dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, June 23, 2013

WABUNGE HAWANA KAZI!

Wabunge nusura wazichape

23rd June 2013


  Ni wa CCM na Chadema
  Kisa mabomu ya Arusha
Mbunge wa Nyamagana (CHADEMA), Ezekiel Wenje (Wapili kushoto), akimuondoa mbunge wa Iringa Mjini (CHADEMA), Mchungaji Peter Msigwa (Wapili kulia), baada ya ``kukwaruzana`` kwa maneno na mbunge Mwigulu Nchemba.
Siasa za uhasama kati ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), zimeingia katika sura mpya baada ya wabunge wake kutaka kuchapana makonde hadharani.
Hali hiyo ilijitokeza jana baada ya Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba (CCM), kurushiana maneno na Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Msigwa (Chadema) nje ya ukumbi wa St. Gasper mjini hapa.
Sekeseke hilo lilitokana na Mchungaji Msigwa kumtuhumu Mwigulu kuwa CCM wana uchu wa madaraka ndiyo maana wanatumia kila mbinu kuua nguvu za Chadema.
Wabunge hao walikuwa wanahudhuria semina ya Chama cha Wabunge cha Kupambana na Ukimwi, mjini hapa.
Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya tukio la mlipuko wa mabomu uliotokea jijini Arusha katika mkutano wa hadhara wa kufunga kampeni ulioandaliwa na Chadema ambapo Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe alitamka kuwa polisi ndiyo waliohusika na tukio hilo.
Akizungumza na NIPASHE, Mwigulu alisema Mchungaji Msigwa alikasirishwa na mchango wake alioutoa katika bajeti ya serikali kuu ambayo itahitimishwa kesho.
“Mimi nilichosema bungeni kuwa inawezekana kabisa matukio hayo ya Arusha yanasababishwa na mambo mbalimbali ikiwamo watu kutoka nje kutumia mwanya wa dini na siasa kuua biashara ya utalii,”alisema.
Alisema pia kuwa tukio hilo huenda limesababishwa na vyama vya siasa ambavyo vinalenga katika kuichonganisha serikali na wananchi.
“Mimi sijashambulia opposition (upinzani), kama anavyodai, ninachofanya ni kuwaeleza ukweli wananchi, kama hivyo ndivyo kukiua chama basi na kife kwa sababu lengo la kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi si kusababisha mauaji kwa Watanzania,” alisema.
NIPASHE pia ilimtafuta Mchunguji Msigwa, kuzungumzia sakata hilo na kukiri kumwambia Mwigulu kuwa CCM ina uchu wa madaraka.
Alisema wakati wakiwa nje ya ukumbi huo, Mwigulu alipita mbele yake huku akichekacheka kitendo kilichomfanya atafsiri kuwa alikuwa akimdhihaki kutokana na vitendo vilivyotokea Arusha.
"Alipita pale akawa ana cheka cheka, mimi niliona ananidhihaki wakati kuna mambo mazito yametokea halafu mtu anapita na kuchekacheka," aliongeza.
Matukio ya wabunge kuonyeshana ubabe yameibuka siku za hivi karibuni ambapo juzi mbunge mmoja anadaiwa kumtolea mwenzake matusi ya nguoni na kutaka kumpiga wakati wakiwa nje ya viwanja vya bunge.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

No comments :

Post a Comment