Na Aisha Ngoma, Mwananchi.
Posted Ijumaa,Marchi22 2013.
Posted Ijumaa,Marchi22 2013.
KWA UFUPI
“Tumeona matukio ya kutekwa, kuteswa na kuuawa kwa waandishi wa habari pamoja na wanaharakati ni mwendelezo wa kubinywa uhuru wa vyombo vya habari.
Marcossy Albane.
Dar es Salaam. Mwanaharakati ambaye pia ni Mkurugenzi wa Civil and Political Rights Watch, Marcossy Albanie ameeleza jinsi alivyotoweka jijini Dar es Salaam baada ya kuwa akifuatiliwa mara tano na watu wasiyojulikana.
Akizungumza na gazeti hili jana, alisema mwaka uliopita alikuwa akifuatiliwa na watu ambao hakujua nia yao.
“Niliwahi kufuatiliwa na gari kutoka Kimara Korogwe hadi Kinondoni Mbuyuni kilipo kituo cha matangazo cha Startv na watu ambao sikuwafahamu, nilipofika ndani ya jengo hilo gari hiyo iligeuza na kurudi ilipotokea “alisema Albanie.
Alisema kilichomtisha zaidi ni kitendo cha siku ya mwisho kabla ya yeye kuamua kutoweka.
Alisema katika siku hiyo, watu watatu walitumia usiku mzima wakizunguka nyumbani kwake.
Alisema kwa sasa amerudi jijini kwa kuwa ameshatoa taarifa polisi juu ya mambo ambayo yanamfanya akose amani ya kufanya kazi zake.
Alisema katika siku hiyo, watu watatu walitumia usiku mzima wakizunguka nyumbani kwake.
Alisema kwa sasa amerudi jijini kwa kuwa ameshatoa taarifa polisi juu ya mambo ambayo yanamfanya akose amani ya kufanya kazi zake.
Albane alisema kwa kipindi hiki amekuwa akitumia muda mwingi kukaa na wafanyakazi wenzake na kuogopa kukaa peke yake kwa kuhofia usalama wake.
Albanie alisema usalama wa waandishi wa habari na wanaharakati unatakiwa kuimarishwa. Alisema mambo yanayoendelea hivi sasa kwa wanahabari ni katika kudhibiti uhuru wa habari nchini hapa
.
.
No comments :
Post a Comment