Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, May 9, 2013

Ahadi 10 za TANU

Flag of Tanganyika.svg

Angalia zinavyovunjwa na wajanja wetu wa leo:

Ahadi 10 za TANU:

1. Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja...............hapana, angalia dini kwanza.
2. Nitaitumikia nchi yangu na watu wake wote..... nitaitumikia familia yangu na washikaji zangu wote.
3. Nitajitolea nafsi yangu kuondoa umaskini, ujinga, magonjwa na dhuluma..........................kuondoa maadili yote ya taifa hili.
4. Rushwa ni adui wa haki. Sitapokea wala kutoa rushwa..............rushwa ni sehemu ya maisha, nitapokea na kutoa kila ninapopata nafasi.
5. Cheo ni dhamana. Sitakitumia cheo changu wala cha mtu mwingine kwa faida yangu..............Cheo ni ulaji; watanikoma.
6. Nitajielimisha kwa kadiri ya uwezo wangu na kutumia elimu yangu kwa faida ya wote.....................nitaiba vyeti na kugushi majina.
7. Nitashirikiana na wenzangu wote kuijenga nchi yetu................nitashirikiana na wageni kuibomoa nchi.
8. Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko......nitasema uongo, nitakuwa mfitini, nitapenda majungu, na nitakuwa mzushi.
9. Nitakuwa mwanachama mwaminifu wa TANU na raia mwema wa Tanganyika na Afrika.....................nitakuwa mwanachama mwaminifu wa makundi ya mafisadi na raia mwizi.
10.                 Nitakuwa mtiifu na mwaminifu kwa Rais wa Serikali ya Tanganyika..............................nitakuwa mtiifu kwa wanaonihonga.

Maskini nchi yetu! Tuipiganie sasa! 

Chanzo: Wanabidii Blog

No comments :

Post a Comment