zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, September 19, 2013

MHE JK ATEMBELEA NORTH AMERICA!

Rais Dkt. Jakaya Kikwete katika picha ya pamoja na mmoja wa viongozi wa TIGU Abdul Majid kutoka Los Angeles, California siku ya Jumatano Sept 18, 2013 kwenye Ubalozi wa Tanzania Washington, DC, nchini Marekani.
 
Rais Dkt. Jakaya Kikwete katika picha ya pamoja na Mpiganaji Sunday Shomari wa VOA bila kusahau sunday Shomari.com wa Washinton, DC siku ya Jumatano Sept 18, 2013 kwenye Ubalozi wa Tanzania Washington, DC, nchini Marekani.
 
Rais Dkt. Jakaya Kikwete katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV, Raymond Abraham siku ya Jumatano Sept 18, 2013 kwenye Ubalozi wa Tanzania Washington, DC, nchini Marekani.
 
Rais Dkt. Jakaya Kikwete katika picha ya pamoja na Mrisho Mzese wa Maryland siku ya Jumatano Sept 18, 2013 kwenye Ubalozi wa Tanzania Washington, DC, nchini Marekani.
 
Rais Dkt. Jakaya Kikwete katika picha ya pamoja na Mpiganaji wa Swahili Villa Blog, Abu Shatry siku ya Jumatano Sept 18, 2013 kwenye Ubalozi wa Tanzania Washington, DC, nchini Marekani.
 
Rais Dkt. Jakaya Kikwete katika picha ya pamoja na Dj Luke wa Vijimambo Blog siku ya Jumatano Sept 18, 2013 kwenye Ubalozi wa Tanzania Washington, DC, nchini Marekani.
 
Rais Dkt. Jakaya Kikwete katika picha ya pamoja na Dr Nirku Kyangu Mordi siku ya Jumatano Sept 18, 2013 kwenye Ubalozi wa Tanzania Washington, DC, nchini Marekani.
 
Rais Dkt. Jakaya Kikwete katika picha ya pamoja na Tumaini Kaisi siku ya Jumatano Sept 18, 2013 kwenye Ubalozi wa Tanzania Washington, DC, nchini Marekani.
 
Rais Dkt. Jakaya Kikwete katika picha ya pamoja na mpiganaji Mubelwa Bandio wa Changamoto yako Blog siku ya Jumatano Sept 18, 2013 kwenye Ubalozi wa Tanzania Washington, DC, nchini Marekani.
 
Rais Dkt. Jakaya Kikwete katika picha ya pamoja na Dr William na mkewe siku ya Jumatano Sept 18, 2013 kwenye Ubalozi wa Tanzania Washington, DC, nchini Marekani. 
 
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya Watanzania waishio katika mji wa Vallejo jimbo la California nchini Marekani leo wakati Rais alipotembelea mji huo wa kibiashara kwa mwaliko wa meya wa mji huo Mstahiki Osby Davis.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewataka Watanzania kuisemea, kuijenga na kuitetea nchi yao badala ya kushiriki katika kuikejeli na kuidharaulisha.

Rais Kikwete amesema kuwa kuisemea na kuitetea Tanzania ni wajibu wa kila Mtanzania awe anaishi ndani ya nchi ana ughaibuni.

Rais Kikwete amesema kuwa ni jambo la ajabu kuwa kazi ya kuisemea, kuitetea na kujenga jina zuri la Tanzania inafanywa zaidi na watu wa nje kuliko baadhi ya Watanzania na hasa wale wanaoishi nje ya nchi.

Rais Kikwete ameyasema hayo usiku wa jana, Jumatatu, Septemba 16, 2013, wakati alipokutana na kuzungumza na Watanzania waishio katika Jimbo la California kwenye siku ya kwanza ya ziara yake ya siku mbili katikia jimbo hilo na baadaye katika sehemu nyingine za Marekani.

Rais Kikwete amewaambia Jumuia ya Watanzania katika Hoteli ya Embassy, San Rafael, California: “Ni wajibu wa Watanzania popote walipo kuisemea vizuri na kutetea maslahi ya nchi yao. Ni jambo lisilo na tija kushiriki katika kuilaumu na kuikejeli nchi yetu. Utasikia na kusoma kwenye mablog baadhi ya watu wakisema kuwa ‘hii nchi gani?” amesema Rais Kikwete.

Rais ameongeza: “Siyo tu kwamba ni wajibu wa kila mmoja wetu kuisemea Tanzania lakini ni wajibu wetu kusaidia kusukuma maendeleo ya Tanzania. Hakuna mtu mwingine wa kuifanya kazi hii isipokuwa Watanzania. Hii ndiyo nchi yetu. Hakuna nchi nyingine hata kama tunailaumu kiasi gani.”

Amesisitiza: “Kama watu wa nje wako tayari kuisemea nchi yetu, nyie mnashindwaji vipi kuifanya kazi hiyo ya kuitetea nchi nzuri hii? Hivi nani tunamwachia aijenge nchi hii, aitetea nchi hii? Wengine wanathubutu kuuliza ‘Nchi nzuri? Turudi’. Hivi nani ulimwachia akujengee nchi nzuri ili uweze kurudi?”

Rais Kikwete amesema kuwa ni lazima Watanzania wajifunze kutoka kwa wenzao, wakiwemo majirani zao kuhusu namna ya kutetea maslahi ya nchi yao kwa kila jitihada.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

17 Septemba, 2013
 

RAIS JAKAYA KIKWETE ATEMBELEA UBALOZI WA

TANZANIA,

WASHINGTON, DC


Rais Dkt Jakaya Kikwete akitembea kwa miguu kutoka hotelini kwake kuja kwenye Ubalozi wa Tanzania Marekani siku ya Jumatano Sept 18, 2013 na kukutana na Mabaozi wa Heshima ambao jana Jumatano wasaini mikataba ya kuwa rasmi Mabalozi wa heshima wataofanyakazi wakiiitangaza Tanzania nchini Marekani kwa ajili ya uwekezaji, Utalii na mambo mengine yatakayosaidia kuinua uchumi wa Tanzania.

Rais Dkat Jakaya Kikwete akisalimiana na Maafisa Ubalozi wakiwemo wafanyakazi mara tu alipoingia Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani uliopo barabra ya 22, Washington, DC.
 
Rais Dkt Jakaya Kikwete akitia saidi kitabu cha wageni Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.
 
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akisaini kitabu cha wageni huku Mhe. Waziri Bernard Membe na Mhe. Balozi Liberata Mulamula wakishuhudia.

Raus Dkt. Jakaya Kikwete akisalimiana na Mama William alipokua akiingia chumba cha mikutano cha Nyerere
 
Rais Dkt Jakaya Kikwete akisalimiana na mmoja wa Mabalozi wa Heshima
 
Rais Dkt Jakaya Kikwete akisalimiana na Balozi wa Heshima Hon. Kjell Bergh kutoka Minnesota
 
Rais Dkt Jakaya Kikwete akisalimiana na Balozi wa Heshima Hon Ahmed Issa kutoka California
 
Rais Dkt Jakaya Kikwete akisalimiana na Balozi wa Heshima Hon. Robert Samuel Shumake kutoka Michigan.
 
Rais Dkt Jakaya Kikwete akiongea machache kuwashukuru Mabalozi wa Heshima kwa kukubali kwao kuitangaza Tanzania nchini Marekani na kusema sio kazi rahisi lakini ana Imani nao na aliwatakia kila la kheri ya kuwa na nia thabiti ya kuitangaza Tanzania nchini Marekani.
 
Rais Dkt Jakaya Kikwete akipokea zawadi ya saa kutoka kwa Balozi wa Heshima Hon. Robert Samuel Shumake kutoka Michigan. Picha zingine baadae.
 

JK ATEMBELEA CAPITOL HILL


Rais Dkt Jakaya Kikwete akiongozana na Mhe. BernardWaziri Membe na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Liberata Mulamula tayari kuelekea Capitol Hill kuendelea na ziara yake nchini Marekani. Rais Kikwete aliwasili Washington, DC leo Jumatano Sept 18, 2013 asubuhi akitokea California
 
Rais Dkt Jakaya Kikwete akiongea na Halima Mamuya na H.V. Street wamiliki wa AmeriTan International ya Louisiana
 
Juu na chini ni Rais Dkt Jakaya Kikwete akijiandaa kuingia kwenye gari kuelekea Capitol Hill kuendelea na ziara yake nchini Marekani
 
 
Gari lililomchukua Rais Dkt. Jakaya Kikwete likiondoka kuelekea Capitol Hill.
                                                                                   
 
CHANZO: VIJIMAMBO
N.B.
Pita tena hapa ZNK baadae kwa pich zaidi!

No comments :

Post a Comment