NA MWANDISHI WETU
27th November 2013.
Tanzania imezibwaga Kenya, Uganda na Rwanda katika medani ya mahusiano ya kimataifa baada ya kupewa fursa ya kujenga jengo la mahakama itakayoendeleza kesi ya mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR).
Jengo hilo jipya la mahakama linatarajiwa kujengwa jijini Arusha baada ya Tanzania kupewa nafasi hiyo kwa kuzishinda nchi nyingine za Afrika Mashariki zilizoomba Umoja wa Mataifa (UN) ili lijengwe katika nchi hizo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, alisema kuwa kati ya nchi tatu zilizoomba mahakama hiyo kujengwa kwake, ni Tanzania pekee iliyopitishwa.Jengo hilo jipya la mahakama linatarajiwa kujengwa jijini Arusha baada ya Tanzania kupewa nafasi hiyo kwa kuzishinda nchi nyingine za Afrika Mashariki zilizoomba Umoja wa Mataifa (UN) ili lijengwe katika nchi hizo.
Katika utekelezaji wa mchakato huo, jana Membe alibadilishana hati na Miguel de Serpa Soares, Kiongozi wa ujumbe kutoka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya sheria, baada ya kutiliana saini mkataba wa ujenzi wa jengo hilo.
Kwa mujibu wa Membe, nchi zilizopeleka maombi hayo katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ni Kenya na Rwanda, lakini Tanzania ikazipiku nchi hizo kutokana na kuwa na historia nzuri ya ushirikiano kati yake na baraza hilo na UN, huku Katibu Mkuu wa UN, Ban Kin Moon, akiridhia hilo.
Sambamba na hilo, Membe alisema gharama zitakazotumika kujenga jengo la mahakama hiyo ni Sh. bilioni 8, ambazo zitatolewa na UN kupitia baraza hilo la usalama.
Kwa mujibu wa Membe kumbukumbu na nyaraka zote kuhusu kesi za ICTR zitahamishiwa kwenye jengo hilo na kwamba masuala mengine ya kesi yaliyokuwa yamebaki yataendelea kushughulikiwa kwenye mahakama hiyo.
Hata hivyo, Membe hakueleza ni lini hasa mahakama hiyo itaanza kujengwa kwa maelezo kuwa UN kupitia baraza hilo ndiyo wenye majibu sahihi.
Mbali na kutunzaji wa nyaraka na vielelezo vilivyokuwa kwenye mahakama ya kwanza, alitaja kazi nyingine kuwa ni kuendeleza masuala yote ya kesi yaliyokuwa yakifanywa na mahakama ya awali.
Pia itahusika na utunzaji wa mafaili yote ya kiutawala, kuwalinda wale wote waliohusika kutoa ushahidi kuhusiana na kesi hiyo, kuendelea kushughulikia wale wote waliohusika na ukiukwaji wa haki za binadamu kwenye mauaji hayo ya mwaka 1994 yaliyosababisha mauaji ya watu takribani milioni moja na wengine kukimbilia katika nchi nyingine kama wakimbizi.

CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment