inakuwezesha mwana-Diaspora kupeleka pesa Zanzibar online kutoka nyumbani kwako, bila ya kuenda benki au exchange house, kwasababu huku majuu muda hatuna wa kuenda huku na kule.

Kwa bahati nzuri hio kampuni imepatikana na tayari inafanyakazi na PBZ Ltd tokea tarehe 31 January, 2013. Tumechelewa kukujulisheni Wazanzibari wa Toronto kwasababu tulikuwa tukiijaribu kwanza hio kampuni ili tupate uhakika wa services na procedures zake kabla hatujaipendekeza kwenu. 
Shk Omar keshaitumia zaidi ya mara 3 na mimi zaidi ya mara 5, na jamaa 2-3 wa hapa Toronto pia washaitumia.

Inafanyakazi kama ifuatavyo:

[1] Unakuenda kwenye website hii hapawww.worldremit.com 
     na hapo unajiandikisha kwanza.

[2] Ukitaka kupeleka pesa ZNZ zipo 3 easy steps ambazo hata 
     mtu mwengine hanahaja ya kukuelekeza - it's so simple and straight         
     forward!

Zaidi ni kuwa, upo uhuru wa kuweza ku-fix amount unayotaka kupeleka either in Canadian Dollars or in TShs na baadae system itakupa gharama zako zote       in Canadian Dollars - yaani unaweza kujaza, say, 100 Dollars unataka kupeleka, au unataka mtu wako apokee TSHS 50,000/-. Siku ya mkutano                   tutaelezea zaidi kama mtu atakuwa na matatizo. Pia, unaweza kupeleka kiasi chochote kile. Minimum ni $15 na minimum fee nadhani ni $1.99 kama hivi.
Kwahivyo, sio lazima uwe na pesa nyingi ndio utake kupeleka.

[3] Ukesha ku-click submit button, baada ya dakika 1 utaletewa email msg isemayo kuwa your transaction was being processed. Kama umejaza sawasawa, basi baada ya dakika moja nyengine utapata email msg yapili inayokueleza kuwa your transaction was successful na anangojewa mtu wako Zanzibar akapokee pesa kutoka PBZ Ltd - branch ya Malindi kwa Zanzibar, Chake Chake kwa Pemba na Kariakoo kwa DSM.

[4] Yule unaempelekea pesa kule ZNZ yeye atapata SMS msg kwenye simu yake na email msg pia akielezwa kuwa umempelekea pesa na anatakiwa aende PBZ kuzichukua. Kwa upande wao PBZ hawatakiwi wafanye lolote isipokuwa kulipa tu, kwani kila kitu kinakuenda automatic. Lakini, juu ya hivyo naona PBZ wanasaidia sana, kwani wanampigia simu mtu uliempelekea na kumueleza kuwa akachukuwe pesa zake. Akizichukua pesa tu wewe huku ughaibuni utaletewa email msg pamoja na SMS msg kukujulisha kuwa jamaa yako uliempelekea pesa Zenj keshachukuwa pesa kutoka PBZ Ltd. Kwahivyo, hunahaja ya kupiga simu ZNZ ukagharimika zaidi!
Ni process rahisi sana na haichukuwi hata dakika 2 kuimaliza.

Pia, ifahamike kuwa tunaweza kufungua foreign currency accounts pale PBZ wakati tupo huku, na kama mtu anataka msaada basi atujulishe tu. Kwavile kupeleka pesa Zanzibar sasa kumerahisika, tutawaomba PBZ wakubali kama itawezekana tupeleke pesa moja kwa moja kwenye accounts zetu za foreign bila ya hizo pesa kubadilishwa kwanza into Shillings. 

OMBI:
Tunachoomba ni kuwa kila mtu amjulishe mwengine juu ya hio address ya website ya World RemitPia, tumetoa maelezo ya hapo juu kabla ya mkutano kwasababu tunataka watu waitembelee hii website na wajaribu kutaka kutuma pesa Zanzibar hata kama mtu hataki kupeleka pesa hivi sasa. Just jiandikishe tu kwenye website ili ukipata emergency ya kupeleka pesa utakuwa hunahaja tena ya kupoteza muda kwa registration. Kama mtu atapata matatizo wakati yupo kwenye website basi ataweza kutuuliza kwenye mkutano, kwani tutajaribu kuja na laptop ili kufahamisha zaidi. Mtu pia anaweza kwa wakati wowote ule kuwasiliana na Shk Omar (416.732.5301) au na mimi (416.438.7857) kwaajili ya maelekezo na maelezo zaidi kuhusu upelekaji wa pesa nyumbani kupitia PBZ Ltd.

Sote tunajua kuwa hatuna uwezo wa kuisaidia nchi yetu ya Zanzibar kama vile ambavyo tungelipendelea, lakini kila mtu anapeleka pesa nyumbani kwa ndugu, wazee na jamaa zetu. Kama tutazipitisha hizo pesa tunazopeleka kwa njia ya PBZ Ltd huo bila ya shaka utakuwa msaada mkubwa sana kwa nchi yetu, kwani utaiwezesha nchi yetu kupata foreign currency. 

Jirani yetu nchi ya Kenya leo inapokea kama Dollar billion 2 kutoka Wakenya wanaoishi nje kwa kila mwaka. Japokuwa wenzetu wapo wengi nje, lakini pia hii inaonesha kuwa wanamoyo wa kuisaidia nchi yao. In fact, Africa yote inapokea kama 60 billion Dollars kila mwaka, lakini kwa Zanzibar ni sehemu ndogo sana inayofika serikalini kwa faida ya wananchi wetu. Kwa zaidi soma hapa chini: 


Tumejaribu pia kuweka matangazo kwenye blogs kama utakavyoona hapa chini ili wengi wazione hizi habari mpya za kupeleka pesa Zanzibar - sio kwa Wazanzibari wa Canada tu bali wa Ulimwengu mzima:




PBZ Ltd kwa hivi sasa imekuwa connected na Wazanzibari wote waliopo UK, Canada, Europe (EU), Australia na New Zealand na karibu itakuwa connceted pia na Wazanzibari waliopo Marekani (USA).

Tukitaka tushinde na tufuzu katika kuisaidia Zanzibar yetu, then, hii isiwe project ya Wazanzibari wa Canada tu, bali wa Ulimwengu mzima na kwahivyo sote tujitahidini kutangaza kwa mdomo pia kwa kuwaeleza wote wale waliopo karibu yetu wanaoishi nje kuwa wapeleke pesa nyumbani kwa kupitia PBZ Ltd.

Kila la kheri / Othman - ZACADIA / Secretary (416.438.7857)
Chanzo: Zanzibar - Canadian Diaspora Association (Toronto, Canada)

No comments :

Post a Comment