Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, November 19, 2013

Dk Shein:Bei ya karafuu kuendelea kuimarishwa

Na Mwandishi wetu

Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein

Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein, amesema nia ya serikali ni kuimarisha bei ya karafuu kwa mkulima kila inapowezakana ili kuhakikisha anafaidika na jasho lake.

Dk. Shein aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na wananchi wa vijiji vya Chanjaani, Mzambarauni na Kinyasini Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba kwa nyakati tofauti baada ya kukagua vituo vya kuuzia karafuu katika vijiji hivyo.

Aliwaeleza wananchi hao kuwa wana wajibu wa kupiga vita biashara ya magendo ya karafuu kwa sababu mbali ya kuinyima serikali mapato, lakini wakulima wanajidhulumu nafsi zao wenyewe.

Alifafanua kuwa serikali inatoa bei nzuri kwa wakulima kwa kuwapata asilimia 80 ya bei ya soko la dunia huku yenyewe ikichukua asilimia 20 tu ambazo nazo hutumika katika kuimarisha huduma mbalimbali zikiwamo za kijamii na za kiuchumi.

Aliwahakikishia wananchi kuwa Tangazo la Serikali la kutopunguza bei ya zao la karafuu, liko pale pale na kubainisha kuwa serikali ingefurahi kuona bei ya karafuu kwa wakulima inaongezeka kila inapowezekana.

“Nia yetu si kupunguza bei bali ni kuwaongezea bei wakulima na tungependa kuona bei ya karafuu katika soko la dunia inaongezeka au inabaki katika hali ya sasa ili wakulima waendelee kufaidi bei nzuri,” alisema.

Akijibu baadhi ya hoja za wakulima likiwamo la ulinzi wa mashamba ya mikarafuu kufuatia wizi ulioibuka, Rais Shei alieleza kuwa tatizo hilo ni kubwa hasa vitendo vya baadhi ya watu hukata mikarafuu.

“Serikali inalifahamu suala hili na kwa kweli linatusikitisha kwani ni uharibifu mkubwa na unarejesha nyuma jitihada zetu za kuongeza uzalishaji wa zao hili. Wito wangu kwenu wananchi sote tushirikiane katika ulinzi shirikishi kukabiliana na vitendo hivyo,” alisema.

Awali, mmoja wa wakulima wa zao hilo katika kijiji cha Mzambarauni, alimueleza Rais kuwa kumeibuka wizi wa karafuu kisiwani humo na baadhi ya wezi hukata matawi ya mikarafuu na kuchuma karafuu zilizopea na kuziacha karafuu changa.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment