zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, October 24, 2013

Serikali yahimiza Watanzania ushindani vitalu vya gesi, mafuta

NA MWANDISHI WETU

24th October 2013


Waziri wa Nishati na Madini,Prof. Sospeter Muhongo
Serikali imewahimiza Watanzania kuchangamkia rasilimali zinazopatikana nchini ikiwa ni pamoja na kujitokeza kwa wingi katika ushindani wa kupata vitalu vya gesi asilia na mafuta kwa ajili ya uwekezaji.

Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo, wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye kongamano na  maonesho ya pili ya mafuta na gesi, yaliyoshirikisha takribani washiriki 600 kutoka nchi mbalimbali duniani.

Kesho Rais Kikwete atakuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa ugawaji wa vitalu vya rasilimali hizo.

“Hakuna Mtanzania aliyezuiliwa kwenda kushindania kupata vitalu vya gesi na mafuta ambavyo vipo nchini, kwani Watanzania nao wanaweza kuingia kwenye shughuli za uatafutaji na uchimbaji wa mafuta. Lakini haiwezekani mtu binafsi akadai apewe vitalu kibinafsi,” alisema Profesa Muhongo na kuongeza:

“Kuna tofauti kati ya wazawa na mtu binafsi. Mwaka 1969 Mwalimu Julius Nyerere, alianzisha Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) kwa ajili ya manufaa ya Watanzania wote kwa matumaini ya kwamba kupitia uwakilishi wa kisekta.”

Alisema mkutano wa gesi na mafuta ni wa muhimu sana kwani unazungumzia upatikanaji wa rasilimali za mafuta na gesi kwa Afrika Mashariki, na dunia kwa ujumla.

Alisema kusudi kubwa la mkutano huo kufanyika nchini, ni kwa ajili ya kuwavutia wageni hao juu ya uwekezaji kwenye rasilimali hizo kubwa nchini na kwamba Watanzania wenyewe wanapaswa kujiamini kwani nchi nyingine zina matumaini makubwa ya kuwekeza kwenye rasilimali hizo kwa sababu wana imani juu ya sheria na taratibu za uwekezaji.

Naye Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib  Bilal, akifungua mkutano huo, alisema, tukio hilo linatoa msukumo wa pekee kwa ukuaji wa sekta ya mafuta na gesi, na kwamba ni kichocheo kikuu cha ukuaji wa viwanda ili kuleta hali bora kwa wananchi.

“Gesi asilia iliyogunduliwa hadi Agosti mwaka huu imefikia futi za ujazo trilioni 43, jambo linalotoa changamoto ya kuongeza juhudi za kuhamasisha Watanzania wengi kushiriki katika sekta hii na pia kuwapa uelewa wa kutosha wa namna ya kunufaika na rasilimali hizi,” alisema Dk. Bilal na kuongeza:

“Wakati tukisherehekea ugunduzi wa hazina kubwa ya gesi nchini, tunapaswa kuzingatia suala la utunzaji wa mazingira, afya na usalama wa wananchi, kwani kumekuwapo na matukio ya kulipuka kwa gesi na umwagikaji holela wa mafuta na kuleta athari kwa viumbe hai ikiwa ni pamoja na vifo.”
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment