zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, September 16, 2013

Hujuma hizi… Zanzibar ichukue hatua

NA MHARIRI

15th September 2013

Maoni ya Katuni
 
Vitendo vya kumwagiwa tindikali kwa baadhi ya viongozi wa madhehebu ya dini huko visiwani vimeshika kasi ya kutishia amani na usalama wa baadhi ya viongozi wa dini ambao ni muhimu sana kwa ustawi wa demokrasia ya kuabudu hapa nchini.
Mwishoni mwa wiki hii, Padri Anselm Mwang’amba alimwagiwa tindikali na watu wasiofahamika wakati akitoka katika ofisi inayotoa huduma za mtandao wa intaneti mjini Zanzibar.
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea kwenye mtaa wa Mlandege mjini Zanzibar, wakati Padre Mwang’amba akitokea katika ofisi hiyo ambapo ghafla alivamiwa na kumwagiwa tindikali, alipata msaada kwa wasamaria wema ambao walimpeleka katika hospitali ya rufaa ya Mnazi Mmoja kwa matibabu.
Kimsingi, tukio hilo ni mfululizo wa matukio kadhaa yaliyowahi kutokea visiwani humo kuanzia mwaka jana, tukio la kwanza lilikuwa kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Zanzibar Rashid Ali Juma.
Likafuatia tukio jingine la Novemba 6, 2012 ambapo Katibu wa Mufti wa Zanzibar, Fadhil Suleiman Soraga, alimwagiwa tindikali na mtu asiyejulikana wakati akifanya mazoezi eneo la Mwanakwerekwe saa 12 asubuhi.Ilipofika Desemba 26, 2012, Padri Ambrose Mkenda wa Kanisa la Katoliki Zanzibar alijeruhiwa vibaya kwa risasi na watu wasiofahamika, alipata majeraha katika maeneo ya shingo na mdomoni.
Mfululizo wa matukio uliendelea tena ambapo Februari 17, mwaka huu, Padri wa Kanisa Katoliki la Minara Miwili lililoko Mji Mkongwe Zanzibar, Evaristus Mushi alifariki dunia baada ya kupigwa risasi tatu kichwani na watu wasiofahamika. Padri Mushi alivamiwa na watu wawili waliokuwa kwenye pikipiki aina ya vespa. Alipigwa risasi hizo wakati anaingia katika kanisa la Betras.
Kama vile hayo hayatoshi, Agosti mwaka huu wasichana wawili, raia wa Uingereza waliokuwa walimu wa kujitolea, walimwagiwa tindikali na kujeruhiwa maeneo ya kifuani, shingoni na maeneo ya usoni.
Vitendo vya kuwamwagia tindikali viongozi wa madhehebu pamoja na hao raia wa Uingereza vinaonekana kufanywa kwa shinikizo la misingi ya ubaguzi.
Ubaguzi ambao umejidhihirisha kutokana na tofauti za kidini pamoja na tofauti za utaifa na rangi. Wasichana raia wa Uingereza waliomwagiwa tindikali walikuwa Zanzibar kufundisha somo la Kiingereza, ambalo kimsingi Wazanzibari wengi walihitaji msaada huo.
Vitendo vya kuhujumiana kwa njia ya kumwagiana tindikali vinaweza kusababisha chuki, uhasama pamoja na uadui mkubwa miongoni mwa wakazi wa Zanzibar, na wakati mwingine chuki hizo zinaweza kusambaa na kuvuka mipaka na hatimaye kutoweka kwa amani.
Nchi yetu imeweka sheria ya uhuru wa kuabudu, sheria hiyo haikuweka mipaka ya ukomo wa imani kwa waumini wa madhehebu yoyote, waumini wote wana haki sawa mbele ya sheia hii, mradi tu wasivunje sheria za nchi.
Utamaduni wa kumwagiana tindikali ambao unaonekana kutawala kwa baadhi ya wananchi wa Zanzibar, unaweza ukawa chanzo cha chokochoko za kuyumbisha amani iliyopo visiwani humo. Ni wajibu wa Serikali sasa kuchukua hatua madhubuti za kupambana na wachache wanaotaka kuharibu sifa za Wazanzibari wengine.
Tunaamini kuwa Serikali ya Zanzibar inafanya kila linalowezekana kudhibiti uhalifu wa aina hii.
Ni wakati muafaka sasa wa kuwasaka na kuwakamata wote waliohusika na matukio ya uhalifu wa kutumia silaha za moto na tindikali kuwahujumu wananchi wengine wasiokuwa na hatia, ili wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria.
Historia ya ubaguzi kwa misingi ya dini umewahi kujitokeza visiwani humo ambapo wakati mmoja kulikuwa na matukio mengi ya kuteketeza kwa moto makanisa na baadhi ya nyumba nyingine za ibada.
Kutokana na jitihada za serikali na vyombo vya ulinzi na usalama za kupambana na uhalifu, hali ya kuchoma nyumba za ibada sasa imetulia, tunaamini kuwa hali hiyo itadumu na kurejesha mahusiano mazuri kati ya waumuni wa madhehebu mbalimbali visiwani humo.
 
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

No comments :

Post a Comment