NA MWANDISHI WETU
30th September 2013
Katika salamu zake hizo, Rais Dk. Shein, amesema wananchi wa Zanzibar wanaungana na ndugu zao wa China katika kusherehekea miaka 64 ya uhuru wa nchi hiyo pamoja na urafiki na mshikamano uliodumu kwa muda mrefu baina ya mataifa hayo mawili.
Aidha, ameipongeza Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kwa mafanikio makubwa iliyoyapata katika sekta zote za maendeleo chini ya uongozi imara wa Chama cha Kikomunisti cha nchi hiyo.
Alielezea matumaini yake kuwa ushirikiano baina ya Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China na wananchi wa Zanzibar utaendelea kuimarika zaidi.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment