zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, August 31, 2013

Suala la mansour Bungeni Dodoma’

Written by   //  31/08/2013

Mansour bungeni

Suala la Halmashauri kuu ya CCM (Nec) kumvua uanachama Himid jana lilibuka bungeni mjini Dodoma.
Sakata la Himid liliibuka katika kipindi cha maswali kwa Waziri mkuu ambapo Mbunge wa Micheweni, Haji Khatibu Kai (CUF), alihoji uhalali wa CCM kuzuia wanachama wake kutoa maoni yao kwa uhuru.
Katika maswali hayo ya papo kwa hapo, Mbunge huyo alisema kwa mujibu wa Ibara ya 18(1) ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni yake na mawazo yake.
“Na kwa kuwa Waziri ama kiongozi yeyote kwa mujibu wa ibara hiyo yuko huru kuwa na maoni yoyote. Unatoa kauli gani kwa chama cha siasa kuwazuia watu kuwa huru na kutoa maoni hasa yanayohusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar,” alisema Mbunge huyo.
Hata hivyo Waziri Mkuu Mizengo Pinda alipiga chenga kujibu swali hilo akisema asingeweza kulijibu labda kama mbunge huyo atakuwa wazi na kukitaja chama kinachofanya vitendo hivyo.
“Mheshimiwa Naibu spika kwa bahati mbaya ameweka usiri mwingi sana sasa sielewi chama gani hicho cha siasa na kimewazuiaje watu. Ndio maana ungetusaidia kabisa chama gani cha siasa kilifanya hivi,”alisema Pinda.
Hapo ndipo mbunge huyo aliposimama na kusema,” alisema.
Akipiga chenga kulijibu swali hilo, Waziri mkuu alisema “mimi nina uhakika mheshimiwa Haji sidhani kama unanitendea haki maana katika hili.”
Chanzo: Mwananchi

No comments :

Post a Comment