Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, May 4, 2013

Dk.Shein-SMZ inawatambua walioshirikiana na Uamsho

NA MWINYI SADALLAH

4th May 2013


Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein amesema Serikali yake inawatambua watu walioshirikiana na Jumuiya ya Uamsho kuanzisha vurugu za kisiasa na kuacha kufanya kazi za kiroho kinyume na malengo ya kusajiliwa kwa jumuiya hiyo visiwani Zanzibar.

Dk Shein alitoa tamko hilo kwa mara ya kwanza la watu walioshiriki kuandaa vurugu hizo tangu zilipotokea mwezi Mei na Oktoba, mwaka jana, na kusababisha uharibifu wa mali na askari polisi, Said Abdularahman, kuuawa kwa kipigwa mapanga.

Akihutubia mkutano wa hadhara, Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja, Dk Shein, alisema jumuiya ya Uamsho iliwalazimisha polisi kutumia nguvu baada ya serikali kuwakanya na kuwaonya zaidi ya mara tatu wasitishe vurugu zao.

Alisema Serikali ina mikono mirefu na tayari imekwishawafahamu wote walioandaa mpango wa vurugu kwa kusingizia kero za Muuungano na wakati ukifika haitosita kuwachukulia hatua za kisheria ili kulinda amani na umoja wa kitaifa Zanzibar.

Alisema kifungu cha 19 (1) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 kimesema kila mtu anastahili kuwa na uhuru wa mawazo, wa imani na wa uchaguzi katika mambo ya dini pamoja na uhuru wa kubadilisha dini au imani yake bila ya kuingiliwa.

Alisema endapo yakizuka matatizo mengine yenye kutishia amani ya nchi Serikali yake itawatafuta wale wote waliohusika na kuwachukulia hatua za kisheria.

Alisema nyumba za ibada zinajulikana na wananchi wako huru kuzitumia lakini kamwe serikali yake haitakubali jumuiya za kidini kutumiwa kwa harakati za kisasa au siasa kufanya kazi za dini.

Aliwaeleza wananchi kuwa mabadiliko ya katiba ya Zanzibar mwaka 2010 yalikusudia kumaliza mpasuko wa kisiasa ambao ulikuwa ukijitokeza kila baada ya uchaguzi mkuu mmoja kumalizika.
Dk Shein alisema kilichofanyika Zanzibar ni kupatikana kwa serikali ya umoja wa kitaifa na si mseto kama baadhi ya wengine wanavyopenda kuiita.

Alisema kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa hakujafuta malengo ya Mapinduzi ya mwaka 1964 na sasa inaongozwa chini ya sera za CCM, dira ya maendeleo ya 2020, mpango wa kukuza uchumi na kupunguza umasikini Zanzibar (Mkuza) pamoja kutimiza malengo ya milenia.

Dk. Shein alitoa tamko hilo baada ya Katibu Mwenezi wa Jimbo la Matemwe, Mosi Mati Nadhari, kutaka jumuiya ya Uamsho ifutwe na viongozi wake wadhibitiwe kwa vile wamekuwa chanzo cha vurugu zilizotokea na kuathiri amani na maendeleo ya sekta ya utalii. 
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment