NA MWINYI SADALLAH
28th August 2013
Mwinyi Issa Makame, mkaazi wa Kiembesamaki alisema Mansoor hakuwa mwanachama muaminifu wa CCM kutokana na kauli zake zilizokuwa zikikinzana na sera pamoja na ilani ya chama hicho.
Teddy Peter William, mkaazi wa Buyu alisema CCM itatenda kosa baya na la kiuonevu ikiwa wamemchukulia hatua za kididhamu yeye peke yake na kuacha wengine ambao walikuwa wakitoa maoni na msimamo kama yake.
“Nimeshangaa kusikia ni Mansour ndiye aliyetolewa kafara na wengine kuachwa,” aliongeza Teddy.
Said Shaaban, mkazi wa Mbweni Mtrekta, alisema atabaki kushngazwa kuona ni kigezo gani kilichotumika cha kumfukuza Mnsour na kuachwa kwa waziri wa zamani wa Sheria, Mzee Hassan Nassoro Moyo.
“Ameunda kamati ya maridhiano na kusema ina uwakilishi wa CCM na CUF ni uhuni wa kisasa usiovumilika, vipi aachwe na kuhukumiwa Mansoir?” alihoji Shaaban.
Katibu wa Sisa na Uenezi wa CCM wilaya ya Mjini Unguja Baraka Shamte, alisema uamuzi wa NEC ni wa kihistoria na kwamba hakutakuwa na athari yeyote kwa siasa za Zanzibar upande wa CCM.
Shangwe na vigelegele vilianza kuibuka juzi jioni baada ya habari za kufukuzwa kwa Mansour na baadhi ya wanachama wa CCM katika jimbo la Kiembesamaki walifanya karamu ya chakula kwenye matawi ya CCM.
Hata hivyo, wapo baadhi ya vijana wanaopinga kitendo cha NEC kumvua uanachama Mansoor huku wakiunga msiomamo ulioonyeshwa na Mwaklilishi huyo akiwa nje na ndani ya Baraza la Wawakilishi akiitetea Zanzibar kupata mamlaka kamili.
Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM wilaya ya Dimani kisiwani Unguja imeunga mkono uamuzi huo.
Katibu wa Wilaya ya Dimani, Yussuf Suleiman, alisema UVCCM wilaya hiyo imepata faraja na imani kuona CCM kikifuata mkondo wa nidhamu .
Mbunge wa Dole (CCM), Sylvester Mabumba, alisema: “Hapana, hapana, niulize chochote nitatoa maoni lakini hilo waulize viongozi wa juu wa chama.”
Mbunge wa Amani (CCM), Mussa Hussein Mussa, alisema: “Sina maoni, chama kina taratibu zake kama taratibu zimefuatwa ni sawa tu, lakini mimi sijui walizungumza nini.” Mbunge wa Jang’ombe (CCM), Hussein Mussa Mzee, alisema: “No comments please (sina maoni tafadhali).”
Mwingine aliyekataa kuzungumzia suala hilo, ni Mbunge wa Mpendae (CCM) Salim Abdullah Turky
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment