UkiwaNewYork City uwezi kuboreka kwani kuna mambo mengi tu ya kukufanya uwe busy kama kibaraka yakufurahisha na kukuachia kumbukumbu kwani akuna kama New York city. Hapa ni sehemu ya kupandia boat la kukupeleka Statue Liberty.
Boat hilo likiwafuhata watu baada ya kuwashusha uko Statue Liberty
Hapa ndiyo watu ushushwa na kulizunguka eneo hili kwa kupiga picha na kujua history ya sehemu hii muhim sana ukipata nafasi kutembelea New York City.
awa ni watu wamevaa ka sanamu hilo kama unavyo ona unaweza kupiga nao picha kwa kuwalipa kitu kidogo hili na wao wasikae bure hapo juani. Mambo ya New York hayo.
New York pia ni makao makuu ya Umoja wa mataifa na jengo hili ndiyo makao makuu ya umoja huo wa mataifa wenye nguvu dunia. Viongozi duniani kote kila mwaka ukutana hapa na kujadiri mstakabri wa dunia unavyooenda. Kama unavyoona kuna bendera ya Tanzania katika ta bendera za mataifa mawili makubwa dunia jibu unalo hapo.
Hapa ni geti kuu la kuingilia kwenye mjengo huo wa umoja wa matifa
New York kuna basi kubwakama hizi na unalipia na kuzunguka uku ukipitishwa sehemu mbali mbali katikati ya Time Square.
Baskeli nazo zipo unanunua kadi maalum na kisha unaswep baskeli inatoka unazunguka nayo mtaani hadi uchoke. Hapa mdau Maro akipata ukodak na uku akisema akirudi bongo na yeye atafungua mradi kama huu sasa swali wakodishaji tarudisha hili mtu mwingine apate nafasi ya kukodisha au???
Usije ukafikiria kuwa ni sanamu ni watu hao wako kazini ukipita dondosha ulichnazo nyumbani mama watoto maji ya ugali yapo jikoni baba kazini atarudi na pesa ya mboga maisha yana songa hii ndiyo NYC.
Pilika pilika ndani ya New York ni burudani tosha kama unavyoona chunguza picha na utaona tu mambo ya kukufanya ushangae ukiwa New York hasa kipindi kama hiki cha summer.
Jamaa nae akitoa pesa yake hili kupata ukodak nahuyo dada mwenye vinguo vya chumbani. na mwili mzima akiwa amepanga rangi hili kupunguza ukali wa kivazi chake. Hii yote anafanya hili hapate pesa na kuendesha maisha yake ya kila siku ndani ya New York City.
Kapozi na mabegi yake mrembo pembeni mechapata ukodak wa kumbukumbu akiwa new York.
Karibu New YorkCity nyumbani kwa Umoja wa Mataifa na jiji la wasilo lala mchana usiku kucha
Chanzo: Vijimambo
No comments :
Post a Comment