Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, April 27, 2013

Mbunge na Mwakilishi wapata wakati mgumu mbele ya Dk Shein Zanzibar

NA MWINYI SADALLAH

27th April 2013


Mwinyihaji Makame Mwadini
Mbunge na Mwakilishi wa jimbo la Dimani Dk Mwinyihaji Makame Mwadini na Maulid Sheria wamepata wakati mgumu kutoka kwa wananchi wa Bweleo Mkoa wa Mjini Magharibi Kisiwani Unguja kufuatia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar kuahidi kukutana nao ili kuzungumzia tatizo lao la maji.

Alitaka kujua pia ni kwa muda gani tatizo hilo limeshindwa kutafutiwa ufumbuzi.
Mbunge na Mwakilishi Dk Mwinyihaji ambaye pia Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu, ambao walikuwepo katika ziara ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, walikuwa katika wakati mgumu pale wananchi walipopaza sauti zao kwa mguno baada ya Rais kuwahusisha na mpango wa kulitafutia ufumbuzi tatizo hilo.

Akihutubia wanachama wa CCM baada ya kuzindua shina Na 5 kijiji cha Bweleo, Dk Shein alisema anashangazwa kuona wananchi wakiendelea kutaabika wakati serikali imekwishatoa Sh milioni 58 kutatua kero hiyo ya maji kijiji hapo.

“Nitawaita watendaji wa Mamlaka ya Maji Zanzibar na viongozi wenu wa jimbo akiwemo Mbunge na Mwakilishi kujua fedha hizo zimetumikaje…,” alisema Dk Shein.
Baada ya matamshi hayo miguno toka kwa wananchi ilisikika na kumfanya Dk Shein apate mshangao na kufanya kazi ya ziada ya kuwanusuru viongozi wa jimbo baada ya hali ya hewa kuchafuka mkutanoni.

Hata hivyo, Dk Shein alifanikiwa kuzima hali hiyo kutokana na ahadi aliyoitoa ya kuhakikisha wananchi wa Bweleo wanapata huduma ya maji safi na salama pamoja na uwanja wa michezo kuhakikisha unachongwa ili kuwapa nafasi vijana kuutumia uwanja huo kwa michezo.

Alisema ameshangazwa kuona uwanja huo umewekwa jiwe la msingi siku nyingi lakini kazi ya ujenzi inayoendelea na kusibabisha vijana kushindwa kuonyesha vipaji vyao kutokana na uwanja huo kuwa na mawe.

Akihojiwa na NIPASHE mara baada ya mkutano huo kumalizika Mbunge wa Dimani Sheria alisema tatizo la uhaba wa maji linachangiwa na wakulima wa mbogamboga katika jimbo hilo wanaojiunganishia mabomba toka katioka bomba kuu la Dimani na kuwakosesha maji wananchi wa Bweleo.

Alisema tatizo hilo amekuwa akitumia muda mwingi kulifuatilia katika mamlaka ya maji Zanzibar lakini amekuwa akipewa ahadi hewa za utakelezaji jambo ambalo linasibabisha kutoeleweka kwa wananchi wa Bweleo.

“Wameguna wakiamini sisi ndiyo tatizo la kukosekana kwa maji, najua wanataabika ila Zawa wanatukaanga na kutuhasimisha na wananchi, hatujakata tamaa ya kuwatumikia,” alisema Sheria. 
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment