NA MWINYI SADALLAH
13th June 2013
Hayo yalisemwa jana na Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko, Nassor Ahmed Mazrui wakati akijibu swali katika Kikao cha Baraza la Wawakilishi kilichoanza jana Chukwani kisiwani Unguja.
Mazrui, alisema wakulima wa mwani wameanza kuathirika na ukosefu wa soko la uhakika na kusababisha kubakia na shehena ya mwani mkavu kwenye nyumba mwao.
Alisema kwamba bahati mbaya Mwani unapokaa muda wa miezi minne tangu kuvunwa bila ya kuuzwa, kiwango cha ubora upungua.
Alisema wakati umefika kwa mwani kutumika kama malighafi ya kuzalisha bidhaa nyingine kama vyakula, sabuni badala ya kuuza kama ulivyo katika soko la Dunia.
Akijibu swali la msingi la Mwakilishi wa Viti Maalum, Bikame Yussuf Hamad, Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Thuwaiba Endington Kisasi, alisema Wizara yake imeanza kufanya utafiti wenye lengo la kusarifu Mwani nchini kabla ya kuuzwa nje.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment