Hapo jana tarehe 16 novemba, 2013 Mtaalamu na mhadhiri wa sheria kutoka chuo kikuu cha Zanzibar (Zanzibar University) alipata fursa ya kuwasilisha mada aliyoifanyia utafiti kuhusu mafanikio na matatizo ya mahkama za Zanzibar katika kipindi cha miaka 50 iliyopita.
Mara baada ya kuwasilishwa kwa mada hiyo mjadala mkali ulifumuka kutoka kwa wachangiaji mbali mbali.
Mjadala huo ulihudhuriwa na watu mbalimbali akiwemo Jaji Mkuu wa Zanzibar, mheshimiwa Omar Othman Makungu ambaye alikuwa mwenyekiti wa mjadala huo, na Mrajis wa mahkama Zanzibar mheshimwa George Kazi; ambao kwa pamoja wamekubali ombi la mtoa mada kusaidiwa kuchapisha kitabu kuhusu kuhusu mada hiyo na pia aendelee kufanya utafiti zaidi.
No comments :
Post a Comment