dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, June 21, 2013

Wakamatwa na bunduki za kutosha platuni

NA MWANDISHI WETU

21st June 2013

Kamanda wa polisi mkoa wa Kigoma, Frasier Kashai
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma linawashikilia watano kwa tuhuma za kukutwa na bunduki 34 na risasi 61 zinazosaidikiwa kutumika katika matukio ya ujambazi.

Kamanda wake, Frasier Kashai alisema kuwa watuhumiwa hao (majina tunayo), walikamatwa  bunduki tatu aina ya SMG , Shortgun mbili na magobori 29 na risasi 61  Juni 17 mwaka huu  saa 12 jioni katika Kijiji cha Lusohoko Wilaya ya Kibondo.

Alisema kukamatwa kwao kunatokana na msako wa polisi baada ya kukithiri kwa matukio ya kuteka magari na unyanganyi wa kutumia silaha katika barabara kuu wilayani humo.

Alisema katika matukio hayo, watu wawili walijeruhiwa kwa risasi kupigwa risasi  katika Vijiji vya Kibingo na Biturana na kuporwa mali.

Aliwataja waliojeruhiwa kuwa ni  Ngendabanyi kwa Andrea (35) kwa kupigwa risasi mguu wake wa kulia na Mathias Christopher (45) mkono  wa kushoto kisha kulazwa Hospitali ya Wilaya ya Kibondo kwa matibabu.

Alisema watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.

 
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment