NA BEATRICE SHAYO
31st August 2013
Hayo yalisemwa jana na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Eliachim Maswi, wakati wa kuwaaga wanafunzi nane wanaoenda kusomo katika vyuo tofauti nchini China kwa ufadhili wa nchi hiyo ambapo wawili ni watumishi wa serikali. “Hao ni tone tu la mahitaji yetu,” alisisitiza.
Maswi alisema kwa sasa wana upungufu wa wataalamu wa masuala hayo zaidi ya 200 na kwamba jambo hilo litasaidia kupunguza nafasi za wageni kupata ajira katika sekta hiyo baada ya Watanzania kupata elimu hiyo.
Alisema kampuni nyingi zinazowekeza katika sekta hiyo zimekuwa zikiajiri wataalamu kutoka nje, jambo ambalo serikali haifurahishwi hivyo wameanza kuchukua hatua kwa kutafuta wataalamu wa ndani kwa kuomba wafadhili na kutumia fedha za ndani kuwasomesha.
Alisema kwa kuwa wizara hiyo ni miongoni mwa wizara chini ya mpango wa matokeo makubwa, ili ifanikiwe wanahitajika wataalamu wazalendo waliobobea katika fani ya mafuta na gesi.
Hata hivyo, alisema bado kuna tatizo la taaluma mbalimbali kama uchumi na sheria ya masuala ya mafuta na gesi yanayohitaji wataalamu na tayari wizara imesishaanza kuchukua hatua za kuwatafuta.
Alisema kuwa wanafunzi wawili waliokwenda kusoma sheria ya mafuta na gesi wanamaliza mwezi ujao, huku wengine wawili wakijiandaa kwenda kusomea masuala hayo nchini China na huku wafanyakazi watano kutoka wizarani wakitarajia kwenda nchini Uingereza kupata mafunzo hayo.
Aliongeza kuwa mchakato wa kuwapata wanafunzi waliofadhiliwa na nchi ya China kusoma shahada ya uzamili, waliomba watu 56 na kupatikana 10 lakini wanaenda nane baada ya wawili kughairi kwenda kutokana na masuala mbalimbali.
Alisema wanafunzi hao wanatarajia kuondoka nchini Septemba 3, mwaka huu na serikali ikiwalipia usafiri na gharama nyingine kwa ajili ya siku chache za mwanzo.
Aliwataja wanafunzi hao kuwa ni Tekla Mponda, Yazidi Iddi, Paul Nsulangi, Grace Mkongwa, Maggi Mtaki, Cosmas Gamba, Angelica Lubango na Januarius Matata.
Akizungumzia wanafunzi watakaoenda kusoma nchini Brazil, alisema wanatakiwa kwenda wanafunzi 10 lakini wamechaguliwa 15 na majina yao kupelekwa ubalozi wa nchi hiyo nchini kuchambuliwa zaidi.
CHANZO: NIPASHE
Wazanzibari wamo katika hao?
ReplyDeleteyaguju kila mkiamshwa nyie mmlala fofofo,hao mnowaonana kuwa ndugu zenu ni pweza wanavutia kwao tu hao hata nchi za east afrika washashtuka
ReplyDelete