zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, August 29, 2013

Rahma Al-Kharoosi Ateuliwa kuwakilisha Comoro…!

Rahma Al-Kharoosi akiwa na Rais wa Comoro mwenye kanzu na kofia, Ikulu ya Moroni
Rahma Al-Kharoosi akiwa na Rais wa Comoro mwenye kanzu na kofia, Ikulu ya Moroni
…Apokewa kwa kishindo Comoro
SULTAN wa Oman, Qaboos bin Said Al Said, amekubali uteuzi wa Rahma Abdulrahman Al Kharoosi (Malkia wa Nyuki) kuwa Balozi wa heshima wa Jamhuri ya Comoro nchini mwake, imefahamika.
Katika waraka wake wa kukubali uteuzi uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Comoro, Dk Ikililou Dhoinine, Sultan Qaboos alitoa maelekezo kwa watendaji wake kumpa ushirikiano Rahma katika majukumu yake mapya.
Katika waraka huo wa April 20, 2013 ambao nakala tumeiona, Sultan Qaboos, amesema amekubali uteuzi huo na kuwataka wote wanaohusika kumpa ushirikiano kulingana na kanuni na mikataba ya Kimataifa.

Rahma Al-Kharoosi akiwa na ujumbe wa serrikali ya Comoro ulioongozwa na Rais wa visiwa hivyo.
Rahma Al-Kharoosi akiwa na ujumbe wa serikali ya Comoro ulioongozwa na Rais wa visiwa hivyo.
Wiki iliyopita Rahma alifanya ziara rasmi ya kwanza katika visiwa vya Comoro na kupata mapokezi makubwa kutoka kwa serikali na wananchi wa visiwa hivyo, ikiwa ni pamoja na kufanya mazungumzo na Rais Dhoinine na Gavana wa  Anjouan, Anissi Chamsidine.
Mbali ya viongozi hao wa juu wa serikali na mawaziri wao, Rahma alikutana pia na Spika wa Bunge la Comoro, Bourhane Hamidou, na kutembelea maeneo ya uwekezaji na huduma za kijamii katika kisiwa cha Anjouan.
Rahma Al Kharoosi ambaye hivi karibuni alichaguliwa kuwa mjumbe wa kamati ya utendaji ya Simba, alifanikisha ziara ya  Simba nchini Oman.
Rahma pia ndiye mmiliki wa RBP Oil, aliwahi kuwa mdhamini mkuu wa Twiga Stars, pia aliwahi kuwa mmoja wa wamiliki wa African Lyon na ni kati ya wapenda michezo.
Ndiye aliyeidhamini safari yote ya Simba Oman kwa kuwalipia hoteli, tiketi pamoja na chakula kwa muda wote wa siku 14.
Rahma Al-Kharoosi akiagana na viongozi  wa serikali ya Comoro ulioongozwa na Rais wa visiwa hivyo.
Rahma Al-Kharoosi akiagana na viongozi wa serikali ya Comoro wakiongozwa na Rais wa visiwa hivyo.

Chanzo: ZanzibariYetu

No comments :

Post a Comment