NA WAANDISHI WETU
15th November 2013
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi , alisema hayo alipozungumza na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam, katika maadhimisho ya Siku ya Kisukari Duniani.
“Utafiti unaonyesha mikoa ya Kaskazini mwa Tanzania ni waathirika wakubwa wa ugonjwa huu kwa sababu ya vyakula wanavyokula na pombe wanazokunywa,” alisema Dk. Mwinyi.
Alisema watu wengi wanapata ugonjwa huo kwa sababu ya kutofuata kanuni bora za afya pamoja na kutokuwa na ulaji unaofaa.
Aliwataka vijana kuachana na tabia na mwenendo mbaya walionao hivi sasa ili kupunguza ugonjwa huo.
Alisema katika nchi 10 zinazoongoza kwa ugonjwa huo Barani Afrika, Tanzania inashika nafasi ya nane.
Hata hivyo, alisema ili kuzuia ugonjwa huo na maradhi mengine yasiyo ya kuambukiza, ni muhimu kufuata kanuni za afya.
Kanuni hizo ni ulaji na mtindo bora wa maisha, ambao utasaidia kuzuia watu kupata kisukari na kupunguza uwezekano wa kupata madhara makubwa ya kiafya
Wakati huo huo, Serikali ya Zanzibar imesema kila mwaka inapokea wagonjwa wapya 332 wa kisukari (asilimia 50).
Imesema hali hiyo inaonyesha ugonjwa huo ni tishio, hivyo akawataka wananchi kuchukuwa tahadhari.
Naibu Waziri wa Afya, Dk. Sira Ubwa Mamboya, alisema watu 4,000 wapo hatarini kupata ugonjwa huo kutokana na sababu mbalimbali.
Aliishauri jamii kubadilisha mfumo wa maisha kwa kufanya uchunguzi wa afya mara kwa mara, kufanya mazoezi ya viungo na kupendelea kula vyakula vya mbogamboga na matunda.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment