zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, September 22, 2013

Idara ya Ardhi Z’bar yawapa mafunzo waandishi wa habari

Afisa mtambuzi wa Ardhi Unguja Shawana Soud Khamis akitoa elimu ya utambuzi, kuisajili na kuitumia ardhi kwa wandishi habari katika ukumbi wa Wizara ya Habari Kikwajuni Mjini Unguja.
Afisa mtambuzi wa Ardhi Unguja Shawana Soud Khamis akitoa elimu ya utambuzi, kuisajili na kuitumia ardhi kwa wandishi habari katika ukumbi wa Wizara ya Habari Kikwajuni Mjini Unguja.
 
Afisa Mkaguzi wa Ardhi Zanzibar Shawana Suod Khamis amewataka wananchi kutoa
mashirikiano katika kufanikisha zoezi zima la Utambuzi na usajili wa ardhi nchini.
Kauli hiyo imetolewa jana katika ukumbi wa Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo wakati akifunga mafunzo ya siku moja ya utambuzi na usajili wa ardhi kwa waandishi wa habari .
Alisema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuweza kuwapa mbinu za kisasa na uwelewa mpana
kwa waandishi ili kuweza kuihamasisha jamii kuhusiana na zoezi hilo.
Alieleza kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kushirikiana na Serikali ya Finland kupitia
mradi wa SMOLE II unaendelea na zoezi la usajili wa Ardhi kupitia maeneo mbali mbali ya Zanzibar.
Mtalamu wa mambo ya Habari kutoka Smole Bw. Ali Rashid Salim akifahamisha kitu katika mafunzo kwa wandishi wa Habari juu usajili wa Ardhi, katika ukumbi wa Wizara ya Habari Kikwajuni Mjini Unguja jana

Shawana ameyataja baadhi ya maeneo ambayo tayari yameanza zoezi hilo na kuonyesha
mafanikio kuwa ni Kijiji cha Nugwi , Jendele, Paje, Chwaka, Kwaalinatu ,Mji Mkongwe, Mkokotoni ,Mwembetanga , Rahaleo, Muembeladu, Muembeshauri, Gulion, Kibondeni,
Kisima Majongoo, Mchangani na Vikokotoni .
Akieleza baadhi ya faida za usajili wa ardhi kuwa ni kupunguza migogoro inayotokea mara
kwa mara katika jamii na kumsaidia mmiliki wa ardhi katika kupata mikopo katika benki,
mashirika na taasisi mbali mbali.
Mkufunzi wa mafunzo hayo Afisa Habari na Mawasiliano wa SMOLE Ali Rashid Salim
amesema migogoro mingi ya Ardhi husababisha usheleweshaji wa mirathi kwa jimii hasa
kwa wanawake watoto yatima na watu wenye ulemavu na kupelekea kukosekana kwa
haki kwa wahusika.
Zoezi la usajili wa ardhi limeanza rasmi mwaka 2008 inatarajiwa kuwa ifikapo mwaka
2015 asilimia 50 ya ardhi yote ya Zanzibar iwe tayari imeshasajiliwa .
Baadhi ya wandishi Habari wa vyombo mbalimbali wakisikiliza kwa makini mafunzo yanayotolewa na Mtalamu wa mambo ya Habari kutoka Smole Bw. Ali Rashid Salim (hayupo pichani) katika ukumbi wa Wizara ya Habari kikwajuni Mjini Unguja jana.

Idara ya habari maelezo
 
Chanzo: ZanzibariYetu

No comments :

Post a Comment