zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, August 21, 2013

Dkt. Shein muwajibishe Mwanasheria – UVCCM

Naibu Katibu Mkuu UVCCM Zanzibar Shaka Hamdu Shaka, akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake Gymkana Mjini Zanzibar kuliani kwake ni Mkuu wa Utawala UVCCM afisi ya Zanzibar Mbaruk Mrakib, kushoto Katibu Idara ya Oganaizeshen Asya Sharifu.
Naibu Katibu Mkuu UVCCM Zanzibar Shaka Hamdu Shaka, akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake Gymkana Mjini Zanzibar kuliani kwake ni Mkuu wa Utawala UVCCM afisi ya Zanzibar Mbaruk Mrakib, kushoto Katibu Idara ya Oganaizeshen Asya Sharifu.
 Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Zanzibar  imemtaka  Rais wa Zanzibar  Dk Ali Mohamed Shein kumfukuza kazi Mwanasheria Mkuu wa Serikali  ya Mapinduzi Zanzibar, Othman Masoud Othman kufuatia matamshi yake  yanayokinzana na kupingana na dhamana aliyopewa na Rais aliyemteua.
Msimamo huo umetolewa leo na Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika katika Afisi Kuu ya Jumuiya hiyo huko Gymkhana mjini Unguja.
Shaka amesema matamshi ya kutaka muundo wa Muungano wa Serikali tatu yamesigana na dhamana pamoja na kukiuka amana ya kimajukumu ya kikatiba  aliyopewa ya  kusimamia na kuitetea ipasavyo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Kijana huyo aliwaambiwa waandishi wa habari kwamba  kitendo cha kushiriki kongamano na kujitambulisha kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali huku akiweka  msimamo  na kupendekeza  muundo wa Serikali tatu badala ya mbili kwa  Serikali anayoitumikia kama mtumishi  wa SMZ  ni kukiuka maadili ya ajira yake ya kazi.
UVCCM imesema kama kweli Othman ni muungwana, anayeheshimu utetezi na msimamo wake wa kushabikia muundo wa Serikali tatu aonyeshe ujasiri na kujiondoa Serikalini mara moja na kasha ndio aweze kuendeleza kile anachokitetea. 

Mwansheria wa Zanzibar Bw. Othman Masoud  - Aichachafya CCM na UVCCM

Aidha Naibu Katibu Mkuu huyo wa UVCCM amesema ni kinyume na taratibu kwa msaidizi wa Rais upande wa masuala ya sheria aliyeapa kumsaidia, kuilinda katiba ya Zanzibar, kuitetea na kuihifadhi akipita njia tofauti ya kisera na Rais wake ambaye amemteuwa.
Shaka amesema ni vyema Mwanasheria Mkuu  akaipinga Serikali ya Mapinduzi Zanzibar  akiwa nje ya serikali kuliko akiwa ndani kwani kubaki ndani ya chombo hicho kazi yake si kupinga bali ni kushauri au kusema baada ya kushauriana na Rais.
Aliongeza kwamba kuna haja kwa Rais  Dk Shein kumfukuza kazi Mwanasheria Mkuu huyo  kwa kitendo chenye ishara ya usaliti na kubeza matakwa ya kisera ya Rais aliyemteua na kumpa dhamana alionayo.
Hata hivyo Naibu Katibu mkuu ambaye aliitisha mkutano na waandishi akiwa na baadhi ya viongozi wenzake wa vijana alipoulizwa ikiwa Rais atakataa ombi la jumuiya hiyo ya kumuoandoa Mwanasheria Mkuu wake watachukua hatua gani, alijibu kwamba  Jumuiya yake itafanya  maandamano ya amani ya kumshindikiza Rais amuondoe Mwanasheria Mkuu huyo Serikalini.
Kwa upande wa maoni juu ya kinachoelezwa kuachia ngazi au kufukuzwa na Jumuiya ya Vijana wa CCM, Mwanasheria Mkuu  Othman Masoud Othman alipopigiwa siku ili atoe maoni na msimamo wake juu ya hilo aliomba radhi kutoakna na kuwa hangeweza kuongea chochote kutokana na kuwepo safarini akielekea nchini Qatar. Lakini aliahidi kutoa ufafanuzi wa suala hilo iwapo atapata nafasi nzuri ya kimawasiliano.                                                                                              
Hivi karibuni Mwanasheria Mkuu huyo alikaribishwa kuhutubia katika kongamano lililoandaliwa na vijana wa vyuo vikuu Zanzibar na akatoa mifano kadhaa ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambapo alisema waziwazi kwamba Muungano uliopo hauna tija na unapaswa kubadilishwa mfumo wake ili kwenda sambamba na dhana ya kuungana kama nchi mbili huru.
Aidha Othman alisema Msingi wa Muungano wa Tanzania ni kuungana kwa nchi mbili huru, Tanganyika na Zanzibar. na lengo la kuungana kwa nchi mbili hizo ni kufanya mambo yao pamoja na kupata faida zaidi na sio nchi moja kuitawala nchi nyengine kama ilivyo sasa.
Kauli hiyo na nyengine za Othman kama aliposema kwamba Zanzibar si mkoa wala wilaya bali ni nchi kamili na katika Muungano, walioungana walikubaliana baadhi ya mambo kufanya pamoja na sio Zanzibar kuwa jimbo la Tanganyika, ndio zilizowaudhi baadhi na watu hasa wafuasi wa CCM wakiwemo vijana na kulazimika kumtaka Dk Shein amuwajibishe kikazi mtumishi wake huyo.

Chanzo: Nipashe

No comments :

Post a Comment