dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, June 15, 2013

JULIUS NYERERE INTERNATIONAL AIRPORT

Uwanja wa ndege wa JK Nyerere wakabiliwa na msongamano

15th June 2013


Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius K.Nyerere(JNIA)
Uwanja wa ndege wa  kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere (JNIA), wa  jijini Dar es Salaam unakabiliwa  msongamano wa abiria kutoka na  uwezo mdogo na miundombinu michache ya kuhudumia wasafiri.
Awali uwanja huo uliojengwa miaka 20 iliyopita ulikadiriwa kuhudumia  abiria  milioni 1.5 kwa mwaka  lakini sasa unapokea abiria milioni 2.1 ambalo ni ongezeko la zaidi ya wasafiri  600.
Mkurugenzi wa kiwanja hicho, Moses Malaki , aliiambia NIPASHE jana mjini Bagamoyo , wakati wa  mkutano mkuu wa mameneja wa mamlaka ya viwanja vya ndege nchini (TAA).
 
Alisema  kutokana na hali hiyo, mamlaka hiyo imekamilisha mchakato wa kutafuta fedha na mkandarasi kwa ajili ya kupanua uwanja huo  na kujenga jengo jipya la abiria mradi unajulikana kama ujenzi wa Terminal III.Upanuzi huo utaongeza uwezo wa kiwanja hicho cha kimataifa kuchukua abiria hadi million tano kwa mwaka na   unategemewa kuanza kujengwa na kampuni ya Uholanzi ya BAAM international kwa kipindi cha miaka  mitatu.
 
Kadhalika aliongeza kuwa kuanza kwa safari za Fast Jet nako kumechangia mahitaji wa upanuzi huo kwani wakati kiwanja hicho kinajengwa zaidi ya miaka ishirini iliyopita, kilisanifiwa kwa ajili ya  abiria million 1.5  kwa mwaka.
 
Alisema kuwa kwa sasa mchakato unaoendelea juu ya ujenzi wa jengo hilo ni kukusanya maoni ya wadau, na kazi ya usanifu kabla ya ujenzi huo kuanza rasmi.
 
Naye Mkurugenzi wa rasilimali watu na utawala wa TAA, Laurent Mwigune, akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu alisema  ukarabati na ujenzi wa jengo hilo la abiria la Terminal III, ni sehemu ya mpango mkubwa wa mamlaka hiyo wa kukarabati na upanuzi wa viwanja kadhaa vya ndege nchini ili viweze kukidhi mahitaji ya usafiri wa kisasa.
 
Alivitaja viwanja vingine amabavyo vipo katika mpango wa ukarabati na uboreshaji kuwa ni pamoja na viwanja vya ndege vya Kigoma, Tabora na Mafia ambavyo ukarabati wa awamu ya kwanza ya viwanja hivyo umekamilika.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment