zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, August 31, 2013

Hospitali yahitaji milioni 200/- kukidhi matibabu

NA DUNSTAN BAHAI

31st August 2013


Hospitali ya Wilaya ya Pangani, inahitaji Sh. milioni 200 kwenye bajeti yake ili kukabili changamoto za afya wilayani hapo.

Akizungumza na waandishi wa habari wa Chama cha Waandishi wa habari za Vijijini na Mazingira (TARUJA), Kaimu Mganga Mkuu wa hospitali hiyo, Dk. Frank Makunde, alisema kutokana na ufinyu wa bajeti, wanashindwa hata kujenga vituo vya afya.

Jopo hilo lilikuwepo wilayani Panganikujifunza uandishi wa habari za vijijini, mafunzo yaliyofadhiliwa na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA).

Dk. Makunde alisema wilaya ina hospitali ya wilaya moja, zahanati 17 za serikali na ya binafsi moja huku kukiwa na kituo kimoja cha afya.

Alisema wilaya itashindwa kutekeleza mpango wa serikali wa kuwa na zahanati moja kwa kila kijiji kutokana na fedha wanazopokewa kutokidhi matakwa hayo.

Alilazimika kutoa ufafanuzi huo baada ya wananchi wa kijiji cha Buyuni kueleza jinsi wanawake wanavyojifungua njiani katikatiya msitu wa Hifadhi ya Taifa ya Saadani (SANAPA) wakati wakifuata huduma hiyokwenye kijiji kingine kilichopo umbali wa zaidi ya kilomita 10.

Dk. Makunde alisema tayari Manispaa imeshaingia mkataba na mfanyabiashara mmoja ambaye ameshaanza kujenga zahanati katika
kijiji hicho.

Alisema ujenzi huo ni wa kusuasua kwa kile alichodai kuwa inawezekana uwezo wa upatikanaji wa fedha wa mfanyabiashara huyo umeyumba kidogo.
Hata hivyo alisema tayari vijiji kadhaa
viko kwenye mpango wa kujengewe zahanati.

Kijiji cha Buyuni chenye jumla ya watu 270 ambao shughuli yao kubwa ya kujiletea uchumi ni uvuvi, kinakabiliwa na changamoto
nyingine zikiwemo za huduma duni za elimu na uchumi. 
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment