dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, June 15, 2013

Kamati ya Chenge yafanikisha ongezeko la bajeti

NA MASHAKA MGETA

14th June 2013


Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Andrew Chenge
Kamati ya Bunge ya Bajeti  imefanikisha ongezeko la  Sh. bilioni 513 kati ya bilioni 654.21 zilizoombwa kupitia kamati za bunge za kisekta kwa wizara zilipowasilisha bajeti bungeni.

Taarifa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Andrew Chenge, ilisema uamuzi wa kuongeza fedha katika baadhi ya mafungu, yalifikiwa baada ya uchambuzi, mijadala na mashauriano yaliyowahusisha wadau tofauti.

Wadau hao ni kamati ya bajeti, wenyeviti wa kamati za kisekta, mawaziri na maoni na ushauri wa wataalamu wa Hazina na tume ya mipango.

Hii ni mara ya kwanza kwa Bunge kuitumia Kamati hiyo katika kuijadili na kuidhinisha bajeti ya serikali.

Kwa mujibu wa Chenge, fedha zilizoidhinishwa ni Sh. bilioni 184.5 katika fungu 49 (Wizara ya Maji), Sh. bilioni 30 katika fungu la 62 (Uchukuzi) na Sh.i bilioni 30, fungu la 44 (Viwanda na Biashara).

Pia zipo Sh. bilioni9 katika fungu 96 la Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
Chenge alisema, fedha nyingine ni nyongeza katika mafungu yaliyoidhinishwa na Bunge bila kupitia Kamati ya Bajeti.

Mafungu hayo na idadi ya fedha kwenye mabano ni fungu 35, idara ya kurugenzi ya mashtaka (Bilioni 10), fungu 40, mfuko wa mahakama (bilioni 20).

Aliongeza kuwa maombi mengine ya Sh. bilioni 370.71 yaliridhiwa na kamati yake, na kuwasilishwa serikalini ambapo ilikubalika kutolewa Sh. bilioni 229.5.

Kiasi cha fedha hizo kilielekezwa katika fungu 15 la tume ya usuluhishi (milioni 350) na fungu 43 kwa ajili ya ruzuku ya mbolea na mbegu bora katika Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika (bilioni 21.15).

Pia kuna fungu la 53 la Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto kwa ajili ya Mfuko wa Wanawake (bilioni 2).

Fungu jingine ni la 58, Wizara ya Nishati na Madini-umeme vijijini (bilioni 186) na fungu 99, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (bilioni 20).

VYANZO VYA MAPATO
Chenge alisema kamati yake haikuweza kujua vyanzo vipya vya mapato vinavyopendekezwa na serikali.

Alisema hali hiyo ilijitokeza kwa sababu kitabu cha kwanza cha makadirio ya mapato hakikutolewa na serikali na kwamati hiyo, hadi ilipotayarisha taarifa yake kwa Bunge.

Chenge alisema mafungu mengine yaliyoombewa nyongeza na kamati za kisekta, hayakufanikiwa kutokana na upungufu wa fedha usiolingana na mahitaji.

Alisema kamati yake ilibaini mafungu mengi kutotengewa fedha ya kutosha katika miradi ya maendeleo, hivyo kusababisha isitekelezwe na kukamilika kwa wakati.

NIDHAMU YA BAJETI
Chenge alisema kuna umuhimu wa kusisitiza nidhamu katika kutayarisha, kupitisha na kusimamia utekelezaji wa bajeti ya serikali kama inavyoidhinishwa na Bunge.

Alisema, Kamati ya Bajeti ilibaini kuwa fedha zinazoinishwa na Bunge na kutolewa na Hazina, mara nyingi inapelekwa kwenye maeneo yasiyo ya vipaumbele vilivyokusudiwa.

Pia alisema kasma za vipaumbele zimekuwa hazitengewi fedha za kutosha, badala yake (fedha hizo) kuelekezwa maeneo yasiyokuwa ya lazima.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment