zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, October 21, 2013

Zanzibar au Tanzania na Jumuiya ya Afrika Masharik (EAC)

Written by   //  21/10/2013 

Nadhani wenzangu nyote mnafuatilia mwenendo wa Tanzania na mahusiano yake na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kuwa kwa kitambo sasa Tanzania inaenguliwa katika vikao muhimu sana vya maamuzi ya EAC. Nchi kama Uganda, Rwanda na Kenya ndio zinashika usukani wa kuiengua TZ katika mazungumzo — wenyewe maarufu wanajiita ‘coalition of the willing’. Burundi imekaa kando kidogo, ingawa imo humo humo. Tanzania ndio ‘out’ kabisa.
* Wakati kikao hichi muhimu kinapofanyika, Tanzania na Rais wao walikwenda Iringa kuanzimisha mbio za Mwenge wa uhuru, sasa upumbavu kama huo unaingizwa kwenye mambo muhimu ya nchi na ‘national interests’ hizo anazosema Kikwete.
Iwe mbio za mwenge ni muhimu kuliko EAC na masuala yake yote ya nchi??
Juzi kimefanyika kikao chengine muhimu zaidi kinachojadili ‘political federation’ ya EAC. Hii haikuwa tena ‘Federation of the willing’ imeitwa ‘coalition of federation’ maana na Burundi pia ameingia tele na kupewa maamuzi na kufanya action plan towards, EAC political federation. TZ imetolewa kabisa hapo.
Tanzania imejitoa na kutolewa kutokana na ubabe wake; zaidi ni switilfahamu baina ya Kikwete na Kagame, hapo imetufanya sote tufuate ‘bwana anavyotaka’ (national interests hizo!).
Lakini sasa swali la kujiuliza, je kama Zanzibar tuna ‘zanzibar interest’ ndani ya Jumuiya hii, lakini ‘mabwana hawataki’ ndio na sisi tukose moja kwa moja. Kwa mfano, sisi Zanzibar kama kisiwa tuna ‘interest’ za kibiashara tokea asili sisi na nchi hizo, kuanzia mifumo ya kodi, ufanyaji biashara n.k — sisi Zanzibar kwa ninavyojua mimi ndio hasa waasisi na vinara wakuu wa EAC, na tulikuwa mbele katika east african common currency/board.
Leo just kwa sababu Bernard Member hataki, na Kikwete hawataki kutokana na ugomvi wao binafsi na Kagame — basi wameona bora litote na tugawane mbao, na Zanzibar ni nani (they are just nothing). Huu ndio msimamo wa Tanzania, na huu ndio faida za Muungano huu tulionao; kuwa kama jambo hawatitaki Tanganyika, basi sooote iwe hatfaidiki nalo hata kwetu Zanzibar ni faida na lina tija kwetu.
Kwa ufupi, naomba mfuatilie vikao hivi vya EAC na maamuzi yake.
Pia naliomba Baraza la Wawakilishi (BLW) linalokaa sasa hivi, wafikiri ‘strategic’ walizungumze hili na kama serikali, SMZ walitolee maamuzi, na wananchi tujue: Nini msimamo, mustakabali wa Zanzibar ndani ya jumuiya hii ya EAC.
Jamani hili ni suala muhimu sana. Mtu kama Uhuru Kenyatta, au Odinga wanajua sisi kuwa ndio EAC na wanapenda kuwa na sisi kw ahilo, lakini tumezidiwa, tumefunikwa na Tanganyika — na ukweli hasa wanatutetea wao yanapozungumzwa mambo muhimu yanayohusu Zanzibar, kama bahari kuu wakati — Tanganyika inatuamisha au wanataka kula ‘keki’ yote. Mifano ipo, mkiitaka sana nitawisilisha (pengine si lazima). Ina maana sisi tunatolewa tonge mdomoni hivi hivi??
Kimsingi wao Tanzania walipofanyiwa survey, imeonekana kuwa 85%ya Watanzania hawako tayari kujiunga na EAC; lakini ni wao Watanganyika, sio sisi Wazanzibari -sisi hata hiyo survey haikufanyika
Hili linaniuma sana maana kwa nia moja au nyengine nimehusika katika ushiriki wa kuifufua EAC miaka ya 1998; na tukaweka msimamo wetu wa SMZ humo.Leo Bernard Membe anatuletea mambo ya ‘yasiyokuwa na maana’ — mambo ya kipuuzi; misaada ya Oman anaizuia, misaada ya climate change anaizuia, misaada mengine na mengine anaizuia, wao ndio nani, ufalme huu mpaka lini? CCM Zanzibar wamekaa tu, wanatokwa na madenda — hawawezi kufikiri hata chembe, hao CUF nao kadhalika– wanapiga kelele kelele tu; not strategic. Hawazungumzii ‘national issues, au issues of interests’ wanasukuma sukuma tu mawazo kama kuendesha rikwama.
– Wazanzibari tuamke jamani — hivi tutakaa hivi mpaka lini — hatuwezi kudai hata chembe ya haki zetu za msingi?
Chanzo: Mzalendo

No comments :

Post a Comment