airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, November 13, 2024

WAPIGA MAKACHU WAMPONGEZA RAIS MPYA WA ZACADIA NA RAIS MPYA WA MAREKANI BW. TRUMP!

WAPIGA MAKACHU maarafu wa Forodhani, kutoka mjini Zanzibar, wamempongeza bi Arafat Ibrahim Mustafa kwa kuchaguliwa kuwa Rais mpya wa Jumuiya ya Diaspora ya Wazanzibari wanaoishi nchini Canada, ijulikanayo kama ZACADIA (Zanzibar-Canadian Diaspora Association).

Wapiga makachu hao pia wamempongeza Bw. Donald Trump kwa kuchaguliwa tena kuwa Rais wa 47 wa Marekani.

Pongezi hizo  walizitoa wapiga makachu hao walipokuwa wakipiga makachu Forodhani mjini Zanzibar,  kama inavyoonekana kwenye video zao za hapa chini.

Tarehe 26 October, 2024, Bi Arafat alichaguliwa na Board of Directors  (BoD) wa Jumuiya ya Zacadia kuchukuwa nafasi ya urais wa Jumuiya hii baada ya Rais wa zamani Shk Omar Ali Said kuachia ngazi kutokana na sababu zake binafsi.

Bi Arafat ni mmoja ya waanzilishi wa Jumuiya ya Zacadia katika mwaka 2011.

Kabla ya kuchaguliwa kuwa Rais bi Arafat alikuwa Chief Secretary wa Jumuiya hii na kabla ya hapo alikuwa Manager wa Management team.

Bi Arafat anayo digrii ya pili (Masters) katika fani ya Community Services & Social Welfare na ni muhitimu wa somo la political science kutoka chuo cha diplomatsia cha Dar Es Salaam, Tanzania.

Above: Bi Arafat Mustafa - The new President of Zacadia

Bwana Donald John Trump ni mfanyabiashara, mjasiriamali wa Marekani aliyezaliwa tarehe 14 Juni 1946, Queens, New York. Alikuwa Rais wa 45 wa Marekani kutoka Januari 20, 2017 hadi Januari 20, 2021. Bw. Trump ni maarufu kama mfanyabiashara wa mali isiyohamishika, akiwa na kampuni ya Trump Organization ambayo inajulikana kwa kujenga majengo maarufu na hoteli duniani kote.

Kabla ya kuingia kwenye siasa, Bw. Trump alijulikana kama mmiliki wa kasino, hoteli, na miradi ya kifahari, na pia alikuwa mwenyeji wa kipindi cha televisheni cha The Apprentice.

Bw. Trump aligombea Urais mwaka 2016 kama mgombea wa chama cha Republican na alishinda uchaguzi dhidi ya Hillary Clinton.
Above: Mr. Donald John Trump - The elected President of  America

Utawala wa Bw. Trump ulijulikana kwa msimamo mkali kuhusu immigration, siasa za biashara za kimataifa, na kubadilisha sera za mazingira na afya. Aliiondoa Marekani kutoka katika makubaliano ya Paris kuhusu mabadiliko ya tabia nchi na alifunga makubaliano ya biashara na nchi kama China na Mexico. Trump pia alisisitiza juu ya "America First", na "Make America Great Again" na alijulikana kwa lugha yake ya moja kwa moja na mtindo wa utawala wa kutokukubali mpango wa kisiasa wa kawaida.

Katika kipindi chake cha urais, Bw. Trump alikumbana na changamoto nyingi, ikiwa ni pamoja na uchunguzi wa kuingilia kati kwa Urusi katika uchaguzi wa 2016. Alikosa kuchaguliwa tena katika uchaguzi wa 2020 aliposhindwa na Rais wa sasa  Rais Joe Biden. Katika uchaguzi wa 2024, Bwana Donald Trump alishinda na tarehe 20 January, 2025 ataapishwa kwa mara yapili kama Rais wa 47 wa Marekani.

Blog hili linaungana na wapiga makachu kutoka kule kwenye kisiwa cha mikarafuu na kumpa hongera Bw. Donald Trump na bi Arafat Mustafa kwa kazi zao nzito!

For more click below:

No comments :

Post a Comment