Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, November 18, 2013

Makamo wa Rais wa ZFA Unguja AlHajjj Haji Ameir Aifanyia tafrija Timu ya Taifa ya Zanzibar.

 Makamo wa Mwenyekiti wa Chama cha Mpira Zanzibar AlHajj Haji Ameir 
(Boss Mpakia) akizungumza na Waandishi wa habari na Wachezaji wa 
Timu ya Taifa ya Zanzibar baada ya kumaliza kupata chakula cha mchana 
alichowaandalia wachezaji hao nyumbani kwake, kuiaga timu hiyo na 
kuitakia safari njema na ushindi katika michuano ya Kombe la Chalenji 
yanayotarajiwa kufanyika Nchini Kenya mwishoni mwa mwezi huu. 

 Katibu wa Chama cha Waamuzi Zanzibar Issa Ahmada Jongoo, akizungumza 
na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa tafrija hiyo na kuwataka 
wachezaji wa Zanzibar kuwa kitu kimoja na kutojali nani hayupo katika 
timu hiyo. Wawe na ari ya kujituma katika mchezo wao. 

 Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya timu ya Taifa ya Zanzibar Juma Sunday 
akizungumza katika tafrija hiyo jinsi timu ilivyojianda na michuano hiyo na 
kuahidi kurudi na ushindi Zanzibar.

 Nahodha wa timu ya Taifa ya Zanzibar akizungumza wakati wa tafrija 
hiyo walioandaliwa na Makamo wa Mwenyekiti wa ZFA Unguja 
Al Hajj Haji Ameir, nyumbani kwake,akitowa shukrani na kuahidi 
kuiletea ushindin Zanzibar katika michuano hiyo inayotarajiwa kufanyika 
nchinin Kenya mwishoni mwa mwezi huu.



                                     Mambo ya Biriani hayo mdau naona unajiramba hapo
(HUYU JAMAA WA KULIA ANAMATONGE MAKUBWA, 
HATUJUI KAMA WENZIWE WALIAMBULIA KITU! - ZNK)
Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar wakikata mpunga katika mnuso 
walioandaliwa na Makamo wa Rais wa ZFA Zanzibar Al hajj Haji Ameir 
nyumbani kwake na kuzungumza nao wakiwa katika maandalizi ya 
Kombe la Chaleji yanayotarajiwa kufanyika Nchini Kenya mwishoni mwa mwzi huu.  

Chanzo: ZanziNews

No comments :

Post a Comment