zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, August 27, 2013

WAZANZIBARI WAKUTANA KUMUOMBEA DUA MWENYEKITI WA MUWAZA

Written by   //  26/08/2013 

WAZANZIBARI WAKUTANA KUMUOMBEA DUA MWENYEKITI WA MUWAZA
MAREHEMU DR YUSSUF SALEH SALIM
Jumamosi, tarehe 19 Mai 2012, Jumuiya za Wazanzibari MUWAZA (Mustakbal wa Zanzibar) na ZAWA (Zanzibar Welfare Association) kwa pamoja zilifanya kisomo cha kumuombea Dua mwanaharakati mkakamavu, Mzanzibari asieyumba na aliyekuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya MUWAZA Dr. Yussuf Saleh Salim alietangulia mbele ya haki siku ya tarehe 21 April 2012 mjini Copenhagen, Denmark na kuzikwa huko huko siku ya Jumatatu tarehe 23 April 2012.
Kisomo cha kumuombea Dua Dr. Yussuf kiliwakutanisha pamoja Wazanzibari kutoka sehemu mbali mbali ndani na nje ya Uingereza katika ukumbi wa East African Education, uliopo 30 Station Road, Manor Park, East London, katika majira ya saa kumi za jioni. Wazanzibari waliohudhuria katika kisomo hicho walipata fursa pia ya kuelezana mambo ya kheri na kupeyana wasia kuhusu umuhimu wa umoja na mshikamano katika kusimamia haki zao na za nchi yao. Wazanzibari walikumbushana pia kwamba Umoja na mshikamano wa Wazanzibari ni miongoni mwa mambo muhimu ambayo marehemu, Dr. Yussuf Saleh Salim amekuwa akiyapigania kwa hali na mali katika uhai wake wote. Katika uhai wake Dr. Yussuf alijaribu kutafuta kila njia za kuwaunganisha Wazanzibari na kuungana nao pamoja kupitia jumuia mbali mbali zikiwemo Umoja wa Wazanzibari Skandinavia, Harakati za Mabadiliko ya Kidemokrasia (Hamaki) na Muwaza (Mustakbal wa Zanzibar).
Mungu amlaze pema marehemu, amfutie madhambi yake na ampe kauli thabit. Amin.
Chanzo: Mzalendo

No comments :

Post a Comment