zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, October 26, 2013

Zitto aendelea kunyooshewa vidole

NA DUNSTAN BAHAI

26th October 2013


Zitto Kabwe
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe, ameendelea kuponzwa na kauli yake ya kusitisha ruzuku kwa vyama vya siasa baada ya vyama hivyo kudai anachokifanya ni fujo na vurugu.
Imeelezwa kuwa kazi ya kukituhumu chama kimoja kimoja ni vurugu kwani yeye (Zitto) alitakiwa kumhoji Msajili wa Vyama vya Siasa na si chama kimoja kama anavyotaka.
Akizungumza na gazeti hili, Msemaji wa vyama vya upinzani vyenye wabunge Bungeni, James Mbatia, alisema utaratibu uliopo ni kamati ya Zitto kumhoji Msajili wa Vyama vya Siasa.
Alisema si jukumu la PAC kuvishutumu vyama hivyo bali vyama hivyo bosi wao ni msajili ambaye angeandaa utaratibu wa kuvialika na kuzungumza navyo.
Utaratibu huo ulifanywa wiki hii na msajili huyo Jaji Francis Mutungi, na kusema kuwa hawezi kusitisha malipo ya ruzuku kwa vyama vya siasa hadi hapo ofisi yake itakapojiridhisha aliyesababisha hesabu za vyama hivyo kutokaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Wiki iliyopita, PAC chini ya Mwenyekiti wake, Zitto ilisema licha ya kuwa vyama hivyo tisa kupokea ruzuku ya jumla ya sh. bilioni 67.7 tangu mwaka 2009, lakini havijawahi kupeleka ripoti yoyote ya ukaguzi wa fedha kwa CAG.
Zitto alitangaza kusitishwa mara moja utoaji wa ruzuku kwa vyama vyote vya siasa nchini mpaka hapo hesabu zake zitakapokaguliwa na CAG.
Vyama vilivyopokea jumla ya ruzuku ya sh. bilioni 67.7 na mchanganuo wake kwenye mabano tangu mwaka wa fedha wa 2009/10 ni CCM (sh. bilioni 50.97), Chadema (sh.bilioni 9.2), CUF (sh. bilioni 6.29) na NCCR (sh. bilioni 0.677).
Vingine ni UDP (sh. bilioni 0.33), TLP (sh. bilioni 0.217), APPT (sh. milioni11), DP (sh. milioni 3.3 na Chausta sh milioni (2.4).
Kwa mujibu wa Mbatia, ruzuku ya vyama vya siasa hupitishwa na bunge na si kamati na msimamizi mkuu wake ni msajili, hivyo kamati husika inatakiwa kufuatilia kwa msimamizi.
“Anachokifanya huyo mwenyekiti wa PAC ni kelele na fujo tu, kwani upo utaratibu wa kufuatilia suala hili,” alisema Mbatia.
Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi Samwel Ruhuza, naye alimponda Zitto huku akipongeza kauli ya msajili wa vyama vya siasa.
Alisema madai ya Zitto hayana msingi kwani ajiulize zamani utaratibu ulikuwaje na sasa kwanini yametokea hayo.
“Hili suala msajili amelitolea maelezo mazuri sana hata katika barua aliyotuandikia amesema marumbano yanayoendelea kati ya Mwenyekiti wa PAC na vyama vya siasa si mazuri,” alisema Ruhuza.
Kwa mujibu wa Ruhuza, sheria inamtaka CAG aende kufanya ukaguzi huo, lakini mwenyewe alishasema hana fedha za ukaguzi.
Hata hivyo alipinga kauli kwamba CAG ndiye atafute kampuni binafsi za kwenda kufanya ukaguzi, kwani kwa kufanya hivyo, vyama vinajikuta vinatoa fedha nyingi kuliko uwezo waliokuwa nao.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment