zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, August 27, 2013

Umoja wa nchi za Ulaya `yaipiga jeki` Tanzania

NA ELIZABETH ZAYA

27th August 2013


Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa
Tanzania imepokea msaada wa Sh. bilioni 101  kwa ajili ya kuboresha miradi ya msingi katika mpango wa Millenia wa kukuza na kupunguza umaskini (Mkukuta), kutoka kwa Jumuiya ya Ulaya (EU).

Akizungumza wakati akipokea hundi  ya fedha hizo, Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa, alisema wamepokea fedha hizo ambazo ni kati ya bilioni 654.7 walizoahidiwa na Jumuiya hiyo mwaka 2009.
Alisema tangu kipindi hicho mpaka sasa, tayari serikali imepokea Sh. bilioni 507.7

Baadhi ya maeneo yaliyopewa kipaumbele katika msaada huo ni sekta ya elimu, afya hususani kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto, maji na sekta ya miundombinu.

“Tunahitaji kuwa na kasi ya kuondoa umaskini, na ndiyo maana tunaamua kuzungumza na wenzetu ambao tunashukuru wametusaidia,” alisema.

Kadhalika, alisema lengo la serikali ni kuweka mikakati ya kupunguza utegemezi wa misaada kutoka nje. Kadhalika alisema deni la serikali linalotokana na mikopo mbalimbali za nje ni Sh. trilioni 41.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment