Right: The flamboyant and the magnificient Shaka excogitating heavily
during one of UVCCM marathon meetings!
(Pic by Global Publishers)
Written by abdisalum // 25/11/2013
Kuna madai kuwa Umoja wa Vijana Zanzibar (UVCCM) imepora kiwanja ambacho kinamilikiwa na ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar. Kiwanja hichi kipo eneno la Tunguu, na kilikusudiwa kujengwa ofisi inahohusika ama na madawa ya kulevya au wale vijana walioathirika na utumiaji wa madawa hayo, maarufu kama SOBER House.
Inasemekana kuwa kiwanja hichi kimewekwa kwa ajili ya shughuli za ofisi ya makamo wa kwanza wa Rais (VP1).
Madai haya ni ya muda mrefu sasa, lakini sulhu inakwenda chini kwa chini huku ofisi hiyo ya Makamo wa kwanza wa Rais, chini ya Maalim Seif Shariff Hamad kama Makamo wa Kwanza wa Rais, Zanzibar inaendelea kudai haki yake kupitia mfumo wa kupata haki – lakini UVCCM imepora ardhi hiyo ni kuigeuza mfumo wa mkaazi yasiyokuwa rasmi ya vijana (kambi!!).
Kesi hii tayari anaijua mwenyewe Mheshimiwa Rais, Dr.Shein, na Waziri wake wa Ardhi, Ramadhan Abdullah Shaban na watendaji wake. Mazungumzo yanaendelea, lakini Shaka Abdu Shaka ‘hawasikii la mtu’ yeye na timu yake.
Sijui itakuaje. OK, mimi sioni tatizo sana hilo mtu/ofisi moja kupora ardhi yake ya mwenzake hapa Zanzibar. Ni kawaida kabisa kwa siku hizi.
Lakini kufikia kupora ardhi ya ofisi ya VP1 au VP2, hii ni jeuri ya mwisho, na kwa kweli ni dalili ya ‘utovu wa adabu’ (disrespect), na hususan tunayoyasikia na kuyaona baina ya UVCCM Zanzibar na Maalim Seif Shariff na Chama chake. Matusi, kejeli, kebehi na dharau inayofanywa na kitoto hichi kama Shaka Abdu Shaka na wenzake dhidi ya ofisi ya serikali ya SMZ. Wao kama nani? Wao wana mamlaka gani ya kufika kote huko, bila kuchukuliwa hukumu au sheria iko wapi?
MKUU wa kitengo cha madawa kulevya Zanzibar naye pia ni mkereketwa kama wao UVCCM, sasa sijui itakuaje. Kama ni uzawa basi yeye zaidi kuliko akina Shaka. Hawa akina Maalim Seif tuwaache maana katika political context ya Zanzibar ni kama wageni tu, ‘vilemba vya Mascut’. Lakini ofisi ile pia wapo ASP, wazee wao pia walikuwa wana-ASP kindaki ndani; au wao sio…..halisi just kwa sababu wanafanya ofisi hiyo??
Chanzo: Mzalendo
No comments :
Post a Comment