zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, October 21, 2013

JKU wamlipa mamilioni ya fedha Naushad Zanzibar

NI baada ya wezi kuvamia nyumbani kwake na kuiba wakati nyumba ikiwa chini ya ulinzi wa askari wa kikosi hicho.
Zanzibar. Jeshi la Kujenga Uchumi Zanzibar (JKU) limelazimika kumlipa fidia ya Sh50 milioni Mfanyabiashara Maarufu Zanzibar, Naushad Mohammeid Suleiman, kinyume na sheria baada ya kuibiwa nyumbani kwake chini ya ulinzi wa askari wa kikosi hicho visiwani humo.
Kwa mujibu wa ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali Zanzibar (CAG) ya mwaka 2011/12 malipo hayo yamefanyika kinyume na sheria ya fedha namba 12 ya mwaka 2005.
CAG Fatma Mohamed Said alisema kwamba JKU wamelazimika kulipa fidia ya kiwango hicho cha fedha baada ya Naushaud kulalamika kuibiwa ndaniya nyumba yake katika Mtaa wa Betras Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Juni 13, mwaka 2010.
“Njia zilizotumika kumlipa mhusika zimekiuka sheria ya fedha namba 12 ya mwaka 2005,” alisema CAG Fatma katika ripoti hiyo.
Alisema uongozi wa JKU umeshindwa kuonyesha nyaraka muhimu zilizotakiwa kuzingatiwa kabla ya kufanyika malipo ya fidia ikiwemo taarifa ya tukio la wizi, taarifa ya Jeshi la Polisi au Mahakama na madai ya maandishi ya mlipwaji.
Nyaraka nyingine ni vielelezo vya tathimini ya hasara na upotevu wa mali, taarifa ya vikao vya uongozi vilivyojadili hasara na upotevu wa mali na fedha, pamoja na taarifa za hatua zilizochukuliwa
dhidi ya askari waliohusika baada ya kutokea kwa wizi huo.
Akizungumza na gazeti hili jana, Naushad alisema wizi huo ulifanyika wakati familia yake ikiwa haipo na yeye akiwa safari India
Alisema wakati wizi unafanyika katika nyumba yake ya Betras, familia yake walikuwa wamekwenda kupumzika katika nyumba yake aliyojenga katika ufukwe wa bahari ya Paje Mkoa wa Kusini Unguja na askari wa JKU wapatao watatu waliokuwa zamu ndiyo walikuwa na dhamana ya usalama wa nyumba siku hiyo. Hata hivyo, Mkuu wa Jeshi la Kujenga Uchumi Zanzibar (JKU) Kamanda Soud alipoulizwa na gazeti hili jana kuhusu Taarifa ya CAG alisema hawezi kuzungumza mambo ya ofisi kwa njia ya simu licha ya kukiri kutokea kwa mkasa.
Naye aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa mjini Magharibi, Azizi Juma Mohamed alisema kwa mujibu wa taratibu na sheria ya Jeshi la Polisi hawezi kuzungumzia mkasa huo.


No comments :

Post a Comment