zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, November 15, 2013

Rais Kikwete awasili Sri Lanka

NA MWANDISHI WETU

15th November 2013


Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Sri Lanka Mhe.Mahinda Rajapaksa alipomtembelea kwa mazungumzo kwenye jengo la Temple Trees Jijini Colombo jana kabla ya ufunguzi rasmi wa mkutano wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Madola mwaka huu.
Rais Jakaya Kikwete, amewasili mjini Colombo, Sri Lanka, tayari kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Serikali za Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola (CHOGM) utaofanyika kwa siku tatu.

Akiwa amefuatana na mkewe, Mama Salma, Rais Kikwete aliwasili mjini Colombo, Sri Lanka, jana akitokea Dubai ambako alipitia juzi apoondoka Dar es Salaam.

Tofauti na mikutano ya CHOGM kwa kipindi cha miaka 40 ambayo hufunguliwa na Malkia wa Uingereza, Elizabeth, safari hii utafunguliwa rasmi na mwanaye,  Prince Charles. Malkia Elizabeth ndiye kiongozi wa Jumuiya ya Madola.

Mara baada sherehe za ufunguzi, Rais Kikwete ataungana na viongozi wenzake kwa ajili ya vikao rasmi vya mkutano huo vitakavyofanyika kwenye Kituo cha Maonyesho ya Kumbukumbu cha Sirimavo Bandaranaike.

Miongoni mwa shughuli kubwa za vikao leo ni mkutano wa viongozi wa Jumuiya hiyo na majadiliano kati ya viongozi hao na viongozi wa vijana kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola.

Aidha, viongozi hao wa Jumuiya ya Madola akiwamo Rais Kikwete watahudhuria hafla rasmi ya makaribisho itakayoandaliwa na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Kamalesh Sharma, katika Ukumbi wa Bandaranaike Memorial International Conference Hall (BMICH).

Jana Rais Kikwete na Mama Salma, walihudhuria Hafla ya Chakula cha Usiku kilikachoandaliwa na Prince Charles na mkewe, The Duchess of Corwall, kwenye Hoteli ya Cinnamon Lakeside.

Jumuiya ya Madola ni umoja wa nchi zilizokuwa chini ya ukoloni na himaya ya Uingereza na nchi nyingine ambazo zenyewe ziliomba na kukubaliwa kujiunga na Jumuiya hiyo ikiwamo Mozambique na Rwanda. Jumuiya hiyo ina nchi wanachama 53, zikiwamo 18 za Afrika ambalo ni Bara lenye wanachama wengi zaidi katika Jumuiya hiyo, nchi nane za Asia, nchi 13 za Marekani na Caribbean, nchi tatu za Ulaya na nchi 11 za Pacific.

Jumuiya hiyo pia ina mchanganyiko wa nchi kubwa na ndogo, nchi 32 kati ya hizo zilihesabiwa kama nchi ndogo kwa maana ya kuwa idadi ya watu milioni 1.5 ama chini ya hapo.

Sri Lanka ambayo mpaka mwaka 1972 ilijulikana kwa jina la Ceylon, inajulikama rasmi kama Jamhuri ya Kidemosia ya Kisoshalisti ya Sri Lanka. Ni nchi kisiwa kilichoko kaskazini mwa Bahari ya India na Kusini mwa pwani ya nchi ya India. Ni nchi yenye mipaka ya maji na India na Maldives.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment