NA MWANDISHI WETU
23rd October 2013
Hayo yalibainishwa ilipokutana na uongozi wa TTCL na bodi yake jana kwa ajili ya kufuatilia utekelezaji na utendaji wa kampuni hiyo ya serikali.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Peter Serukamba, alisema TTCL inadai Sh. bilioni 10 kutoka kwa wadaiwa sugu ambao ni wizara na idara za serikali na kwamba ili kujinusuru, serikali inatakiwa kuiondolea ubia Airtel kutoka shirika lake (TTCL).
“Tunaitaka serikali kununua hisa zote za Airtel zilizopo TTCL kwa kuwa serikali haiwezi kuyalipa madeni hayo inayodaiwa isipokuwa kwa kuiondolea ubia Airtel, na pia kwa ajili ya kuleta ushindani kati yao,” alisema Serukamba.
Serikali ina hisa asilimia 65 kwenye kampuni ya TTCL na Aitel asilimia 35.
Baadhi ya wizara na idara za serikali ambazo zinadaiwa kuwa ndiyo wadaiwa sugu wa kampuni ni pamoja na, kwenye mabano kiasi cha deni, Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Jeshi la Polisi na Wizara ya Fedha
Nyingine ni Ofisi ya Rais (RSO), Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Wizara ya Elimu, Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Udom, Wizara ya Ulinzi na ile ya Sheria.
Kamati hiyo ilibainisha ofisi nyingine za serikali kuwa ni pamoja na Wizara ya Katiba na Sheria, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknlojia, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, TBC, Usalama Pemba, KMKM na Costech.
Sambamba na hilo, kamati iliiagiza TTCL kufuatilia madeni hayo ndani ya miezi mitatu kuanzia mwezi huu hadi Desemba na iwapo kuna ofisi yoyote itakuwa bado kulipa ikatiwe huduma.
“Jamani kwa ukweli TTCL ni shirika letu, naombeni tulipe priority (kipaumbele), hamlipi madeni na mnataka tunyamaze. Siku 72 umepatiwa huduma halafu hutaki kulipa, haiwezekani tukawaogopa eti kwasababu watahama huduma,” alisema Serukamba.
Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Kamugisha Kazaura, alisema hali ya kampuni hiyo hadi Agosti mwaka huu haikuwa ya kuridhisha lakini kwa kushirikiana na wizara husika wanaendelea na mikakati mbalimbali ikiwamo ya kuboresha mawasiliano ya simu za mikononi.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment